- Kitaumana tena leo Jumanne katika Dakika 90 nyingine ngumu za mashindano ya UEFA Champions League katika jiji la Liverpool nchini England.
- Ni Liverpool vs Paris Saint-Germain, mechi ya Robo Fainali ya pili itakayopigwa kwenye Uwanja wa Anfield.
- Ikumbukwe mchezo wa mkondo wa kwanza kwenye Uwanja wa Parc des Princes, ubao wa matokeo ulisoma Paris Saint-Germain 2-0 Liverpool.
- Mshindi wa jumla baada ya mchezo wa leo, atafuzu moja kwa moja hatua ya Nusu Fainali.
Dakika 90 nyingine ngumu za mashindano ya UEFA Champions League zitapigwa leo Jumanne katika jiji la Liverpool nchini England. Ni Liverpool vs Paris Saint-Germain, ambayo ni mechi ya Robo Fainali ya pili. Katika mchezo wa mkondo wa kwanza kwenye Uwanja wa Parc des Princes, ubao wa matokeo ulisoma Paris Saint-Germain 2-0 Liverpool. Mshindi wa jumla baada ya mchezo wa leo, atafuzu moja kwa moja hatua ya Nusu Fainali.
SOMA HII PIA: Alexander Isak atua Liverpool: Avunja rekodi ya uhamisho Premier League, kwa £130m
Unataka mkwanja? Cheza sasa mchezo wa Aviator ‘Kindege’ cha SportPesa ushinde mpaka Milioni 800
Mchezo wa Kindege cha SportPesa unaendelea kutoa mamilionea, ambapo sasa unaweza kushinda mpaka Milioni 800 za Tanzania, cheza sasa na ushinde.

Liverpool vs Paris Saint-Germain h2h

Timu hizi hazina historia ya matokeo ya sare tangu zimeanza kukutana, katika mechi zote miongoni mwao hupatikana mbabe. Msimu uliopita walikutana katika hatua ya 16 bora, ambapo PSG walisonga mbele kwa mikwaju ya Penalti baada ya matokeo ya jumla ya 1-1. Hii ni baada ya kila timu kushinda ugenini, msimu huu wamekutana kwenye hatua ya Robo Fainali na tayari PSG anaongoza kwa mabao 2-0. Je, Liverpool wataivua ubingwa PSG? Dakika 90 zitatoa majibu.
Vikosi vinavyotarajiwa Liverpool vs Paris Saint-Germain
Liverpool:
Kipa: Mamardashvili
Walinzi: Szoboszlai, Konate, Van Dijk, Kerkez
Viungo: Gravenberch, Mac Allister; Salah, Wirtz, Ngumoha
Mshambuliaji: Ekitike
Paris Saint-Germain:

Kipa: Safonov
Walinzi: Hakimi, Marquinhos, Pacho, Mendes
Viungo: Zaire-Emery, Vitinha, Neves, Doue
Washambuliaji: Dembele, Kvaratskhelia
Habari za timu

Kocha Arne Slot alishuhudia timu yake ikipoteza kwa mabao 2-0 dhidi ya mabingwa hao watetezi wa Ulaya, kwenye mchezo wa kwanza wiki iliyopita. Liverpool walikuwa na Bahati kuepuka kipigo kikubwa zaidi, kutokana na nafasi ambazo PSG walitengeneza. Katika mchezo wa kwanza, Slot alifanya mabadiliko ya kushangaza kwa kutumia mfumo wa 3-5-2 wenye wachezaji wengi wa ulinzi, huku Mohamed Salah akikosa nafasi kwenye kikosi hicho. Katika mechi hiyo, Desire Doue na Khvicha Kvaratskhelia walifunga mabao yaliyoiwezesha PSG kushinda 2-0.
Pamoja na kuwa nyuma kwa mabao 2-0, Liverpool bado wana matumaini ya kupindua meza. Hii inachangiwa na kumbukumbu ya ushindi wao wa kihistoria wa 4-0 dhidi ya Barcelona, katika nusu fainali miaka saba iliyopita. Wikiendi iliyopita, Liverpool walirejea kwenye ushindi kwa kuifunga Fulham 2-0 katika Ligi Kuu England. Katika mechi tano zao za mwisho nyumbani Anfield, wameshinda nne, hawajapoteza na wamefunga mabao 15.
PSG, hawakuwa na mechi ya ligi mwishoni mwa wiki baada ya ratiba yao kurekebishwa ili kuwapa muda wa kujiandaa na mchezo huu. Timu hiyo inaendelea kuwa na kiwango kizuri, ikiwa imeshinda mechi tano mfululizo. PSG pia wana rekodi nzuri ugenini, wakiwa wameshinda mechi zao nne zilizopita nje ya uwanja wao, na hawajaruhusu bao katika mechi tatu kati ya hizo.
SOMA HII ZAIDI: Barcelona vs Atletico Madrid UEFA Champions League: Live Score, h2h, Lineups, prediction na habari za timu
Taarifa za wachezaji wenye majeraha
Liverpool
Curtis Jones anaweza kurejea baada ya kuanza mazoezi, lakini klabu inaendelea kuwa na majeruhi ya baadhi ya mastaa ambao ni: Alisson Becker, Wataru Endo, Giovanni Leoni na Conor Bradley. Kinda Rio Ngumoha mwenye miaka 17, aliweka rekodi mpya ya kuwa mfungaji mdogo zaidi wa Liverpool katika Anfield, na anaweza kupewa nafasi ya kuanza.
PSG
Wao hawana majeruhi mapya, huku pia wakipata faida ya kurejea kwa Bradley Barcola. Fabian Ruiz pekee ndiye bado yuko nje kutokana na jeraha. Hii inawafanya PSG kuwa na jeuri kubwa ya kupanga kikosi imara kulinganisha na wapinzani wake.
Utabiri na hitimisho

Kwanza ijulikane kuwa huu ni mchezo mgumu, Liverpool vs Paris Sait-Germain umekuwa vita kubwa katika kipindi cha misimu miwili sasa. Liverpool wanacheza nyumbani na wanapewa nafasi kubwa ya kuboresha kiwango chao kulinganisha na mchezo wa kwanza, angalau kuonyesha dhamira ya kushinda. Tatizo kubwa kwao ni ubora wa PSG kwa sasa, kuanzia kwenye kiwango hadi utimamu wa wachezaji, hivyo PSG wanapewa nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi angalau wa mabao 2-1.

