Arsenal vs Sporting CPArsenal vs Sporting CP
  • Arsenal vs Sporting ni tafsiri halisi ya vita ya kufuzu nusu fainali ya UEFA Champions League itakayopigwa Uwanja wa Emirates.
  • Arsenal wanasaka kuipata nafasi hiyo kwa mara ya pili mfululizo, lakini watalazimika kuidhibiti Sporting CP leo Jumatano usiku.
  • Ikumbukwe mchezo wa mkondo wa kwanza uliisha kwa matokeo ya Sporting CP 0-1 Arsenal.
  • Unataka kubashiri? Matokeo ya Over 1.5 FT yana nafasi kubwa kutokea.

Arsenal vs Sporting ni vita ya kufuzu nusu fainali ya UEFA Champions League. Arsenal wanasaka kuipata nafasi hiyo kwa mara ya pili mfululizo, lakini watalazimika kuidhibiti Sporting CP leo Jumatano usiku. Ikumbukwe mchezo wa mkondo wa kwanza uliisha kwa matokeo ya Sporting CP 0-1 Arsenal.

Unaweza kubashiri mechi hii moja kwa moja kwa kugusa hapa Arsenal vs Sportng CP. Fuatilia matukio ya karibuni ya UEFA Champions League Quarter Finals match , mabao, takwimu na habari za hivi sasa kupitia SportPesa blog

SOMA HII PIA: Arsenal FC muhtasari, ratiba, matokeo, habari za usajili, msimamo wa ligi na takwimu

Unataka mkwanja? Cheza sasa mchezo wa Aviator ‘Kindege’ cha SportPesa ushinde mpaka Milioni 800

Mchezo wa Kindege cha SportPesa unaendelea kutoa mamilionea, ambapo sasa unaweza kushinda  mpaka Milioni 800 za Tanzania, cheza sasa na ushinde.

Aviator game jackpot banner TSh 800 Million prize
Rukia ushindi! 🛫 Win up to TSh 800,000,000 with Aviator. Cheza leo

Rekodi ya head-to-head, Arsenal vs Sporting CP

Katika mechi 5 za mwisho walizokutana, Arsenal wanaongoza kwa kushinda mechi 2, huku Sporting wakiwa wameshinda mechi moja tu. Usshindi ambao Sporting CP waliupata ni wa mabao 2-1, ambao ulipatikana kwenye mashindano ya UEFA Europa League misimu miwili iliyopita. Mechi mbili kati ya wababe hawa zilimalizika kwa matokeo ya sare.

Fomu ya timu mechi 5 zilizopita

Sporting Lisbon vs Arsenal &#x b;&#xfe f;
Sporting Lisbon vs Arsenal

Arsenal wamepoteza mechi 3 kati ya 5 zilizopita, ikiwemo ile ya Bournemouth, na sasa wanakutana na Sporting ambao wameshinda mechi nne kati ya tano zilizopita. Sporting pia wamepoteza mechi moja tu kati ya 11 za mwisho walizocheza ugenini kwenye mashindano yote. Hii inazidi kuonyesha kuwa, mechi hii ina ushindani mkubwa.

Fomu kwa ufupi;

Arsenal – LWLLW

Sporting – WLWWW

SOMA HII ZAIDI: Sporting Lisbon vs Arsenal: Live Score, h2h, lineups, prediction, na habari za timu, Robo Fainali UEFA Champions League

Kuhusu mechi ya Arsenal vs Sporting CP

Arsenal vs Sporting CP
Arsenal vs Sporting CP

The Gunners walilazimika kusubiri hadi dakika ya 91 kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza nchini Ureno, kupata bao pekee la mchezo. Bao hilo lilifungwa na staa wao wa kimataifa wa Ujerumani, Kai Harvertz hivyo kuwapa ushindi muhimu wa 1-0 ugenini. Licha ya ushindi huo, Arsenal wako kwenye kiwango kisicho cha kuridhisha, ambacho kinaweza kuhatarisha nafasi yao ya ubingwa wa English Premier League. Arsenal haijashinda ubingwa wa EPL kwa miaka 24.

Kikosi cha Arteta kilikubali kipigo cha kushangaza cha mabao 2-1 nyumbani, dhidi ya Bournemouth mwishoni mwa wiki. Sporting wao wameibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Estrela Jumamosi iliyopita. Klabu hiyo kutoka Ureno inaingia kwenye mechi hii ikiwa kwenye kiwango bora zaidi, na walionesha uwezo mzuri katika mechi ya kwanza.

Hata hivyo, Sporting wameshinda mechi moja tu, kati ya nane za mwisho walizocheza ugenini barani Ulaya. Hii inaweza kuwa changamoto yenye kushusha ari ya kikosi. Ikiwa Sporting CP watafanikiwa kuifunga Arsenal, watakuwa wamefuzu nusu fainali kwa mara ya kwanza katika historia ya mashindano haya.

SOMA HII ZAIDI: Arsenal vs Manchester City Carabao Cup Final: Live Score, lineups, h2h, habari za timu na utabiri wa matokeo

Taarifa za wachezaji majeruhi

---

Kwa upande wa wenyeji, bado watakosa huduma za Bukayo Saka na Martin Ødegaard, ambao kukosekana kwao kumeonekana katika mechi za karibuni. Kai Havertz anaweza kuanza baada ya kuwa shujaa wa mechi iliyopita, pamoja na Leandro Trossard. Noni Madueke huenda akaanzia benchi, huku, Eberechi Eze na Viktor Gyökeres wakiongoza safu ya ushambuliaji. Safu ya ulinzi inatarajiwa kubaki ileile kama ya mechi ya kwanza, huku David Raya akiwa golini.

Fuatilia habari za hivi punde za mechi ya Arsenal vs Sporting CP ikiwemo Live odds, stats, Match Updates na Lineups kupitia SportPesa.

Utabiri wa Arsenal vs Sporting

h-h (-)
h-2-h

Kabla ya mechi ya wiki iliyopita, michezo minne ya awali kati ya timu hizi mara nyingi ilizaa mabao zaidi ya 2.5. Inatarajiwa kuwa mchezo huu wa marudiano utakuwa wazi zaidi kuliko ule wa kwanza, na kutoa nafasi kwa washambuliaji wa pande zote mbili. Chaguo zuri zaidi la mchezo huu kubashiri uwezekano wa kupata mabao 2 au zaidi yaani (over 1.5)

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.