Chelsea vs Manchester CityChelsea vs Manchester City
  • Baada ya matokeo ya Arsenal 1-2 Bournemouth siku ya jana Jumamosi, ligi Kuu England hapatoshi leo Jumapili.
  • Ni Chelsea vs Manchester City, mechi ambayo huenda inakwenda kutoa mwelekeo mpya wa ubingwa wa Ligi Kuu EPL.
  • Mechi hii inatarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Stanford Bridge, London England, huku timu hizo zikikumbuka matokeo ya sare ya 1-1 katika mchezo wao wa mzunguko wa kwanza.

Mechi kubwa itapigwa leo Jumapili kwenye Uwanja wa Stanford Bridge, London England. Ni Chelsea vs Manchester City, mechi ambayo inakwenda kutoa mwelekeo mpya wa ubingwa wa Ligi Kuu EPL. Baada ya matokeo ya Arsenal 1-2 Bournemouth siku ya jana Jumamosi, Manchester City leo wana nafasi ya kupunguza pengo la pointi mpaka kufikia leo kufikia 7. Ikumbukwe pia Manchester City ana pungufu ya michezo miwili kulinganisha na vinara Arsenal.

SOMA HII PIA: Chelsea FC- Fixtures, Schedule & Scores

Bado haujashinda na SportPesa? Cheza mchezo wa aviator ‘Kindege’ uvune mpaka milioni 800 sasa

Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi milioni 800 muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Sportpesa Aviator- 800Mil

Chelsea vs Manchester City h2h

haaland vs Chelsea
haaland vs Chelsea

Timu hizi zimekutana katika michezo 181 jumla, ambapo Chelsea wana rekodi bora ya matokeo ya ujumla kwa faida ya michezo 3, ambapo wameshinda mechi 71. Manchester City wao wameibuka na ushindi katika michezo 68, huku michezo 45 ikiisha kwa matokeo ya sare. Mara ya mwisho kwa timu hizi kukutana ilikuwa Jan 4, 2026 ambapo mchezo huo uliisha kwa matokeo ya sare ya bao 1-1.

Vikosi vinavyotarajiwa Chelsea vs Manchester City

Chelsea

Kipa: Sanchez

Walinzi: Gusto, Fofana, Adarabioyo, Cucurella

Viungo: Santos, Caicedo; Neto, Palmer, Estevao

Mshambuliaji: Pedro

Manchester City

Kikosi cha Manchester City
Kikosi cha Manchester City

Kipa: Donnarumma

Walinzi: Nunes, Khusanov, Guehi, O’Reilly

Viungo: Silva, Rodri, Semenyo, Cherki, Doku

Mshambuliaji: Haaland

Habari za timu

Chelsea vs Manchester City
Mwenendo Vita ya ubingwa

Hili ni pambano kubwa la Premier League leo Jumapili, ambapo Chelsea FC wanaowania nafasi ya kucheza UEFA Champions League wakikabiliana na Manchester City ambao wanauwinda ubingwa. Timu zote mbili zilirejea kutoka mapumziko ya kimataifa kwa ushindi mkubwa katika mashindano ya FA Cup. Chelsea ya kocha, Liam Rosenior iliifunga Port Vale mabao 7, huku timu ya Pep Guardiola ikiichapa Liverpool 4-0.

Chelsea wametoka kupoteza mechi 4 mfululizo, kabla ya ushindi huo mkubwa dhidi ya timu ya Daraja la 3.  Ikicheza bila, Enzo Fernandez Chelsea waliichapa Port Vale 7-0 ugenini na kujihakikishia nafasi ya nusu fainali dhidi ya Leeds United katika dimba la Wembley. Licha ya ushindi huo, presha bado ipo kwa Rosenior, hasa kufuatia sakata la Fernandez na Real Madrid, ambapo mchezaji huyo anatumikia adhabu ya ndani ya mechi 2.

Manchester City wanatafuta ushindi wa tatu mfululizo bila kuruhusu bao, baada ya mafanikio yao katika hatua ya mtoano ya mashindano mengine. Ushindi wa 2-0 dhidi ya Arsenal ulimfanya Guardiola kuweka rekodi ya kushinda Kombe la Ligi mara tano, huku ushindi mwingine dhidi ya Liverpool ukichangiwa na hat-trick ya Erling Haaland ambayo ni ya 12 tangu ajiunge na klabu hiyo mwaka 2022. Ingawa Manchester City wako nyuma kwa pointi tisa dhidi ya Arsenal, City bado wana mechi 2 mkononi na wanatarajia kuvaana na Arsenal wiki ijayo.

SOMA HII ZAIDI: Manchester United vs Chelsea ‘live’: h2h, Vikosi, Muhtasari, Amorim kufukuzwa kazi?

Taarifa za wachezaji majeruhi na watakaokosa mechi

Chelsea

Enzo
Enzo

Kocha wa Chelsea, Liam Rosenior amethibitisha kuwa Fernandez hatakuwepo, hii ni kutokana na adhabu ya ndani. Pamoja na Fernandez na wachezaji walioumia ambao wanatarajia kukosa mchezo huu ni; Reece James, Levi Colwill, Jamie Bynoe-Gittens, Filip Jorgensen, Trevoh Chalobah. Habari njema kwa Chelsea ni uwezekano wa kurejea kwa Benoit Badiashile.

Manchester City

Majeruhi wa City wako zaidi kwenye safu ya ulinzi ambapo mastaa kama;

Ruben Dias, Josko Gvardiol wanaendelea kukosekana. Mlinzi mwingine, John Stones anaweza kurejea mazoezini. Pia, Bernardo Silva anaweza kuweka rekodi ya kucheza mechi nyingi zaidi za Premier League kwa mchezaji wa Ureno (297) ikiwa atacheza leo.

SOMA HII PIA: Chelsea FC: Habari za Hivi Karibuni, Ratiba, Taarifa ya Kikosi na Maarifa ya Kubashiri

Utabiri

Chelsea vs Manchester City, huu ni zaidi ya mchezo, hii ni vita kubwa ya timu mbili zinazoonekana kuwa na malengo makubwa mawili tofauti. Manchester wanautaka ubingwa wa EPL, huku Chelsea wakiisaka nafasi ya kumaliza ndani ya 5 bora ili kufuzu Ligi ya mabingwa Ulaya msimu ujao. Kwa kuangalia fomu ya timu hizi mbili Manchester City wanatabiriwa kushinda kwa angalau mabao 3.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.