Simba SC inamfuatilia Salim AdamsSalim Adam
  • Simba SC inamfuatilia Salim Adams kiungo mshambuliaji wa Medeama SC ya Ghana
  • Chobwedo atajwa kuhitajika na mnyama, Yanga SC kutoka TRA United
  • Kelvin Nashon wa Pamba Jiji FC mapema atajwa kumalizana na mabosi wa Msimbazi

Inaelezwa kuwa Simba SC inamfuatilia Salim Adams wa Medeama SC raia wa Ghana. Kiungo huyo anacheza katika Ligi Kuu ya Ghana amekuwa na kiwango chakuvutia. Mbali na huyo mnyama anatajwa kuwinda pia saini ya Ramadhan Ramadhan maarufu kwa jina la Chobwedo kiungo wa TRA United.

TAARIFA KUHUSU USAJILI: Usajili wa Chama Simba SC washtua! Mayele, Kagere, Okwi wafunguka Mazito

Je, bado hujashinda pesa? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa

Ni zamu yako sasa, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Aviator game jackpot banner TSh 800 Million prize

Simba SC inamfuatilia Salim Adams kiungo mshambuliaji

Simba SC inamfuatilia Salim Adams
Salim Adams.

Tetesi zinaeleza kuwa Simba SC inamfuatilia Salim Adams kiungo mshambuliaji mwenye miaka 22. Rekodi zinaonyesha kuwa akiwa Medeama SC amekuwa akifuatiliwa na timu nyingi Afrika. Hiyo inatokana na kiwango chake akiwa uwanjani.

Takwimu za Adams zinaonyesha amecheza mechi 25, amefunga magoli tisa, ametoa pasi moja ya goli. Ameshinda tuzo saba za mchezaji bora wa mechi, (Man of The Match). Anasifika kuwa na uwezo wa kubadili matokeo pale anapopata nafasi.

Taarifa kutoka vyanzo vya karibu zinaeleza kuwa Simba SC wanaendelea kumfuatilia kwa karibu mchezaji huyo. Mnyama anahitaji kuimarisha kikosi chake kwa msimu ujao. Msimu huu eneo hilo yupo Clatous Chama aliyesajiliwa akitokea Singida Black Stars.

Bado hakuna ofa rasmi iliyothibitishwa mpaka sasa. Ikiwa Simba SC watakosa saini yake uwezekano wa kubaki hapo ni mdogo. Hiyo inatokana na uwezo alionao na timu zilizo nje ya Afrika Magharibi kutajwa kuwania saini yake.

SOMA HII: Simba SC kufanya usajili mkubwa | Maeneo yatakayoboreshwa | Mo atoa tamko zito | Ahmed atamba

Aviator game jackpot banner TSh 800 Million prize

Chobwedo atajwa mitaa ya Msimbazi

Simba SC inamfuatilia Salim Adams
Chobwedo kiungo wa TRA United.

Mbali na Adams raia wa Ghana inatajwa kuwa Simba SC inamfuatilia Chobwedo. Kiungo huyo amekuwa katika ubora NBC Premier League jambo linalofanya timu nyingi kumfuatilia.  Inaelezwa kuwa Simba SC na Yanga SC zinahitaji huduma ya kiungo huyo.

Chobwedo kwenye mchezo dhidi ya Yanga SC alitwaa tuzo ya mchezaji bora. Baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid ulisoma TRA United 0-0 Yanga SC. Pia walipokutana na Simba SC alikuwa na kiwango bora.

Kelvin Nashon mapema atajwa kusaini Msimbazi

Simba SC inamfuatilia Salim Adams
Nashon

Inaelezwa kuwa kiungo Kelvin Nashon wa Pamba Jiji FC amemalizana na mabosi wa Msimbazi. Taarifa zimeeleza kwamba kabla ya dirisha la usajili kufunguliwa mnyama aliamua kufanya mazungumzo na mchezaji na uongozi. Ni miaka miwili inatajwa mkataba aliopewa kiungo huyo.

Bosi Simba SC afafanua kuhusu usajili

Crescentius Magori, Mwenyekiti wa Bodi ya Simba SC hivi karibuni alibainisha kuwa hawataki kurudia makosa msimu ujao. Kuhusu usajili alibainisha kuwa kuna hatua ambazo wameanza kuzifanya. Aliwaomba mashabiki kuwa watulivu na kuinga mkono timu hiyo.

“Simba SC ni timu kubwa ambayo inafanya vitu vyake kwa vitendo. Mashabiki ni muhimu kuwa watulivu ili na kuinga mkono timu. Kuelekea msimu ujao tayari kuna taratibu za usajili tumeanza kuzifanya,”.

SOMA HII: Mapya sakata la Jonathan Sowah amerejeshwa Simba SC na kupelekwa U 20

Hitimisho

Simba SC inamfuatilia Salim Adams kuelekea usajili wa dirisha kubwa la msimu wa 2026/27.Mbali na kiungo huyo Chobwedo naye inaelezwa anafuatiliwa. Je unadhani wachezaji hawa watapata nafasi kikosi cha kwanza usajili wao ukikamilika?

Share this: