- Zimamoto iliwazima Coastal Union kuwakabili Yanga nusu fainali Aprili 29 2025 Muungano Cup.
- JKU SC iliyowafungashia virago Singida Black Stars kukabiliana na matajiri wa Dar Azam FC Aprili 28 2025.
- Dennis Nkane wa Yanga azua gumzo kwa kumnyima pasi Aziz Ki na kumpa mateso mlinda mlango.
Zimamoto FC vs Yanga SC, ni nusu fainali ya pili Muungano Cup inayotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Gombani Aprili 29.

Mshindi wa mchezo huo atakata tiketi kwenye hatua ya fainali na anatarajiwa kukutana na mshindi wa mchezo wa Aprili 28 2025 kati ya JKU SC vs Azam FC.
ZIMAMOTO ILIWAZIMA COASTAL UNION
Aprili 25 2025 kwenye mchezo wa robo fainali Zimamoto iliwazima Coastal Union inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara kwa ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na nyota Rashid Salum dakika ya 28.
Bao hilo lilidumu mpaka mwisho wa mchezo na Coastal Union ikawa imegota mwisho katika Muungano Cup 2025 ambayo imekuwa na ushindani mkubwa kwa timu zinazoshuka uwanjani kusaka ushindi.
Ipo wazi kwamba mchezaji bora wa mchezo huo alichaguliwa kuwa mfungaji wa bao pekee la ushindi ambaye ni Rashid Salum nyota wa Zimamoto hivyo Aprili 29 2025 watakuwa kwenye kazi msako wa ushindi kwa timu itakayotinga hatua ya fainali.
DENNIS NKANE ALITABIRIWA MAPEMA
Dennis Nkane ameweka wazi kuwa aliambiwa na kiungo mshambuliaji Maxi Nzengeli kwamba atapata nafasi kwenye mechi za Muungano Cup, Zanzibar.

Nkane ndani ya Yanga kwenye mechi za ushindani hajawa na nafasi ya kwanza kikosi cha kwanza ambapo Yanga ni vinara wa ligi wakiwa na pointi 70 baada yakucheza mechi 26.
Alipata nafasi yakucheza kwenye mchezo wa robo fainali dhidi ya KVZ FC kwenye Muungano Cup akitokea benchi na Yanga ikpata ushindi wa mabao 2-0 na kutinga hatua ya nusu fainali ambapo itakutana na Zimamoto FC, Aprili 29 2025.
Kiungo huyo amesema kuwa furaha kubwa kupata nafasi kwenye mechi za ushindani na aliamini kwamba kwa namna yoyote angefunga kutokana na ugumu wa mchezo wenyewe ulivyokuwa.
“Maxi aliniambia kwamba kwa muda mrefu sijapata nafasi yakufanya jambo ndio maana nilipofunga alishangilia kwa furaha, ninanajua wachezaji wengi walifurahi lakini Maxi alifurahi zaidi.
“Ulikuwa ni mchezo mgumu wenye ushindani mkubwa, niliwaambia wachezaji wenzangu ambao tulikuwa benchi kwamba nikiingia halafu nikafunga basi washangilie kwa nguvu kuwa sisi ni familia.
“Nilipofunga niliangalia wapo ambao hawakushangilia kwa nguvu najua hao nitaonana nao mwenyewe kwa kuwa mchezo huu tulikuwa tunauhitaji, kazi yetu ni kuhakikisha tunawapa furaha mashabiki.”
Yanga ilipata ushindi wa mabao 2-0 ambapo bao la ufunguzi lilifungwa na kiungo Aziz Ki na bao la pili alifunga Nkane ambaye alikuwa na nafasi yakutoa pasi kwa Aziz Ki aliyekuwa kwenye nafasi yakufunga bao hilo.
WAPINZANI WA YANGA NUSU FAINALI MUUNGANO CUP
Yanga imetinga hatua ya nusu fainali itakwenda kumenyana na Zimamoto hatua ya nusu fainali na mchezo unaotarajiwa kuchezwa Aprili 29 2025 na mshindi wa mchezo wa Aprili 28 kati ya JKU ama Azam FC watakutana na mshindi wa nusu fainali ya Aprili 29.
Aziz Ki alifungua pazia la mabao dakika ya 29 kwenye mchezo huo. Ilikuwa Aprili 26 2025 siku ya Muungano ambapo alipachika bao hilo Uwanja wa Gombani kwa mguu wake wa kushoto akipiga shuti kali ambalo lilimshinda mlinda mlango wa KVZ FC.
Kiungo Dennis Nkanne dakika ya 85 alipachika bao la pili la ushindi kwa Yanga akiwa ndani ya 18 kwa mguu wake wa kulia baada ya beki wa KVZ FC kutoa pasi ambayo haikumfikia mlengwa kwa kuwa tayari Nkane aliingia mchezo huo.
Nkane ambaye alianzia benchi kabla ya kufunga bao hilo aliwaambia wachezaji wenzake waliokuwa benchi kuwa akiingia akifunga lazima washangilie ikiwa hawatafanya hivyo atawapa adhabu kwa kuwa watakuwa wamemsaliti mshikaji.
JKU VS AZAM FC NUSU FAINALI YA KWANZA
Ni Azam FC Aprili 28 2025 wanatarajiwa kuwa kazini kwenye mchezo wa nusu fainali Muungano Cup, visiwani Zanzibar.

Azam FC itakuwa Uwanja wa Gombani, Pemba, leo Jumatatu saa 1.15 usiku kuvaana na JKU ambayo iliwafungashia virago Singida Black Stars hatua ya robo fainali huu utwakuwa ni mchezo wa nusu fainali.
Aprili 25 2025 Azam FC ilitinga nusu fainali kwa ushindi mbele ya KMKM 0-1 Azam FC bao likifungwa na Lusajo Mwaikenda na kiungo James Akamiko alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo.

