Arsenal-Sporting-CPArsenal-Sporting-CP

TIMU GANI KWENDA ROBO FAINALI EUROPA LIGI LEO

Leo ni siku nyingine adhimu ya kimichezo, hasa hasa mchezo wa mpira wa miguu, ambapo mechi za ligi ya Europa, mzunguko wa 16, zitachezwa kuanzia majira ya saa za usiku mbili na nusu usiku, ambacho mechi za awali zitaanza kuchezwa.

Hapa tunaangaza kidogo jinsi mechi hizi zinavyoweza kuwa.

Betis VS Man United

Kwa namna matokea ya mechi ya kwanza mzunguko uliopita timu ya Man United ilishinda kwa magoli 4-1 dhidi ya Real Betis. Kwa hivyo leo Kocha wa Real Betis Manuel Pellegrini atahitajika kutumia uzoefu wake wote wa kitaalamu kushinda mechi hii ili timu yake iweze kusonga mbele kwenda hatua ya Robo Fainali.

Kocha huyo raia wa Chile amepoteza mara moja tu katika uwanja wa nyumbani dhidi ya Man united katika mechi 7 ambazo wamecheza katika mashindano yote ambayo wamewahi kukutana.

Kuna angalizo moja tu ninaloweza kuwapa, wapenzi na mashabiki wa Man United ambao kwa muda huu wanatamba na ushindi wa magoli 4-1 dhidi ya Real Betis kutoka mechi iliyopita.

Wasivimbe kichwa

Katika historia ya Man United timu ya Sir Matts Busby iliwahi kushindwa kufuzu kwenda robo fainali ya kombe la EUROPA Winners Cup, katika msimu wa Mwaka 1963/1964, baada ya kuongoza mzunguko wa kwanza kwa magoli 4-1 dhidi ya Sporting CP ya Ureno na kupigwa kwa magoli 5-0 jijini Lisbon.

Arsenal VS Sporting CP (2-2)

Moja kati ya mechi kali na ya kusisimua ambayo ilihusisha miamba hawa wawili wa Lisbon na London ilichezwa wiki iliyopita na kutoa matokeo ya magoli 2-2 ambayo yalifungwa back-to-back.

Mechi ya Leo ni ngumu kutabirika ingawaje Arsenal anategemewa kutumia vizuri faida ya kucheza uwanja wa nyumbani emirate Stadium, huku akiwa pia na faida ya goli la ugenini.

Kocha wa Sporting CP Ruben Amorim amesema ana matumaini wachezaji wake watajitahidi kupambana kama ambavyo walivyopambana nyumbani kwao wiki iliyopita, akisema mechi yao leo dhidi ya Arsenal bado ipo wazi na ni matumaini yake wanaweza kushinda 2-1 au 3-1.

Hata hivyo Arsenal hajafungwa mechi nne katika uwanja wa nyumbani katika mashindano haya. Je sporting CP kutibua rekodi hiyo.

Mechi ya mwisho kuwapa uchambuzi ni

Fenebache VS Sevilla (2-0)

Nawakumbusha tu, timu hizi mbili zina historia ambayo inaweza kujirudia siku ya leo. Katika msimu wa mwaka 2007/2008 wa ligi ya kombe la UEFA Champions League timu hizi zilikutana katika mechi kabambe ambayo imebaki kuwa historia kwa wapenzi wa soka duniani.

Man-U-Betis-Katika mechi ya mzunguko wa Kwanza timu ya Sevilla ilishinda 3-2 dhidi ya Fernabache, magoli yakifungwa na Dani Alves (5), Keita (9) na Kanoute (41) wakati magoli ya Fernabache, yote mawili yakifungwa na Deivid (20) na (79).

Siku ya mechi ya marudiano kama leo, Sevilla waliingia na hali ya kujiamini sana, wakicheza mpira wa madaha na kupoteza muda na kutawala kipindi chote cha kwanza.

Mungu si Athumani kipindi cha pili Fernabache walianza kuonyesha uhai wakijaribu kushambulia kwa kushitukiza na kufanikiwa kushinda kwa magoli (2-3), na kufanya matokeo ya jumla kuwa (5-5), na hivyo kwenda dakika za nyongeza.

Dakika za nyongeza nazo hazikuzaa ushindi kwa timu yoyote ndipo kipa wa Fernabache Volkan Demirel alipoibuka shujaa kwa kupangua penati 3 kati ya 5 zilizopigwa na Sevilla na kuwafanya Sevilla kutupwa nje ya mashindano.

Kocha wa Fernabache amerejea historia hiyo siku ya jana wakati akiongelea mchezo wa leo na kuikumbusha dunia, kwamba historia ina utamaduni wa kujirudia.

Kama kawaida ya SportPesa, mechi zote 8 za Europa League na nyinginezo zinazochezwa leo zipo katika tovuti yetu Sportpesa.co.tz na pia unaweza kucheza Supa Jackpot ambayo kwa sasa imesimamia 1,090,583,531, kwa wiki hii.

 

 

 

 

Share this: