- Kutoka kundi D ni Australia vs Turkey FIFA Kombe la Dunia 2026, Juni 14, 2026
- Imepita miaka 22 tangu wababe hawa wakutane H2H ilikuwa 2004 kwenye mchezo wa kirafiki
- Turkey ni bora eneo la kiungo huku Australia wakiwa imara kwenye matumizi ya mipira ya adhabu
Australia vs Turkey FIFA Kombe la Dunia 2026 mechi ya kundi D inatarajiwa kuchezwa Juni 14, 2026. Ni Uwanja wa BC Place Vancouver mchezo utapigwa. Wababe hawa watakuwa kazini kusaka pointi tatu saa 7:00 asubuhi kwa Afrika Mashariki lakini Canada itakuwa ni saa 9:00 usiku.
Fuatilia mwenendo wote wa mashindano ya Kombe la Dunia 2026; Ratiba, matokeo, mechi, magoli na habari za papo kwa papo kupitia SportPesa Blog na ushinde mamilioni kwa kubashiri kupitia odd kubwa za SportPesa.
Shinda mamilioni na Twenzetu Duniani ya SportPesa kwenye mechi Kombe la Dunia 2026
Twenzetu Duniani ya SportPesa inakuletea nafasi ya kushinda mamilioni kupitia odds kubwa za Kombe la Dunia 2026.Kwa mechi ya Australia vs Turkey, angalia odds, linganisha fomu ya uchambuzi wako, kisha weka mkeka wako kupitia SportPesa kwa kubonyeza picha hii chini. Beti kwa uwajibikaji.

SOMA HII: Ratiba FIFA Kombe la Dunia 2026 | Mechi zote 104 | Tarehe | Muda wa mechi | Uwanja utakaotumika
Taarifa muhimu za mechi
Mechi: Australia vs Turkey
Mashindano: FIFA Kombe la Dunia 2026
Kundi: D
Tarehe: Juni 14, 2026 saa 7:00 asubuhi kwa saa za Afrika Mashariki.
Takwimu muhimu Australia vs Turkey
Mataifa mawili Australia vs Turkey FIFA Kombe la Dunia 2026 yatakutana uwanjani yakiwa na takwimu tofauti. Australia wana uzoefu na wa kutosha kwenye mashindano makubwa. Hii ni mara ya ya 6 kushiriki Kombe la Dunia, 2022 walifika hatua ya 16 bora. Changamoto yao itakuwa kudhibiti ubunifu wa eneo la kiungo na kasi ya washambuliaji wa Uturuki.
Turkey wanarejea Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza tangu 2002. Kikosi kina wachezaji wenye uwezo binafsi na ubunifu.Arda Guler, mshambuliaji wa Juventus Kenan Yildiz na winga kutoka Galatasaray Kerem Akturkoglu ni wachezaji wanaoweza kuamua mchezo.
Mechi 5 zilizopita kwa Australia
Switzerland 1-1 Australia, mechi ya kirafiki
Mexico 1-0 Australia, mechi ya kirafiki
Australia 5-1 Curacao, FIFA Series
Australia 1-0 Cameroon, FIFA Series
Colombia 3-0 Australia, mechi ya kirafiki
Australia wamekuwa katika ubora hivi karibuni. Ushindi wa mfululizo kwenye mechi za FIFA Series ilikuwa ni Machi umeonesha ubora eneo la ushambuliaji. Mchezo wa kirafiki Juni dhidi ya Switzerland licha ya kufungana 1-1 bado imeonesha ukomavu kwenye ushambuliaji na mbinu ya kujilinda ikiwa ni silaha.
Matokeo ya mechi 5 zilizopita kwa Turkey
Turkey 2-1 Venezuela, mechi ya kirafiki
Turkey 4-0 North Macodonia, mechi ya kirafiki
Kosovo 0-1 Turkey, kufuzu Kombe la Dunia
Turkey 1-0 Romania, kufuzu Kombe la Dunia
Hispania 2-2 Turkey, kufuzu Kombe la Dunia
Turkey imefuzu FIFA Kombe la Dunia 2026 ikiwa haijafungwa katika mechi zilizopita. Inajumuisha ushindi mechi 4 na sare 1. Mchezo dhidi ya Hispania walionyesha ubabe wakitokea nyuma na kuweka mzani sawa.
Rekodi ya timu hizi zilipokutana
Rekodi zinaonyesha ni mara 2 kwenye mechi za kirafiki 2004. Turkey ilipata ushindi mechi zote kwa 3-1 na 1-0. Ni miaka 22 imepita tangu wakutane uwanjani.
Turkey kikosi kinachotarajiwa kuanza

SOMA HII: USA vs Paraguay FIFA Kombe la Dunia 2026 | H2H| Vikosi |SportPesa Blog

Bayindir, Zeki, Celick, Demiral, Soyuncu, Kadioglu, Calhanoglu, Kaan Ayhna, Barris, Alper Yilmaz, Arda Guler. Kikosi rasmi kitathibitishwa kabla ya mchezo.
Kikosi kinachotarajiwa kuanza Australia
Ryan, Souttar, Degenek, Burgess, Geria, Irvine, Metcalfe, Boston, Irankunda, Leckie na Mabil. Kikosi rasmi kitathibitishwa karibu na muda wa mchezo.
Utabiri
Turkey anapewa nafasi kubwa kupata ushindi wa magoli 2-1. Uimara wa kikosi na ubunifu uliopo unawapa nguvu kuibuka na pointi muhimu. Uwepo wa Arda Guler, Kenan Yildiz na Kerem unaongeza morali ya ushindi. Mechi 5 bila kufungwa kunadhihirisha uimara wa timu. Australia wanapewa nafasi kushinda ikiwa watapata faida hasa katika mipira ya adhabu.Huu ni mtazamo wa kiuhariri, si hakikisho la matokeo.
Austaralia vs Turkey itachezwa lini?
Mechi ya Australia vs Turkey itachezwa Juni 14, 2026
Austaralia vs Turkey ni kundi gani?
Austaralia vs Turkey ni kundi D kwenye FIFA Kombe la Dunia
Austaralia vs Turkey itachezwa uwanja gani”
Austaralia vs Turkey itachezwa Uwanja wa BC Place, Vancouver, Canada
Austaralia vs Turkey zimewahi kukutana?
Ndio timu hizi zimewahi kukutana mara mbili kwenye mechi za kirafiki 2004 na Turkey alishinda mechi zote mbili.
Hitimisho
Miongoni mwa mchezo wakuvutia ni Australia vs Turkey FIFA Kombe la Dunia 2026. Timu hizi zimekuwa zinapishana eneo la ubora, Turkey wakiwa imara katika ushambuliaji na ulinzi, Australia ni imara katika kutumia mipira ya adhabu.

