- Ratiba ya Sherehe za ufunguzi FIFA Kombe la Dunia 2026 zimefika rasmi. Usiku huu watu wote Duniani watashuhudia kufunguliwa rasmi kwa mashindano hayo makubwa duniani.
- Mwaka huu Kombe la Dunia linafanyika kwa ushirikiano wa maandalizi ya nchi 3, ambazo ni; Marekani (USA), Canada na Mexico.
- Makala hii inakuletea ratiba ya ‘show’ za wasanii wote wakubwa watakaotumbuiza kwenye sherehe za ufunguzi, ambazo kwa mara ya kwanza zitakuwa 3.
- Kila nchi mwandaaji itafanya shoo yake ya ufunguzi, huku wasanii wakubwa kama Shakira, Burna Boy, Madonna, Katty Perry
Usiku wa Sherehe za FIFA Kombe la Dunia 2026 umefika. Usiku huu watu wote Duniani watashuhudia kufunguliwa rasmi kwa mashindano hayo makubwa duniani. Mara ya mwisho mashindano ya Kombe la Dunia yalifanyika nchini Qatar mwaka 2022, mwaka huu Kombe la Dunia linafanyika kwa ushirikiano wa maandalizi ya nchi 3, ambazo ni; Marekani (USA), Canada na Mexico. Makala hii inakuletea ratiba ya ‘show’ za wasanii wote wakubwa watakaotumbuiza kwenye sherehe za ufunguzi, ambazo kwa mara ya kwanza zitakuwa 3.
Fuatilia mwenendo wote wa mashindano ya Kombe la Dunia 2026; Ratiba, matokeo, mechi, magoli na habari za papo kwa papo kupitia SportPesa Blog na ushinde mamilioni kwa kubashiri kupitia odd kubwa za SportPesa.
Shinda mamilioni na Twenzetu Duniani na SportPesa kwenye mechi Kombe la Dunia 2026
Twenzetu Duniani ya SportPesa inakuletea nafasi ya kushinda mamilioni kupitia odds kubwa za mechi za Kombe la Dunia. Ili kushinda beti mechi ya Ufunguzi kati ya Mexico vs South Afrika kwa kubonyeza picha hii chini

Kuhusu Ratiba ya Sherehe za ufunguzi FIFA Kombe la Dunia 2026
Mexico leo Juni 11, 2026 saa 20:00 BTS

Kwa mara ya kwanza katika historia, mashindano hayo yatakuwa na sherehe 3 za ufunguzi yaani kila taifa litafanya shoo moja ya ufunguzi. Leo Juni 11, 2026 mwimbaji maarufu wa muziki wa pop kutoka Colombia, Shakira atatumbuiza wimbo wake rasmi wa Kombe la Dunia 2026 uitwao ‘Dai Dai’. Hii ni katika sherehe za ufunguzi wa mashindano hayo nchini Mexico.
Shakira atafanya ‘pafomansi’ hiyo akishirikiana na Burna Boy, katika dimba la Estadio Azteca jijini Mexico City. Hii itakuwa dakika chache, kabla ya mechi ya ufunguzi kati ya Mexico na South Africa. Mechi hii itapigwa majira ya saa 20:00 BST, ikumbukwe Dai Dai ni kauli ya lugha ya Kiitaliano, yenye maana ya “twende” au “haya twende”.
Ukiachana na Shakira na Burna Boy, Nyota wengine wa muziki watakaotumbuiza ni pamoja na staa wa reggaeton kutoka Colombia, J Balvin. Wengine ni pamoja na mwimbaji na mtunzi wa nyimbo kutoka Afrika Kusini, Tyla, Andrea Bocelli na Ejae.
SOMA HII PIA: Sheria mpya za mechi Kombe la Dunia 2026 zashtua! Nini kimebadilishwa?
Canada tarehe 12 Juni 2026 saa 20:00 BST.
Nchini Canada, waimbaji na watunzi wa nyimbo Michael Bublé na Alanis Morissette wataongoza sherehe za ufunguzi, katika dimba la BMO Field jijini Toronto. Hii ni muda mchache kabla ya Canada kucheza dhidi ya Bosnia and Herzegovina siku ya Ijumaa, tarehe 12 Juni 2026 saa 20:00 BST.
Marekani tarehe 13 Juni 2026
Nchini Marekani, nyota wa muziki wa pop Katy Perry na rapa Future watatumbuiza kabla ya Marekani kucheza dhidi ya Paraguay katika dimba la SoFi Stadium jijini Los Angeles. Kutokana na utofauti wa masaa mechi hii itachezwa siku ya Ijumaa kwa baadhi ya nchi na Jumamosi kwa saa za Afrika Mashariki. Kwa majira ya BST itakuwa sawa na saa 02:00 BST.
SOMA HII ZAIDI: Ratiba FIFA Kombe la Dunia 2026 | Mechi zote 104 | Tarehe | Muda wa mechi | Uwanja utakaotumika
Je, bado hujashinda pesa? Cheza aviator ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa
Changamka! sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi zaidi ya Milioni 800 muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Jipatie nafasi ya kujishindia milioni 800 na Aviator
Ratiba ya sherehe za Fainali

Shakira, pamoja na Madonna na kundi la K-pop BTS, pia watakuwa waimbaji wakuu wa burudani ya mapumziko ya katikati ya mchezo (half-time show) ya fainali. Shoo hii itafanyika kwa mtindo wa Super Bowl, wakati wa fainali ya Kombe la Dunia 2026. Hii itakuwa ni jumapili ya tarehe 19 Julai.
Hitimisho

Sherehe za ufunguzi FIFA Kombe la Dunia 2026, zilisubiliwa kwa hamu kubwa na hatimaye zimewasili. Ni siku takribani 40 za mfululizo ya mechi za mashindano makubwa zaidi, kwa ngazi ya soka duniani. Nani atafanya makubwa katika shoo yake? Ni suala la kusubiri na kuona.

