- Mzambia Clatous Chama aongeza presha Yanga SC vita ya ubingwa
- Takwimu za Mei NBC Premier Leageu kuna kona ya Chama, goli la Chama dhidi ya Mashujaa FC
- Simba SC macho yote kwenye kupunguza pointi dhidi ya mabingwa watetezi
Kiungo wa Simba SC, Clatous Chama aongeza presha Yanga SC vita ya kuwania ubingwa. Hii inatokana na magoli mawili aliyofunga Mei 14, 2026 dhidi ya Mashujaa FC ya Kigoma. Simba SC imekutana mara mbili na Mashujaa FC na imeshinda mechi zote nje ndani. Mchezo uliopita ubao wa Uwanja wa Lake Tanganyika ulisoma Mashujaa FC 0-3 Simba SC, goli moja lilifungwa na Seleman Mwalimu.
SOMA HII: Clatous Chama usajili wake umelipa | Takwimu na timu alizocheza CAF Champions League
Bado hujashinda pesa? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa
Ni zamu yako sasa, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Mzambia Clatous Chama aongeza presha Yanga SC NBC Premier

Nyota mwenye miaka 34, Clatous Chama aongeza presha Yanga SC kwenye ushindi dhidi ya Mashujaa FC. Mnyama amepunguza gap la pointi dhidi ya vinara ambao wana pointi 54 ikiwa ni tofauti ya pointi 2. Timu zote hizi za Kariakoo zimecheza jumla ya mechi 23.
Mbio za ubingwa zimeanza upya kwani awali kulikuwa na tofauti ya pointi 5. Chama alianza mapema kufunga ndani ya dakika 5 za mwanzo akifunga goli kwa pigo la kona. Raia huyo wa Zambia amefikisha magoli 8 kwenye ligi akiwa na matumaini ya kufukuzia kiatu cha ufungaji bora.
Kinara kwenye eneo la ufungaji ni Feisal Salum ambaye ana magoli 11. Prince Dube wa Yanga SC anafuata akiwa amefunga 9. Hivyo mbali na presha kwenye eneo la kuwania ubingwa kuna vita nyingine tuzo ya ufungaji bora.
Takwimu za Clatous Chama Mei NBC Premier League

SOMA HII: Kariakoo Dabi-Goli la Clatous Chama gumzo kubwa | Ahmed Ally atamba | SportPesa Blog

Clatous Chama Mei amekuwa katika ubora uwanjani ndani ya NBC Premier League. Kuna uwezekano mkubwa akachaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi. Amekuwa akifunga na kutoa pasi za magoli.
| Mechi | Matokeo | Magoli ya Chama | Man of the Match |
|---|---|---|---|
| Simba SC 2-2 Yanga SC | Sare | 1 | 1 |
| Simba SC 1-0 JKT Tanzania | Ushindi | 1 | 2 |
| Simba SC vs Tanzania Prisons | Ushindi | 1 | 3 |
| Mashujaa FC 0-3 Simba SC | Ushindi | 2 | 4 |
Simba SC macho kwenye kupunguza deni kwa Yanga SC
Katika mechi zote zilizobaki mnyama hesabu kubwa ni kupata pointi kulipa deni dhidi kwa Yanga SC. Mpaka sasa timu zote zimecheza mechi 23 zikisalia mechi 7. Mabingwa watetezi wa NBC Premier League wana mataji wa pointi 2 mkononi kwa sasa.
Seleman Matola, kocha msaidizi wa Simba SC amebainisha kuwa kila mchezo ni muhimu kupata ushindi.Kocha huyo ameongeza kwa kusema kila mechi ni ngumu. Aliwaomba mashabiki kuendelea kujitokeza kwa wingi.
“Kwenye mechi zetu ambazo zimebaki tuna kazi kubwa kufanya kutafuta matokeo. Wachezaji wapo tayari na tunaendelea kupambana. Kikubwa ni kushirikiana na mashabiki kujitokeza kwa wingi,”.
SOMA HII: Usajili wa Chama Simba SC washtua! Mayele, Kagere, Okwi wafunguka Mazito
Hitimisho
Ni Clatous Chama aongeza presha Yanga SC kutokana na kuwa mhimili wa ushindi. Jumla amehusika kwenye magoli 12 akifunga 8 na kutoa pasi 4 za magoli. Je ataendelea katika ubora huo mechi zijazo? Endelea kufuatilia SportPesa Blog kwa taarifa na matokeo.

