- Hatimaye Liverpool imemsaini straika, Alexander Isak kutoka Newcastle United.
- Isak anunuliwa kwa ada iliyovunja rekodi ya mauzo kwenye wachezaji wa EPL, baada ya kuuzwa kwa dau la £130m.
- Mchezaji huyo aishukuru Newcastle United kwa mapenzi yao ya daima baada ya kuondoka.
Yametimia! Ndivyo unavyoweza kusema hii ni baada ya taarifa kutoka England kuthibitisha, Alexander Isak atua Liverpool kwa ada ya uhamisho inayovunja rekodi. Mshambuliaji huyo mashuhuri wa Swedeni aliyezaliwa Septemba 21, 1999 atavaa uzi wa Liverpool. Hii ni baada ya kuwepo mvutano mkubwa kuhusu uhamisho wake kutoka Newcastle United.
SOMA HII PIA: Premier League kumechangamka Aprili 26, Chelsea vs Everton
Bado haujashinda? Cheza na ushinde mamilioni leo kwa kupaisha Kindege cha SportPesa (bonyeza picha hii chini)

Historia fupi ya soka ya Isak

Nyota huyo mzaliwa wa Sweden alianza safari yake ya soka katika klabu ya AIK alipokuwa kwenye kikosi cha timu ya makocha vijana. Katika msimu huo aliichezea AIK mechi 29 za ligi na kufunga magoli 13. Baada ya hapo, staa huyo alijiunga na kikosi cha Borussia Dortmund B kabla ya kujiunga na timu ya wakubwa. Baada ya hapo alienda kwa mkopo Willem II ya Uholanzi na akaendeleza rekodi yake kwa kufunga mabao 14 katika michezo 18.
Isak akaondoka Willem II na kujiunga na kikosi cha Real Sociedad ya Hispania kuanzia mwaka 2019 hadi 2022. Akicheza mashindano mbalimbali ya ndani na kimataifa, alifunga magoli 33 katika ligi, 8 kwenye kombe la mfalme na magoli 3 kwenye michuano ya Ulaya. Kwa jumla ya takriban mechi 132, Isak alifanikiwa kufunga magoli 44.
SOMA HII ZAIDI: Diogo Jota afariki kwa ajali akiwa na miaka 28 | Liverpool yatoa taarifa, ameacha mke na watoto
Atua England, auwasha moto Newcastle United

Tangu kujiunga na Newcastle United kuanzia mwaka 2022–2025), rekodi za staa huyo zimetikisa ambapo ni kama ifuatavyo:
2022‑23: Premier League mechi 22, magoli 10; jumla mechi 27, magoli 10.
2023‑24: Premier League mechi 30, magoli 21; jumla mechi 40, magoli 25.
2024‑25: Premier League mechi 34, magoli 23; jumla mechi 42, magoli 27.
Kutokana na rekodi hizo zinamfanya Isak awe amefunga jumla ya magoli 54, katika mechi 86 alizoichezea Newcastle kwenye Premier League. Jumla ya mechi 109 aliweza kufunga mabao 62 tangu atue ndani ya timu hiyo. Takwimu zake za mashindano yote, zinamfanya kuwa miongoni mwa washambuliaji wa kutisha duniani kwa sasa. Ikumbukwe tangu 2017 hadi Machi 2025, amefunga magoli 16, katika mechi 52 za timu ya taifa ya Sweden.
Alexander Isak atua Liverpool, avunja rekodi ya usajili EPL

Taarifa mbalimbali zilizolipotiwa nchini England, ikiwemo kituo cha matangazo cha Sky Sports zimethibitisha kuwa Liverpool wamekubaliana na Newcastle United kumnunua Isak. Biashara hiyo inatajwa kuvunja na kuandika rekodi ya Uhamisho ghali zaidi England. Hii ni baada ya kuandikisha dau la takribani £125 milioni ya awali na nyongeza mpaka kufikia £130 milioni.
Isak anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka sita na Liverpool. Taarifa ambazo pia zimethibitishwa na jarida la The Sun, na mwandishi maarufu wa Habari za michezo Fabrizio Romano. Fabrizio amethibitisha hayo kupitia ripoti za Omni/Swedish news.
SOMA HII PIA: Chelsea VS Liverpool- Nani kuibuka kidedea?
Isak agomea mazoezi na mechi za EPL za Newcastle United akishinikiza uhamisho wake

Awali iliripotitwa kuwa Newcastle haikutaka kuuza Isak isipokuwa pale tu, itakapopewa ada ya hadi £150 milioni. Licha ya mapingamizi hayo, Fabrizio alisema kuna uwezekano wa asilimia 60 wa uhamisho kufanyika. Changamoto kubwa ilikuja kwa ofa ya mshahara wa £300,000 kwa wiki aliohitaji staa huyo. Mazungumzo yalijibu changamoto hiyo.
Baada ya Newcastle United kuweka ngumu kumuachia, staa huyo, aliweka mgomo wa kuhudhuria mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya ‘Pre-season’. Kama hiyo haitoshi, aligomea pia kushiriki kwenye michezo ya awali ya msimu mpya. Hii yote akishinikiza mabosi wake wamuachie.
Hitimisho
Historia imeandikwa Alexander Isak atua Liverpool kwa uhamisho wa rekodi EPL. Safari ya soka kutoka AIK hadi Liverpool, kupitia vilabu mbalimbali ulaya kama Dortmund, Sociedad na Newcastle imefanikiwa. Isak sasa anaingia Anfield akiwa na rekodi bora, uwezo mkubwa na matarajio makubwa.
Pata habari za sasa za uhamisho za EPL kupitia SportPesa blog

