TRA United kiboko ya vigogo NBC Premier League 2025/26 | Simba SC na Yanga SC zakwama | Highlights, kadi nyekundu, msimamo

ByLunyamadizo Mlyuka

April 9, 2026
TRA United kiboko ya vigogo NBC Premier LeagueKapombe vs TRA UnitedKapombe vs TRA United
  • Simba SC yaachwa pointi 8 na Yanga SC, kiporo hakijalika Arusha
  • TRA United kiboko ya vigogo NBC Premier League 2025/26
  • Aprili 9, 2026 matokeo ya hivi punde TRA United 0-0 Simba SC, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid
  • Valentino Nouma aonyeshwa kadi nyekundu dakika ya 87 ya mchezo

TRA United kiboko ya vigogo NBC Premier League 2025/25 kwa kugawa dozi na kuvuna pointi nyumbani. Aprili 9, 2025 matokeo rasmi ni TRA United 0-0 Simba SC. Machi 18, 2026 ilikuwa TRA United 0-0 Yanga SC. Wakusanya mapato chini ya Kocha Mkuu, Ettiene Ndayiragije wamewasumbua vigogo Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

SOMA HII: TRA United yaibana mbavu Yanga SC NBC Premier League/ Highlights, statics, standings

Je, bado hujashinda mamilioni? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune pesa sasa

Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Aviator game jackpot banner TSh 800 Million prize

TRA United kiboko ya vigogo NBC Premier League 2025/25

TRA United kiboko ya vigogo NBC Premier League
TRA United vs Simba SC NBC Premier League 2025/26

TRA United kiboko ya vigogo NBC Premier League 2025/26 wakiwa nyumbani kwa kuwazuia kupata pointi tatu. Aprili 5, 2026 ilikuwa TRA United 2-0 Singida Black Stars wakishusha dozi kwa vigogo wa Singida. Wababe hawa kwenye mechi kubwa tatu wakiwa nyumbani hawajapoteza msimu wa 2025/26.

Ni mechi 9 imecheza ikiwa nyumbani NBC Premier League. Ushindi ni mechi 4 ikipoteza mchezo mmoja na kupata sare 4. Ni nafasi ya 7 kwenye msimamo kwa matokeo ya nyumbani pekee ikivuna pointi 16.

Simba SC yaachwa pointi 8 na Yanga SC

TRA United kiboko ya vigogo NBC Premier League
Vinara wa NBC Premier League 2025/26 Yanga SC.

Simba SC yaachwa pointi 8 na Yanga SC NBC Premier League 2025/26 baada ya kuangusha pointi mbili. Aprili 9, 2026 mnyama alikuwa ugenini dhidi ya wakusanya mapato. TRA United imekutana kwenye mechi mbili na mnyama.

Katika mchezo uliochezwa Dar matokeo ilikuwa Simba SC 3-0 TRA United. Mchezo wa ugenini wamegawana pointi. Kwenye mtanange wa leo Valentino Nouma wa TRA United alionyeshwa kadi nyekundu.

SOMA HII: Simba SC 3-0 TRA United highlights, H2H, standings, twakimu | Matokeo ya NBC Premier League

Aviator game jackpot banner TSh 800 Million prize

Takwimu mchezo wa TRA United 0-0 Simba SC

TRA United kiboko ya vigogo NBC Premier League
TRA United vs Simba SC, NBC Premier League.
TRA United Simba SC
10Mashuti10
4Lenga lango6
39%Umiliki61%
6Mashuti yasiyolenga lango4
1Kadi nyekundu0
1Kadi ya njano1
5Kona4
0Magoli0

Walioonyeshwa kadi za njano

Valentino Nouma wa TRA United kadi njano za mbili dakika ya 82 na 87. Kadi hizo zikapelekea kuonyeshwa kadi nyekundu. Nickson Kibabage wa Simba SC alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 66.

Msimamo wa NBC Premier League 2025/26

 Msimamo wa NBC Premier League uliobereshwa muda huu. Simba SC nafasi ya pili pointi 36. TRA United nafasi ya 7 pointi 24.

POSMPWDLPTS
Yanga SC18135044
Simba SC17106136
3. Azam FC18810034
4. JKT Tanzania1878329
5.Singida Black Stars1884628
6.Pamba Jiji FC1868426
7.TRA United1866624
8. Dodoma Jiji FC1866624
9.Mtibwa Sugar1858523
10.Namungo FC1857622
11.Mashujaa FC1848620
12.Mbeya City1845917
13.Coastal Union1837816
14.Fountain Gate1744916
15.Tanzania Prisons18341113
16. KMC FC1822148

SOMA HII: Yanga SC: Historia, Usajili wote, kikosi, Ratiba, Matokeo na Takwimu

Hitimisho

TRA United kiboko ya vigogo NBC Premier League 2025/26. Katika timu mbili zilizo nafasi ya kwanza na ile ya pili hakuna iliyopata pointi tatu ugenini. Vinara ni Yanga SC wakiwa na pointi 44 waliangusha pointi mbili mbele ya wakusanya mapato.

Share this: