blog.sportpesa.co.tz "Simba SC vs Gaborone United"Sowah Red
  • Jonathan Sowah amerejesha Simba SC kwa sharti la kupelekwa U 20 kufanya mazoezi
  • Ahmed Ally athibitisha taarifa hiyo na maamuzi ya kamati ya nidhamu
  • Mshambuliaji huyo mwenye miaka 27 raia wa Ghana abainisha bado ana mkataba na Simba SC

Jonathan Sowah amerejeshwa Simba SC kwa sharti lakutakiwa afanye mazoezi na timu ya vijana chini ya miaka 20, (Simba SC U 20). Mshambuliaji huyo anayecheza Simba SC ana miaka 27 ni raia wa Ghana alisimamishwa Februari 2026 timu ilipokuwa inajiandaa kuikabili Dodoma Jiji FC. Alikosekana kwenye mechi kubwa za ushindani ikiwemo mchezo wa Kariakoo Dabi, Yanga SC 0-0 Simba SC.

SOMA TAARIFA YA USAJILI: Usajili mpya Yanga balaa! Sowah, Bada, Chikola kwenye Yanga mpya

Paisha Kindege cha SportPesa uvune mamilioni sasa hivi

Muda ni sasa kushinda mamilioni ukicheza mchezo wa Aviator. Ni rahisi sana kwa kila rubani kuvuna mamilioni. Cheza sasa upate mgao wako bila chenga ni rahisi sana

Sportpesa Aviator Rain Free Bets- Mil

Jonathan Sowah amerejeshwa Simba SC, Ahmed Ally athibitisha

Jonathan Sowah amerejeshwa Simba SC
Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari Simba SC.

Rasmi baada ya kukosekana uwanjani kwa muda Jonathan Sowah amerejeshwa Simba SC na ametakiwa kufanya mazoezi na U 20. Simba huyo mweusi alisajiliwa unyamani akitokea kikosi cha Singida Black Stars. Awali tetesi zilikuwa zinaeleza kuwa alikuwa anawindwa na Yanga SC.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC amesema mchezaji huyo alifika mbele ya kamati ya nidhamu ya klabu na kupatikana na hatia kwa baadhi ya makosa yaliyokuwa yakimkabili. Aliongeza kuwa kamati imeamua Sowah afanye mazoezi na timu ya vijana chini ya uangalizi wa karibu. Kurejea kikosi cha wakubwa itategemea na mwenendo wake.

“Kwa sasa Sowah bado ni mchezaji wetu na anatakiwa kufanya mazoezi na timu ya U20. Hii ni sehemu ya mchakato wa kumfuatilia na pindi kamati itakaporidhika na tabia yake, atarejea kwenye kikosi cha wakubwa,”.

SOMA HII: Jonathan Sowah rasmi asaini Simba SC: Ahmed atangaza mashine 7 mpya  tetesi usajili Ligi Kuu NBC 2025/26

Aviator game jackpot banner TSh 800 Million prize

Sowah: Nina mkataba na Simba SC

Jonathan Sowah amerejeshwa Simba SC
Sowah kwenye moja ya mchezo wa ushindani.

Sowah katika mazungumzo yake kupitia Crown FM, amesema yeye ni binadamu na ana pande mbili. Mshambuliaji huyo amebainisha kuwa hana upande wa mazuri pekee bali na mabaya yapo pia. Huku akiongeza kuwa yeye ni mtaalamu.

“Ikiwa mimi ni mtaalamu, nikiwa mtaalamu, sina upande wangu mzuri, sina upande wangu mbaya? Moja kwa moja mimi ni binadamu, hivyo nitakuwa na mazuri na mabaya.

“Watu hawatanipata nikiwa huko nje na uniambie huyu hana nidhamu. Hapana. Wakati wowote utakaonipata kusema sina nidhamu ni uwanjani… Ninapocheza mpira na nikipoteza, nakasirika sana. Lengo langu ni kufunga bao, hata kama nitapata kadi nyekundu au njano, sijali.

“Hawapaswi kuwa na wasiwasi. Kila kitu kitakuwa sawa. Ninachoweza kusema ni kwamba nahitaji maombi yao na wanikumbuke kwenye maombi. Hivyo tu,”.

SOMA HII: Ratiba ya Simba SC 2025/26 Machi dakika 450 za kazi | Msimamo, matokeo

Hitimisho

Jonathan Sowah amerejeshwa Simba SC baada ya kusimamishwa kutokana na utovu wa nidhamu. Mshambuliaji huyo hayupo kwenye mpango wa mchezo ujao dhidi ya Fountain Gate. Kuna hatihati akakosekana mchezo wa Simba SC vs Yanga SC, Mei 3, 2026 saa 11:00 jioni.

Share this: