- Utovu wa nidhamu wamponza mlinda mlango namba moja wa Yanga SC
- Djigui Diarra wa Yanga SC amefungiwa mechi 3 na TPLB
- Waamuzi Mtibwa Sugar 1-1 Yanga SC wafungiwa, mmoja ashushwa daraja
- Ali Kamwe afunguka kuhusu adhabu na makipa watakaobeba mikoba ya Diarra
Djigui Diarra wa Yanga SC amefungiwa mechi 3 na TPLB (Bodi ya Ligi Kuu Tanzania). Matukio ya utovu wa nidhamu Mtibwa Sugar 1-1 Yanga SC, Uwanja wa Jamhuri, Dodoma ni sababu. Mbali na kufungiwa pia ametozwa jumla ya milioni kwa makosa tofauti.
SOMA HII: Kariakoo Dabi vita ya Diarra na Camara inaanza | Takwimu, mechi, magoli | Septemba 16 2025
Paisha Kindege cha SportPesa uvune mamilioni sasa hivi
Muda ni sasa kushinda mamilioni ukicheza mchezo wa Aviator. Ni rahisi sana kwa kila rubani kuvuna mamilioni. Cheza sasa upate mgao wako bila chenga ni rahisi sana

Djigui Diarra wa Yanga SC amefungiwa mechi 3 na TPLB

Mlinda mlango Djigui Diarra wa Yanga SC amefungiwa mechi 3 na TPLB. Adhabu hiyo imetokana na mechi namba 126. Diarra ni mlinda mlango namba moja akiwa anaongoza kwa hati safi, (clean sheet) anazo 10.
Mchezo huo ulichezwa Machi 21, 2026 Dodoma walipogawana alama mojamoja. Goli la Yanga SC lilifungwa na Pacome Zouzoua. Mtibwa Sugar walipata goli kupitia kwa Ismael Mhesa.
Hizi hapa adhabu alizopewa Diarra
Diarra raia wa Mali mwenye miaka 31 amepewa adhabu yakufungiwa mechi 3 na kutozwa faini ya Sh. 2,000,000 (Milioni mbili) kwa kosa la kumshambulia mwamuzi baada ya mchezo kumalizika. (Kwa mujibu wa Kanuni ya 41:5(5.3). Pia ametozwa faini ya milioni mbili kwa kosa la kuonyesha kidole cha kati wakati akitoka uwanjani, kitendo kinachotafsiriwa ni utovu wa nidhamu. Kwa adhabu zote jumla ametozwa faini ya milioni 4.
SOMA HII: Mtibwa Sugar watibua mabadiliko Yanga SC / Mhesa na Pacome goal 2025/26 / Highlights, standings

Mechi ambazo Diarra atakosekana NBC Premier League
Yanga SC vs Tanzania Prisons, Aprili 4,2026. Mchezo huu Yanga SC watakuwa nyumbani, Uwanja wa KMC Complex. Mzunguko wa kwanza alianza Diarra ugenini waliposhinda kwa goli 1-0.
Pamba Jiji FC vs Yanga SC, Aprili 8,2026. Wananchi watakuwa ugenini. Mchezo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Yanga SC vs Mbeya City, Aprili 16,2026. Mabingwa watetezi watakuwa nyumbani. Uwanja wa KMC Complex.
Ali Kamwe, maoni kuhusu Diarra

Ali Kamwe, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Yanga SC amesema: “Diarra golikipa bora wa muda wote Ligi Kuu ya Tanzania amefungiwa mechi tatu. Tumejiandaa vizuri kwa kuwa tuna makipa wengine wawili ambao ni bora, Hussen Masalanga na Aboutwalib Mshery.
“Mshery amekuwa akipata clean sheet kwenye mechi alizocheza, amefungiwa Diarra tutakwenda kuongea naye na makipa waliobaki watahakikisha tunacheza michezo yetu na kupata matokeo mazuri,”.
Waamuzi Mtibwa Sugar 1-1 Yanga SC wafungiwa
Kwenye taarifa hiyo ya TPLB imeeleza kuwa Gilbert Mrina Mwamuzi wa Kati mchezo wa Mtibwa Sugar 1-1 Yanga SC ameshushwa daraja la uamuzi. Sababu kushindwa kuchukua hatua dhidi ya mlinda mlango Djigui Diarra baada ya mechi. Adhabu hii imezingatia kuwa hili ni kosa la kujirudia kwa kuwa aliwahi kufanya hivyo mchezo namba 65, Mbeya City vs Namungo FC na akaadhibiwa kufungiwa mizunguko mitatu.
Abdulaziz Ally, Mwamuzi Msaidizi Namba 2 kutoka Arusha amefungiwa mizunguko mitano (5) ya Ligi Kuu kwa kosa la kushindwa kutafsiri sheria ya kuotea (offside). Ally alimnyooshea kibendera Emmanuel Mwanengo wa Yanga katika dakika ya 36 akidai ameotea, hata hivyo hakukuwa na kosa la kuotea kwa mujibu wa sheria za mpira wa miguu.
SOMA HII: TRA United yaibana mbavu Yanga SC NBC Premier League/ Highlights, statics, standings
Hitimisho
Djigui Diarra wa Yanga SC amefungiwa mechi 3 na TPLB ni pigo katika Idara ya ulinzi. Kwenye mechi tatu zijazo kutakuwa na mabadiliko kikosi cha kwanza. Ni Aboutwalib Mshery na Hussen Masalanga huenda watakuwa langoni.

