- Abdihamid Moalin kocha msaidizi ameanza kazi rasmi mara baada ya kuwasili Tanzania
- Wachezaji wanne wa Yanga SC warejea kazini, Chadrack Boka, Bacca, Edmund John kazi inaendelea
- Depu taarifa yake mpya imetolewa na uongozi kuhusu maendeleo ya hali yake
- Kituo kinachofuata kwa Yanga SC ni Aprili 4, 2026 vs Tanzania Prisons
Wachezaji wanne wa Yanga SC warejea kazini Prince Dube, Chadrack Boka, Ibrahim Bacca na Edmund John. Nyota hao walikuwa hawapo fiti wameanza mazoezi tayari kwa mechi za ushindani. Mchezo ujao kwa mabingwa watetezi ni Aprili 4, Yanga SC vs Tanzania Prisons, Uwanja wa KMC Complex.
SOMA HII: Beki Ibrahim Bacca wa Yanga SC amefungiwa mechi 5 na TPLB
Je, bado hujashinda pesa? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa
Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Wachezaji wanne wa Yanga SC warejea kazini, morali yaongezeka

Ipo wazi wachezaji wanne wa Yanga SC warejea kazini tayari kuendelea na mapambano. Ni nyota muhimu eneo la ulinzi wakiongozwa na Ibrahim Bacca na katika eneo la ushambuliaji Prince Dube. Katika mechi dhidi ya Mtibwa Sugar walikosekana na ubao ulisoma 1-1.
Ali Kamwe, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Yanga SC amesema mipango inakwenda vizuri. Kuhusu wachezaji kurejea na kuanza mazoezi ni taarifa njema. Aliongeza kuwa Depu bado ataendelea kuwa katika uangalizi wa madaktari
“Kuhusu Prince Dube, Chadrack Boka, Ibrahim Bacca na Edmund John hawa tayari wametoka chumba cha daktari. Wameanza mazoezi na walianza na program ya gym. Depu bado yupo kwenye chumba cha daktari na atarejea uwanjani hivi karibuni.
“Hatutaki kumuharakisha Depu kwa kuwa tunahitaji kuona anarejea akiwa bora. Baada ya wiki moja hivi tunaamini atakuwa imara. Hapo atarejea kwenye mazoezi kwa ajili ya mechi zijazo,”.
SOMA HII: Depu mtambo wa mabao: Ataziba pengo la Mayele? Takwimu, rekodi zake hizi hapa, zatikisa bongo

Kikosi cha Yanga SC charejea kambini

Aprili 30, 2026 kikosi cha Yanga SC kilirejea kambini na kuanza mazoezi. Chini ya Kocha Mkuu, Pedro Goncalvels kazi inaendelea. Kwenye uwanja wa mazoezi wachezaji walikuwa wakifundishwa mbinu mbalimbali za ushindi.
Miongoni mwa wachezaji waliokuwa katika eneo la mazoezi ni Bacca, Boka, Pacome Zouzoua, Hussen Masalanga, Aziz Andabwile. Mchezo ujao kwa Yanga SC watakuwa nyumbani wakiwakabili Tanzania Prisons. Katika mzunguko wa kwanza walipata ushindi wa goli 1-0.
SOMA HII: Taarifa mpya Depu na Boka wa Yanga SC haifurahishi/ Orodha ya wachezaji majeruhi

Kocha mpya ameanza kazi

Baada ya kumtambulisha Abdihamid Moalin, tayari ameanza kazi. Siku ya kwanza kuwanoa wachezaji ilikuwa ni Aprili 30, 2026. Kocha huyo msaidizi alikutana na wachezaji wa timu hiyo Uwanja wa KMC Complex.
Miongoni mwa wachezaji ambao aliwahi kufanya nao kazi ni Kibwana Shomari, Bakari Nondo, Ibrahim Bacca. Ataendelea kufanya nao kazi kwa kuwa bado wapo ndani ya kikosi. Ikumbukwe kwamba 2024/25 alikuwa ni Mkurugenzi wa Ufundi kwenye kikosi hicho.
Ratiba ya Yanga SC NBC Premier League
Yanga SC vs Tanzania Prisons, Aprili 4,2026
Pamba Jiji FC vs Yanga SC, Aprili 8,2026
Yanga SC vs Mbeya City, Aprili 16,2026
KMC Fc vs Yanga SC, Aprili 16,2026
Yanga SC vs Coastal Union, Aprili 30,2026
Simba SC vs Yanga SC, Mei 3,2026
Dodoma Jiji FC vs Yanga SC, Mei 6, 2026
Yanga SC vs Dodoma Jiji FC, Mei 15,2026
Yanga SC vs Namungo FC, Mei 19,2026
Mashujaa FC vs Yanga SC, Mei 23,2026
SOMA HII: Yanga SC hawana utani wamerejea kazini 2025/26/ Orodha ya wachezaji waliopo AFCON

Hitimisho
Wachezaji wanne wa Yanga SC warejea kazini baada ya kuwa nje kwa muda. Mshambuliaji Depu anatarajiwa kurudi hivi karibuni kuendelea na kazi. Mchezo unaofuata kwa mabingwa watetezi ni dhidi ya Tanzania Prisons.

