- Vita ya mabingwa watetezi! Yaani Mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA Champions League), dhidi ya mabingwa watetezi wa Ligi Kuu England (EPL).
- Ni Paris Saint-Germain vs Liverpool, mechi itakayopigwa katika Uwanja wa Parc Des Princes, nchini Ufaransa.
- Mchezo huu unatajwa kuwa wa kisasi kwa Liverpool kwani, timu hizi zilikutana katika hatua ya 16 bora msimu uliopita ambapo PSG waliitoa PSG kwa mikwaju ya Penalti baada ya kila timu kushinda mchezo wa ugenini.
- Hizi hapa dondoo muhimu za mchezo huu;
Mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA Champions League), Paris Saint Germain wanashuka uwanjani leo Jumatano kuvaana na Liverpool. itaendelea tena leo Jumatano. Mechi hii ya Paris Saint-Germain vs Liverpool itapigwa katika Uwanja wa Parc Des Princes, nchini Ufaransa. Mchezo huu unatajwa kuwa wa kisasi kwa Liverpool kwani, timu hizi zilikutana katika hatua ya 16 bora msimu uliopita ambapo PSG waliitoa PSG kwa mikwaju ya Penalti baada ya kila timu kushinda mchezo wa ugenini. Hizi hapa dondoo muhimu za mchezo huu;
SOMA HII PIA: Clash of Titans: PSG vs Barcelona in the UEFA Champions League Quarter-Finals
Je, bado hujashinda na SportPesa? Cheza mchezo wa aviator ‘Kindege’ uvune mpaka milioni 800 sasa
Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi milioni 800 muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Paris Saint-Germain vs Liverpool h2h

Takwimu rasmi kutoka Shirikisho la soka Ulaya UEFA ni kuwa, timu hizi zimekutana katika michezo 4. Mpaka sasa hakuna mbabe katika makutano yao, kwani kila timu imefanikiwa kushinda mechi 2 na hawajawahi kupata matokeo ya sare. Hivyo timu itakayoshinda leo, inajiweka kwenye nafasi ya kuongoza kwenye rekodi ya h2h.
Vikosi vinavyotarajiwa
Paris Saint-Germain
Kipa: Safonov
Walinzi: Hakimi, Marquinhos, Pacho, Mendes
Viungo: Zaire-Emery, Vitinha, Neves
Washambuliaji: Doue, Dembele, Kvaratskhelia
Liverpool

Kipa: Mamardashvili
Walinzi: Frimpong, Konate, Van Dijk, Kerkez
Viungo: Gravenberch, Mac Allister, Salah, Szoboszlai, Wirtz
Mshambuliaji: Ekitike
Habari za timu

Liverpool watahitaji kufanya kazi kubwa sana ikiwa wanataka kuiondoa PSG na kutinga Nusu Fainali ya mashindano haya ya Ulaya. Mabingwa hao wtetezi wa Ligi Kuu England waliishangaza PSG kwa kuichapa bao 1-0, katika uwanja wa Parc des Princes msimu uliopita. Furaha ya ushindi huo haikudumu kwani, PSG nao walilipiza kisasi walipoenda Anfield, na hatimaye kufuzu kwa mapigo ya Penalti.
Liverpool wamekuwa kwenye kiwango kisichoridhisha katika mechi za hivi karibuni, wakipata matokeo mabaya dhidi ya Brighton na Manchester City. Kipigo cha mabao 4-0 walichopata kutoka kwa City kiliwaondosha kwenye mashindano ya Kombe la FA. Kwa ujumla, Liverpool wamepoteza mechi 15 katika mashindano yote msimu huu, ikiwa ni idadi kubwa zaidi tangu msimu wa 2014-15. Pia wamepata ushindi mmoja tu, katika mechi tano zilizopita, japokuwa walipata ushindi mkubwa dhidi ya Galatasaray katika hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa.
Paris Saint-Germain, wanaonekana kuanza kurejea katika ubora wao na wanaongoza mbio za ubingwa wa Ligue 1 kwa tofauti ya alama nne, huku wakiwa bado na mchezo mmoja mkononi. Walipata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Toulouse katika mchezo wao wa mwisho, huku Ousmane Dembele akifunga mabao mawili. PSG pia wako kwenye mfululizo mzuri wa matokeo, wakiwa hawajapoteza katika mechi 7 zilizopita dhidi ya timu za England kwenye Ligi ya Mabingwa, wakishinda mechi 5 kati ya hizo.
SOMA HII ZAIDI: MERSEYSIDE DERBY KUPIGWA, KOCHA LIVERPOOL HANA CHAGUO
Taarifa za majeruhi
Paris Saint-Germain

Bradley Barcola hatakuwepo kutokana na jeraha la kifundo cha mguu. Fabian Ruiz na Quentin Ndjantou pia hawatacheza. Wachezaji muhimu kama Vitinha, Joao Neves na Nuno Mendes wanatarajiwa kurejea kwenye kikosi cha kwanza, pamoja na nahodha Marquinhos.
Liverpool
Kipa, Alisson Becker ana hatihati ya kukosa mchezo huu, na huenda akakosekana kwenye baadhi ya mechi zijazo kutokana na majeruhi. Conor Bradley, Giovanni Leoni na Wataru Endo wao wanatarajiwa kukosa sehemu iliyobaki ya msimu kutokana na majeraha. Taarifa njema kwao ni kuwa Liverpool hawakupata majeruhi mapya katika mchezo wao wa mwisho, na baadhi ya wachezaji muhimu kama Mohamed Salah, Federico Chiesa na Jeremie Frimpong wamerejea kutoka majeruhi.
SOMA HII PIA: PSG Vs Arsenal UEFA CL: H2H, Vikosi, uchambuzi, utabiri
Utabiri na Hitimisho
Liverpool hawajawahi kutoka sare ya 0-0 katika mechi zao 36 zilizopita dhidi ya timu za Ufaransa, na kuna uwezekano mdogo wa matokeo ya bila mabao katika mchezo huu wa Paris Saint-Germain vs Liverpool. PSG wanaogopeka kwa kuwa na safu hatari ya ushambuliaji kwa sasa, na kama safu ya ulinzi ya Liverpiil itazembea basi PSG wanaweza kupata ushindi wa mabao mengi. Utabiri wa matokeo ya mchezo huu ni wa mabao mengi.

