- Mabingwa watetezi Yanga SC wanakwenda kuwakabili Singida Black Stars live Mei 22, 2026 Uwanja wa KMC Complex
- SportPesa Blog tumekuletea taarifa, h2h za mtanange huo mkali
- Yanga SC imepata ushindi kwenye mechi 7 kati ya 9 walizokutana ndani ya NBC Premier League
Yanga SC vs Singida Black Stars NBC Premier League ni mchezao ujao Mei 22, 2026 kwa wababe hawa kukutana. Uwanja wa KMC Complex utashuhudia mchuano mkali kwa wanaume 22. Mchezo uliopita Uwanja wa Airtel, matokeo yalikuwa Singida Black Stars 0-3 Yanga SC. Head 2 head kwenye mechi walizokutana Yanga SC imekuwa ikipata ushindi mara nyingi zaidi.
SOMA HII: Ratiba ya mechi zilizobakia za Yanga SC NBC Premier League 2025/26 | SportPesa Blog
Cheza na ushinde sasa na ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni muda huu
Hujashinda na kindege cha SportPesa? Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kubashiri SportPesa bonyeza picha hii chini.

Yanga SC vs Singida Black Stars NBC Premier League saa 10:00 jioni

SOMA HII: Uongozi wa Yanga SC umeweka wazi vita ya MVP/ Pacome na Jean Ahoua kitaumana

Kituo kinachofuata ni Yanga SC vs Singida Black Stars NBC Premier saa 10:00 jioni burudani itaendelea. Matokeo ya hivi punde kwa wababe hawa walipokutana pointi tatu zilikuwa kwa mabingwa watetezi. Je mchezo huu nani atavuna pointi tatu muhimu?
Yanga SC inakwenda kuwakabili Singida Black Stars baada ya kutoka kupoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Dodoma Jiji FC. Ubao wa Uwanja wa Airtel Mei 13, 2026 ulisoma Dodoma Jiji FC 3-2 Yanga SC hivyo hasira za kupoteza zinawaka kwa wachezaji wa timu zote. Mabingwa watetezi kupoteza mchezo uliopita na Singida Black Stars kupoteza mchezo wa mzunguko wa kwanza.
H2H Yanga SC vs Singida Black Stars NBC Premier League

05/03/2026, Singida Black Stars 0-3 Yanga SC
17/02/2025, Yanga SC 2-1 Singida Black Stars
30/10/2024, Singida Black Stars 0-1 Yanga SC
11/03/2024, Yanga SC 5-0 Singida Black Stars
04/10/2023, Singida Black Stars 2-1 Yanga SC
16/01/2023, Yanga SC 1-0 Singida Black Stars
29/11/2022, Singida Black Stars 2-1 Yanga SC
15/07/2021, Yanga SC 2-0 Singida Black Stars
23/12/2020, Singida Black Stars 0-3 Yanga SC
Msimamo wa Yanga SC vs Singida Black Stars
| Nafasi | Timu | Mechi | Ushindi | Sare | Poteza | Magoli ya Kufunga | Pointi |
|---|---|---|---|---|---|---|---|
| 1 | Yanga SC | 23 | 16 | 6 | 1 | 52 | 54 |
| 4 | Singida Black Stars | 23 | 11 | 5 | 7 | 30 | 38 |
Tofauti ya Yanga SC vs Singida Black Stars ni pointi 16. Wananchi safu yao ya ushambuliaji ni kali ikiwa na magoli 52 huku wapinzani wakiwa na magoli 30. Kwenye kupoteza mechi Yanga SC imepoteza mchezo mmoja pekee.
Hitimisho
Ni vita kali Yanga SC vs Singida Black Stars NBC Premier League. Mabingwa watetezi wapo kazini kuwania taji lao na wageni wanapiga hesabu kumaliza 4 bora. Nani ataibuka mbabe kwenye mtanange huu? Endelea kufuatilia SportPesa Blog kwa taarifa za hivi punde na matokeo.

