- Atletico Madrid vs Barcelona Je, nani anakwenda Nusu fainali ya UEFA Champions League leo Jumanne?
- Barcelona wanahitaji kufanya comeback kubwa, maarufu ‘Remontada’ ili kuokoa matumaini yao ya kushinda ubingwa wa Ligi ya Mabingwa.
- Ni katika mchezo mkali wa marudiano utakaopigwa Uwanja wa Wanda Metropolitano, jijini Madrid. Ikumbukwe mchezo wa kwanza uliisha kwa matokeo ya Barcelona 0-2 Atletico Madrid Uwanja wa Camp Nou
- Makala hii inachambua na kukupa utabiri wa matokeo ya mchezo huu.
Atletico Madrid vs Barcelona nani anakwenda fainali leo Jumanne? Barcelona wanahitaji kufanya comeback kubwa, maarufu ‘Remontada’ ili kuokoa matumaini yao ya kushinda ubingwa wa Ligi ya Mabingwa. Hii ni katika mchezo mkali wa marudiano utakaopigwa kwenye Uwanja wa Wanda Metropolitano, jijini Madrid. Ikumbukwe mchezo wa kwanza uliisha kwa matokeo ya Barcelona 0-2 Atletico Madrid mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Camp Nou Jumatano iliyopita. Ikumbukwe huu ni mchezo wa 3 mfululizo kwa vigogo hao kukutana, ndani ya kipindi cha siku 10 tu.
SOMA HII PIA: Barcelona vs Atletico Madrid UEFA Champions League: Live Score, h2h, Lineups, prediction na habari za timu
Unataka mkwanja? Cheza sasa mchezo wa Aviator ‘Kindege’ cha SportPesa ushinde mpaka Milioni 800
Mchezo wa Kindege cha SportPesa unaendelea kutoa mamilionea, ambapo sasa unaweza kushinda mpaka Milioni 800 za Tanzania, cheza sasa na ushinde.

Atletico Madrid vs Barcelona h2h

Timu hizi zinakutana kwa mara ya 3 katika kipindi kisichozidi siku 15. Katika mapambano mawili yaliyopita kila timu imeibuka na ushindi wa mechi moja, na kila timu ilishinda ugenini. Barcelona waliichapa Atletico mabao 2-1 kwenye La Liga kabla ya Atletico kulipa kisasi kwa kuichapa Barcelona 2-0 kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza ugenini Camp Nou kwenye mchezo wa Mkondo wa kwanza wa UEFA Champions League. Dakika 90 za leo zitaamua nani anakwenda Nusu Fainali.
Vikosi vinavyotarajiwa kuanza Atletico Madrid vs Barcelona
Atletico Madrid:

Kipa: Musso
Walinzi: Molina, Lenglet, Le Normand, Ruggeri
Viungo: Simeone, Llorente, Koke, Lookman
Washambuliaji: Griezmann, Alvarez
Barcelona:
Kipa: J. Garcia
Walinzi: Kounde, Araujo, E. Garcia, Cancelo
Viungo: Pedri, De Jong; Yamal, Lopez
Washambuliaji: Rashford, Torres
Habari za timu

Barcelona walipata pigo kubwa kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza, walipofungwa 2-0 nyumbani huku wakiwa pungufu ya mchezaji mmoja. Matokeo hayo yameiacha Atletico ikiwa na nafasi kubwa ya kusonga mbele, kwenye hatua ya nusu fainali ambapo watavaana na Arsenal, au Sporting Lisbon. Katika mchezo wa kwanza uliochezwa Jumatano iliyopita, Barcelona walionekana kuelemewa na presha iliyochangiwa pia na beki chipukizi Pau Cubarsi kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 44. Atletico walitumia vyema nafasi hiyo, ambapo Julian Alvarez alifunga bao la kwanza kwa mpira wa adhabu uliopigwa kwa ustadi mkubwa.
Alexander Sorloth aliongeza bao la pili na kuwanyamazisha mashabiki wa Barcelona, ndani ya dimba lao la Camp Nou. Kabla ya mchezo huo, Atletico walikuwa wanapitia kipindi kigumu baada ya kupoteza mechi tatu mfululizo, ikiwemo kipigo cha 2-1 kutoka kwa Barcelona kwenye La Liga. Hata hivyo, walirejea kwa nguvu katika mchezo wa mkondo wa kwanza. Wikiendi iliyopita, Atletico walipoteza tena 2-1 dhidi ya Sevilla, lakini kocha Diego Simeone alifanya mabadiliko mengi kikosini ili kujiandaa na mchezo huu wa marudiano.
Licha ya matokeo hayo, Atletico wana rekodi nzuri nyumbani, wakiwa wameshinda mechi sita mfululizo katika Uwanja wa Wanda Metropolitano kabla ya kupoteza hivi karibuni dhidi ya Barcelona. Atletico pia wamefunga angalau bao, katika karibu kila mechi ya nyumbani msimu huu. Hata hivyo, historia inaonyesha kuwa Atletico waliwahi kushinda mchezo wa kwanza wa robo fainali lakini wakatolewa kwenye mchezo wa pili, jambo linaloweza kuwapa Barcelona matumaini kidogo.
Barcelona wao waliibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Espanyol, mwishoni mwa wiki. Katika mchezo huo, Lamine Yamal aliweka rekodi ya kuwa mchezaji mdogo zaidi kufikisha mechi 100 za La Liga na alifunga bao pamoja na kutoa pasi ‘assist’ mbili za mabao. Barcelona wanaongoza ligi ya La Liga kwa tofauti ya pointi tisa dhidi ya Real Madrid, hivyo mchezo huu wa Jumanne unaonekana kuwa muhimu zaidi kwao msimu huu. Ili kufanikisha comeback hiyo, safu ya ushambuliaji ya Barcelona italazimika kuwa makini na kutumia kila nafasi watakayopata.
SOMA HII ZAIDI: Barcelona vs Atletico Madrid: Live Score, h2h, line-up, utabiri
Taarifa za majeruhi na watakaokosa mechi
Atletico Madrid
Atletico walipata changamoto ya majeraha katika mchezo wa kwanza, ambapo David Hancko alitoka mapema kutokana na jeraha la kifundo cha mguu. Mbadala wake, Marc Pubill alipata kadi ya njano inayomfanya akose mchezo huu. Hancko pamoja na Jose Gimenez wote wapo hatarini kukosa mchezo huu, lakini wachezaji kama Johnny Cardoso na Pablo Barrios wameanza mazoezi. Kipa namba moja, Jan Oblak pia anaweza kurejea.
Barcelona

Pau Cubarsi atakosa mchezo huu kutokana na kadi nyekundu aliyopata, Ronald Araujo au Eric Garcia wanatarajiwa kuchukua nafasi yake. Gerard Martin alipata maumivu madogo katika mchezo dhidi ya Espanyol, lakini anatarajiwa kuwa fiti. Hata hivyo, Raphinha na Marc-Andreas Christensen watakosekana kutokana na majeraha.
SOMA HII PIA: Atletico Madrid vs Barcelona – A Battle for Supremacy in La Liga
Utabiri na hitimisho
Atletico Madrid vs Barcelona sio mchezo tu utakuwa mchezo mgumu, bali vita halisi ya Uwanjani kuisaka tiketi ya Nusu Fainali ya Mashindano ya Klabubarani Ulaya. Wenyeji Atletico wana faida ya matokeo ya mchezo wa kwanza na wanacheza nyumbani, jambo linalowapa nafasi kubwa ya kusonga mbele. Kuna uwezekano mkubwa mchezo huu ukaisha kwa matokeo ya sare ya mabao.

