Mwamuzi wa Morrocco Hamza El FaruqMwamuzi wa Morrocco Hamza El Faruq
  • Je, Waamuzi Simba SC vs Yanga SC wanatoka Morocco? Ni swali gumu ambalo mashabiki wanajiuliza kuelekea mchezo mkali wa Simba SC vs Yanga SC
  • Mchezo huu wa Ligi Kuu Bara (NBC Premier League), utapigwa Jumapili tarehe 3/5/2026, katika Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Dar es Salaam.
  • Hii itakuwa mara ya 2 timu hizi kukutana ndani ya wiki hii, ambapo jana Jumatano walivaana katika Fainali ya Muungano Cup 2026 na Simba SC kuibuka bingwa kwa matokeo ya Yanga SC 0-1 Simba.
  • Kamati ya Waamuzi yatoa tamko zito kuhusu kuleta waamuzi kutoka Morocco.

Taarifa ya Waamuzi Simba SC vs Yanga SC kutoka Morocco kuamua mchezo wa Kariakoo Dabi kati ya Jumapili 3/5/2026, imezidi kuwa gumzo. Hii ni kuelekea mchezo huo mkali wa Ligi Kuu Bara (NBC Premier League), ambapo Simba SC wataikaribisha Yanga SC. Mchezo huu ambao utapigwa kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Dar es Salaam utatoa taswira ya ubingwa msimu huu. Hii itakuwa mara ya pili kwa timu hizo kukutana wiki hii, mara baada ya jana Jumatano Simba SC kuibuka mabingwa wa Muungano Cup 2026 kwa matokeo ya Yanga 0-1 Simba SC.

Fuatilia mwenendo wote wa mashindano ya Ligi Kuu Bara ‘NBC Premier League’ 2025/26; Ratiba, matokeo, mechi, magoli na habari za papo kwa papo kupitia SportPesa Blog.

Je, wajua? Unaweza kushinda mpaka Shilingi Milioni 800 na SportPesa

Wengi tayari wamevuna mamilioni kupitia mchezo wa Kindege yaani ‘Aviator’ ya SportPesa. Wewe unasubiri nini? Nafasi ni yako cheza Aviator na kushinda mpaka Shilingi Milioni 800 sasa kwa kubonyeza picha hii chini.

SportPesa Aviator Challenge
SportPesa Aviator Challenge: Paisha kindege ushinde mpaka zaidi Milioni 800

Kuhusu Waamuzi Simba SC vs Yanga SC kutoka Morocco kusimamia mechi

Simba SC vs Yanga SC kupigwa Uwanja wa Meja Isamuhyo
Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo

Taarifa ambayo imekuwa gumzo, ambayo inasubiri uthibitisho wa Bodi ya Ligi Tanzania ni uamuzi wa kuwaleta waamuzi wa Morocco kusimamia mchezo huu mkubwa. Tetesi za taarifa hiyo zimeeleza kuwa, uamuzi huo umefikiwa ili kuhakikisha kunakuwa na uendeshaji bora wa mchezo huo. Katika hatua nyingine, baadhi ya majina ya waamuzi wa Morocco yanayotajwa kupewa mchezo huo ni; Mwamuzi Hamza El Faruq, Mwamuzi Lahsene Azkawi, Mwamuzi Hamza El Nasri, na Mwamuzi Mostafa Kchaaf.

SOMA HII PIA: Mwamuzi Yanga SC vs Simba SC balaa! kuna kadi nyekundu leo?

Kamati ya Waamuzi wa Ligi Kuu ya NBC watoa tamko

Baadhi ya waamuzi bora wa Tanzania
Baadhi ya waamuzi bora wa Tanzania

Wakati tetesi hizo zikizidi kupamba moto, Kamati ya Waamuzi kupitia kwa Mwenyekiti wake, Soud Abdi akizungumza na Chombo kimoja cha Habari amesema: “Uamuzi wa kuwatumia waamuzi wa kigeni unalenga kuongeza uwazi, na kuondoa malalamiko yanayojitokeza mara kwa mara kwenye michezo mikubwa ya ndani. Kwa uzoefu wao, waamuzi wa kigeni wanaopewa mechi hizi, wanatarajiwa kuhakikisha mchezo unaendeshwa kwa haki na kufuata sheria zote za soka.

“Kwa hali hiyo, matarajio ya wengi ni kuona dabi yenye ushindani mkali lakini yenye uamuzi wa haki. Pia hii inalenga ubora wa timu uwanjani, kuamua matokeo. Hali hii hisababisha kupungua kwa malalamiko na mijadala baada ya mchezo kuisha.

“Mpaka sasa bado hatujatoa taarifa rasmi ya Waamuzi ambao watasimamia mechi hii, na wakati utakapofika basi tutaweka wazi. Kanuni za ligi yetu zinaturuhusu kutumia Waamuzi wowote, ambao watatoa matokeo bora ya uamuzi wa mchezo. Na waamuzi wa kigeni waliosimamia mechi kadhaa, wameonekana kupunguza sana malalamiko, lakini kama Taifa pia tuna Waamuzi wengi bora ambao wanaweza kusimamia mechi hizi kubwa.”

SOMA HII ZAIDI: Yanga SC vs Simba SC taarifa muhimu kuhusu waamuzi wa mchezo Juni 15 2025 viingilio kutolewa

Simba SC vs Yanga SC, historia ya h2h

Yanga SC (0) vs Simba SC (1) Fainali Muungano Cup 2026
Seleman Mwalimu

Katika miaka ya karibuni timu hizi zimekutana katika michezo 23 ya mashindano yote, Simba SC imeshinda mechi 4 tu, Yanga SC wao wameshinda mechi 8 ikiwemo mechi 6 mfululizo. Mechi 11 zilizosalia ziliisha kwa matokeo ya sare. Jumla ya mabao 45 yamefungwa katika mechi hizo kama jedwali hapa chini linavyoonyesha;

KipengeleSimba SCYoung Africans (Yanga)
Mikutano 23 ya Mashindanoushindi 4ushindi 8
Sare1111
Jumla ya Mabao ya Kufunga1827
TareheMashindanoMatokeo
29 Aprili 2026Kombe la Muungano (Fainali)Simba 1–0 Yanga
1 Machi 2026Ligi Kuu Tanzania BaraYanga 0–0 Simba
25 Juni 2025Ligi Kuu Tanzania BaraYanga 2–0 Simba
19 Oktoba 2024Ligi Kuu Tanzania BaraSimba 0–1 Yanga
8 Agosti 2024Ngao ya Jamii (Community Shield)Yanga 1–0 Simba
20 Aprili 2024Ligi Kuu Tanzania BaraYanga 2–1 Simba
5 Novemba 2023Ligi Kuu Tanzania BaraSimba 1–5 Yanga

Hitimisho

Vita ya wachezaji Yanga SC vs Simba SC
Vita ya wachezaji Yanga SC vs Simba SC

Tetesi za Waamuzi wa Morocco kusimamia mechi ya Simba SC vs Yanga SC zinazidi kupamba moto, hii ni kuelekea mchezo huu mkubwa utakaopigwa Jumapili 3/5/2026. Tetesi hizi zimezidi, baada ya kushuhudia mechi ya Fainali ya Muungano Cup 2026 ikisimamiwa na mwamuzi wa Kenya, Dickes Mimisa. Mechi hiyo iliisha kwa Simba SC kuibuka na ubingwa huku kukiwa na maoni tofauti, juu ya mwamuzi huyo. Muda utatoa majibu y ani nani Pilato wa Jumapili.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.