- Mtibwa Sugar vs Yanga SC ni mchezo unaofuata Machi 21,2026 Uwanja wa Jamhuri, Dodoma
- Uchovu wa Yanga SC utawapa faida Mtibwa Sugar?
- Pedro Goncalves, Kocha Mkuu wa Yanga SC ataja changamoto ya ugumu wa ratiba
Uchovu wa Yanga SC utawapa faida Mtibwa Sugar? Ni swali ambalo linasubiri majibu kuelekea mchezo wa NBC Premier League kesho Machi 21, 2026 Uwanja wa Jamhuri, Dodoma. Hii ni baada ya Pedro Goncalves Kocha Mkuu wa Yanga SC kubainisha wanapitia ratiba ngumu.
Cheza na ushinde sasa na ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni muda huu
Hujashinda na kindege cha SportPesa? Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kubashiri SportPesa bonyeza picha hii chini.

Uchovu wa Yanga SC utawapa faida Mtibwa Sugar?

Kutokana na mabingwa watetezi kucheza mechi ngumu mfululizo wachezaji wanapitia kipindi kigumu. Uchovu wa Yanga SC utawapa faida Mtibwa Sugar? Kesho wababe hawa wanatarajia kupambana kwenye mchezo wa NBC Premier League.
Mtibwa Sugar wamepata muda mrefu wa kupumzika. Machi 8,2026 ulikuwa ni mchezo wao wa ushindani uliopita. Mtibwa Sugar 0-1 Mbuni wakiondolewa CRDB Federation Cup. Yanga SC Machi 18, 2026 walitoka kucheza mchezo dhidi ya TRA United.
Maoni ya Kocha wa Yanga SC, Pedro

“Maandalizi yetu kuelekea mchezo wa kesho yamekuwa na changamoto kubwa. Tulitoka Arusha jana baada ya safari ndefu na tulipowasili hapa, wachezaji wengi walifanya mazoezi ya kurejesha nguvu (recovery), huku wengine wakifanya mazoezi mepesi uwanjani.
“Kwa kipindi cha wiki tatu hadi nne zilizopita tumekuwa na ratiba ngumu. Mchezo wa kesho utakuwa wa saba ndani ya siku 21 jambo ambalo ni changamoto kubwa. Pia tunapaswa kuzingatia kuwa baadhi ya wachezaji wako kwenye mfungo wa Ramadhani pamoja na safari za mara kwa mara kwa ujumla tunapitia kipindi kigumu sana cha msimu,”.
SOMA HII: Ratiba ya Yanga SC 2025/26 ni moto/ Mechi 5 NBC Premier League ugenini/ Msimamo, matokeo

Maoni ya kocha wa Mtibwa Sugar
Awadhi Juma, kocha msaidizi wa Mtibwa Sugar amebainisha kuwa wapo tayari kwa mchezo dhidi ya Yanga SC. Aliongeza maandalizi yanakwenda vizuri na wanatambua ugumu wa mpinzani wao.
“Morali ipo juu kwa asilimia mia moja. Tumecheza michezo mingi Uwanja wa Jamhuri na tumepata matokeo, mechi nyingine tumekosa. Tumepata muda wa kurudi katika kiwanja cha mazoezi na kufanyia kazi nina amini tutakuwa imara. Tuna wachezaji zaidi ya 7 ambao watakosekana kwenye mchezo wetu.
“Ambacho tunakifanya ni kuwaandaa wale waliopo kwa ajili ya kufanya kazi kwenye mchezo wetu. Hatujapata matokeo mchezo wetu wa CRDB Federtion Cup hivyo makosa tutafanyia kazi,”.
Msimamo wa Mtibwa Sugar vs Yanga SC

| POS | MP | W | D | L | PTS |
| 1. Yanga SC | 15 | 11 | 4 | 0 | 37 |
| 10.Mtibwa Sugar FC | 16 | 5 | 5 | 5 | 21 |
SOMA HII: Yanga SC haijapoteza mechi 2025/26 NBC Premier League / Kariakoo Dabi inanukia, matokeo, rekodi

Aziz Andabwile afungukia kwa niaba ya wachezaji
“Kwa niaba ya wachezaji wenzangu, tunatambua vyema umuhimu wa mchezo wa kesho, na tutaingia uwanjani kwa juhudi na ari ya hali ya juu, hususan tukizingatia matokeo tuliyoyapata katika michezo iliyopita.
Licha ya kuwa na ratiba ngumu pamoja na changamoto ya majeruhi, dhamira yetu sote ni moja kuhakikisha kwamba katika kila mchezo tunapata alama tatu,”.
Hitimisho
Uchovu wa Yanga SC utawapa faida Mtibwa Sugar? Wapinzani wao ni wagumu kuacha pointi 3 uwanjani 2025/26. Wananchi hawajapoteza kwenye mechi 15 mfululizo ndani ya ligi. Walima miwa wamepoteza mechi 5 kati ya 16, watatoboa mbele ya wananchi?

