Yanga SC vs Singida Black Stars Fainali ya CRDBYanga Bingwa Muungano Cup ---- (-)

  • JKU 0-1 Yanga SC: Yanga bingwa Muungano Cup 2025 kwa bao pekee la kiungo Maxi nzengeli dakika ya 45 ya mchezo.
  • Matokeo ya fainali yamejirudia kwani mara ya mwisho Yanga na JKU walikutana Oktoba 10, 2021 na Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0.
  • Mashindano hayo yameshirikisha timu 8 msimu huu, 4 kutoka Tanzania Bara na 4 kutoka Tanzania Visiwani.

JKU 0-1 Yanga SC: Yanga bingwa Muungano Cup 2025 Hatimaye kikosi cha Yanga kimefanikiwa kutangazwa kuwa mabingwa wapya wa mashindano ya Kombe la Muungano, hii ni baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mchezo wa fainali dhidi ya JKU.

Kama ambavyo ilitarajiwa na wengi mchezo huo ambao umepigwa kwenye Uwanja wa Gombani, Zanzibar ulikuwa mkali na wenye  ushindani mkubwa.

Ni bao pekee la kiungo mshambuliaji wa Yanga Mkongomani, Maxi Nzengeli ndilo ambalo alilifunga mwishoni mwa kipindi cha kwanza ndilo lilitosha kuipa Yanga ubingwa huo.

Yanga wamefanikiwa kutinga Fainali kwa changamoto ya matuta 1-3 dhidi ya KVZ katika mchezo wa Nusu ambao ulikuwa na ushindani wa aina yake ulipigwa kwenye Uwanja wa Gombani, Zanzibar na kukosekana mshind ndani ya dakika 90.

JKU 0-1 Yanga, Fainali ilikuwaje?

JKU 0-1 Yanga: Yanga bingwa Muungano Cup 2025
Yanga na JKU wakipambana

Mchezo wa fainali ulianza kwa kila timu kucheza kwa tahadhari kubwa, huku Yanga wakifanya majaribio kadhaa ya hatari huku JKU wakikaa imara na kuyadhibiti.

Baada ya majaribio kadhaa  ambayo yaliondolewa na safu ya ulinzi ya JKU, hatimaye juhudi za Yanga zilizaa matunda baada ya Maxi kuiandikia Yanga bao pekee la mchezo huo muda mchache kabla ya mapumziko.

Mara baada ya bao hilo Yanga waliendelea kutawala mchezo lakini hawakufanikiwa kutumia nafasi walizotengeneza, huku JKU nao wakijibu kwa mashambulizi ya kujibu bila mafanikio yoyote mpaka filimbi ya mwisho ya mwamuzi.

Njia ya kufuzu fainali

Yanga SC ilifanikiwa kutinga fainali ya Muungano Cup 2025 baada ya kuwaondosha Zimamoto, katika mchezo mkali wa Nusu Fainali ulioisha kwa sare ya bao 1-1 na mchezo kulazimika kuamuliwa kwa changamoto ya Penalti.

Yanga waiibuka na ushindi wa Penalti 3-1 dhidi ya Zimamoto ambapo kip awa Yanga, Aboutwalib Mshery aliibuka shujaa kwa kuokoa penalty 2.

Ikumbukwe JKU wao walikata tiketi ya kucheza Fainali baada ya kuwaondosha Azam FC katika mchezo wa Nusu fainali kwa ushindi wa mabao 2-1.

Nne bora ya Muungano Cup 2025

Robo Fainali ya Muungano Cup msimu huu ilishuhudia mzani ukisawazwa, kwa kuwa na timu mbili kutoka Tanzania Bara na timu mbili kutoka Tanzania Visiwani.

Ukiachana na Yanga waliofuzu fainali, timu nyingine ambazo zilifuzu Nusu Fainali mpaka sasa ni, Azam FC, Zimamoto na JKU.

walichosema Yanga baada ya ubingwa

------------------------------------------------n
Mwamnyeto na kombe

Mara Baada ya ushindi huo JKU 0-1 Yanga SC: Yanga bingwa Muungano Cup 2025 walikiri kuwa na furaha kubwa ya kushinda fainali na kufanikisha malengo ambayo walijiwekea katika mashindano hayo ya Muungano Cup 2025.

Akizungumzia kwa furaha mara baada ya kukabidhiwa kombe hilo Nahodha wa Yanga, Bakari Mwamnyeto amesema: “Ulikuwa mchezo mgumu, tunawapongeza JKU kwa kuonyesha ushindani mzuri, hiyo ndio maana ya fainali na jambo jema kwetu ni kuwa tumeshinda ubingwa.

“Malengo yetu yalikuwa kufanikisha na kutwaa ubingwa na tulijua wazi kuwa safari haiwezi kuwa rahisi, lakini maandalizi makubwa ambayo tumeyafanya yametupqa matokeo chanya.”

MAANDALIZI SIRI YA UBINGWA YANGA

------------------------------------------------n
Maxi Nzengeli

Baada ya kushinda ubingwa huo, benchi la ufundi la Yanga SC limeelezea furaha yake kuhusu ushindi huo, ambapo wamesema kuwa Yanga SC kuwa mabingwa wa Muungano Cup 2025 ni matokeo ya maandalizi mazuri na ushirikiano.

Benchi hilo limetamba na kuongeza kuwa ubingwa huo unawapa jeuri na ari ya kufanya vizuri katika michezo yao ya mashindano mengine ambayo wanashiriki.

wachezaji wako tayari kwa changamoto ya mchezo wa hatua ya fainali zinazofuata katika michuano ya Kombe la Muungano 2025.​

Mashabiki Yanga watamba kuzoa makombe

Mashabiki wa Yanga SC walijitokeza kwa wingi katika Uwanja wa Gombani, wakishangilia timu yao kwa nguvu, baada ya ubingwa huo wametamba kuendeleza kasi ya kuzo amakombe.

Sehemu ya mashabiki hao walisema kwao hatua hiyo ni ya kujivunia  na ni ishara ya mafanikio makubwa katika michuano ya Kombe la Muungano 2025.​

Kituo kinachofuata Ligi Kuu na FA

Baada ya ushindi huo, Yanga SC wanatarajia kurejea Dar es Salaam kwa ajili ya maandalizi ya michezo ya mashindano ya Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho la CRDB ambayo inaendelea.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.