- Kivumbi kitatatimka Simba SC vs TRA United NBC Premier League kwenye msako wa pointi tatu muhimu uwanjani.
- Dimitar Pantev kwenye kazi nyingine ugenini kwa mara ya kwanza baada ya kubeba mikoba ya Fadlu Davids.
- TRA United kupitia Ofisa Habari Chritina Mwagala yatamba kuwapa tabu wapinzani katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.
Simba SC vs TRA United NBC Premier League ni mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora. Timu zote mbili kwenye mechi zao zilizopita hakuna iliyopata ushindi. TRA United ilicheza na Mashujaa mchezo wa ligi na Simba SC ilicheza na Nsingizini Hotspurs Ligi ya Mabingwa Afrika. Licha ya kila mmoja kuwa nyumbani matokeo yalikuwa 0-0.
SOMA HII: Che Malone wa Simba SC aanza kazi kwa Waarabu | Mrithi wake huyu hapa | Rekodi, magoli
Cheza na ushinde sasa na ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni muda huu
Hujashinda na kindege cha SportPesa? Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kubashiri SportPesa bonyeza picha hii chini.

Simba SC vs TRA United NBC Premier League mtihani wa Pantev kwenye ligi

Simba SC vs TRA United NBC Premier League utakuwa ni mtihani wa kwanza kwa Dimitar Pantev kwenye ligi. Mrithi wa mikoba ya Fadlu Davids amekiongoza kikosi kwenye mechi mbili za Ligi ya Mabingwa Afrika. Kete ya kwanza ndani ya ligi itakuwa ugenini dhidi ya TRA United.
Katika mechi hizo mbili, Simba SC ilishinda mchezo mmoja wa ugenini kwa magoli 3-0. Mchezo wa pili wakiwa nyumbani walilazimisha sare. Pantev kazini ugenini kwenye mechi ya ligi.
Mechi 5 za TRA United
TRA United 0-0 Mashujaa FC
Pamba Jiji 0-0 TRA United
TRA United 2-2 Dodoma Jiji FC
Coastal Union 1-1 TRA United
Azam FC 5-0 TRA United.
H2H
Februari 2,2025, TRA United 0-3 Simba SC, Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.
Agosti 18,2024- Simba SC 3-0 TRA United, Uwanja wa KMC Complex
Mei 6,2024- Simba SC 2-0 TRA United, Uwanja wa Azam Complex
Februari 6,2024- TRA United 0-4 Simba SC, Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.
SOMA HII: Simba yaanza ligi kwa mkwara mzito, yaichapa Tabora 3-0

Mechi 5 za Simba SC
Oktoba 26,2025 Simba SC 0-0 Nsingizini Hotspurs. Ligi ya Mabingwa Afrika.
Nsingizini Hotspurs 0- 3 Simba SC, Oktoba 19,2025. Ligi ya Mabingwa Afrika.
Oktoba Mosi 2025, Simba SC 3-0 Namungo FC, mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Septemba 28 2025, Simba SC 1-1 Gaborone United, Ligi ya Mabingwa Afrika.
Septemba 25 2025, Simba SC 3-0 Fountain Gate mchezo wa Ligi Kuu Bara.
Christina Mwagala Ofisa Habari wa TRA United maoni yake
Ofisa Habari wa TRA United, Christina Mwagala amesema kuwa wapo tayari kwa mchezo huo. Aliongeza kuwa maandalizi yalianza muda mrefu jambo linalowafanya waamini kwamba watapata pointi tatu. Amewaomba mashabiki kununua tiketi mapema.
“Tupo tayari kwa mchezo na kila kitu kipo sawa. Mashabiki wanunue tiketi kwa wingi na kujitokeza uwanjani mapema. Uwepo wao ni muhimu na mchezo utakuwa mgumu lakini wachezaji wapo tayari kwa mchezo,”.
Ikumbukwe kwamba TRA United awali ilikuwa inaitwa Tabora United. Kwa sasa imebadilisha jina inaitwa TRA United. Makao yake yapo palepale Tabora mji wenye asali na maziwa.
Kikosi cha TRA United kinachotarajiwa kuanza vs Simba SC
Noel, Kapama, Christopher, Makame, Kombo, Joseph, Lusajo, Adam, Chuku, Lazarus, Chilunda.
Kikosi cha Simba SC kinachotarajiwa vs TRA United

Mlinda mlango
Yakoub Suleman
Mabeki
Chamou
Mligo
David Kameta
De Reuck
Viungo
Yusuph Kagoma
Joshua Mutale
Ellie Mpanzu
Morice Abraham
Jean Ahoua
Mshambuliaji
Jonathan Sowah
Hitimisho
Simba SC vs TRA United NBC Premier League mnyama amekuwa akipewa nafasi kubwa kupata ushindi. Je TRA United itakubali kukosa ushindi kwa mara ya tano mfululizo mbele ya mnyama? Majibu yatatolewa uwanjani baada ya mchezo.

