Yanga SC 2-0 Mtibwa Sugar NBC Premier LeagueZimbwe (-)
  • FT: Yanga SC 2-0 Mtibwa Sugar NBC Premier League Oktoba 28,2025 Uwanja wa KMC Complex.
  • Zimbwe Jr na Celestin Ecua wafunga magoli makali wakiwa nje ya 18.
  • Kocha mpya wa Yanga SC Pedro Goncalves mrithi wa mikoba ya Romain Folz ameanza kazi rasmi.

Yanga SC 2-0 Mtibwa Sugar NBC Premier League matokeo rasmi ya mchezo uliochezwa Uwanja wa KMC Complex. Ni mchezo wa tatu kwa mabingwa watetezi Yanga SC kushuka uwanjani, wakishinda mechi mbili na kuambulia sare mchezo ya 0-0 dhidi ya Mbeya City. Iliwachukua dakika 38 kuzifumania nyavu za mpinzani kupitia kwa beki Mohamed Hussen Zimbwe Jr ambaye amechaguliwa kuwa mchezaji.

SOMA HII: Yanga SC vs Mtibwa Sugar NBC Premier League Oktoba 28,2025/ H2H, live score, vikosi

Cheza na ushinde sasa na ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni muda huu

Hujashinda na kindege cha SportPesa? Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kubashiri SportPesa bonyeza picha hii chini.

image

Yanga SC 2-0 Mtibwa Sugar NBC Premier League magoli yamefungwa kwa mtindo gani?

Yanga SC 2-0 Mtibwa Sugar NBC Premier League
Yanga vs Mtibwa Sugar mchezo wa Ligi Kuu Bara, Uwanja wa KMC. Source: Yanga SC.

Yanga SC 2-0 Mtibwa Sugar NBC Premier League magoli yamefungwa kwa mtindo wa kushtukiza. Baada ya dakika 30 majaribio kukutana na ukuta wa Mtibwa Sugar, mbinu zilibadilishwa. Wachezaji wa Jangwani walianza kutuma makombora wakiwa nje ya 18.

Jaribio la beki Mohamed Hussen Zimbwe Jr dakika ya 38 lilileta goli. Kipindi cha pili dakika ya 83 Celestin Ecua naye alifunga goli la pili akiwa nje ya 18. Mpaka kipyenga kinapulizwa, magoli hayo yalidumu mpaka mwisho wa mchezo.

Kocha Mkuu Yanga SC ameanza kazi kwa ushindi

Kocha Mkuu wa Yanga SC, Pedro Goncalves mchezo wake wa kwanza kaanza kwa ushindi. Huyu ni mrithi wa mikoba ya Romain Folz ambaye alifutwa kazi. Amekaa kwenye benchi kwa mara ya kwanza rasmi Oktoba 28,2025 na kushuhudia timu ikipata ushindi.
Mchezo wa mwisho kwa Romain ilikuwa katika Ligi ya Mabingwa Afrika uliochezwa nchini Malawi dhidi ya Silver Strikers. Mchezo huo ulikuwa ni wa Ligi ya Mabingwa Afrika. Mara baada ya mchezo huo uongozi wa Yanga SC ulitoa taarifa ya kuvunja mkataba na kocha huyo.

Msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara

  1. Mbeya City, pointi 8 baada ya kucheza mechi 6
  2. Pamba Jiji, pointi 8 baada ya kucheza mechi 5
  3. Mashujaa FC, pointi 8 baada mechi 6.
  4. Yanga SC, pointi 7 baada yakucheza mechi 3
  5. JKT Tanzania, pointi 7 mechi 5.

Kikosi cha Yanga SC vs Mtibwa Sugar

Kipa

Djigui Diarra

Mabeki

Israel Mwenda

Zimbwe Jr

Dickson Job

Bakari Nondo

Viungo

Duke Abuya

Maxi Nzengeli

Mohamed Doumbia

Offen Chikola

Edmund John

Mshambuliaji

Dube

Wachezaji wa akiba

Yanga SC vs Mtibwa Sugar
Prince Dube mshambuliaji wa Yanga SC kwenye mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar. Source: Yanga SC.

Aboutwalib Mshery, Balla Conte, Lassine Kouma, Ecua Elastine, Chadraclk Boka, Aziz Andambwile, Frank Assink, Andy Boyel, Abdulnassir Abdallah, Abubakar Othman.

SOMA HII: Matokeo ya Yanga SC 2025/26 | Wafungaji, magoli, ratiba ya mechi zijazo

image

Kikosi cha Mtibwa Sugar kilichoanza dhidi ya Yanga SC

Yanga SC KMC
Yanga SC vs Mtibwa Sugar, Uwanja wa KMC. Source: Yanga SC.

Costantine Malimi

Erick Kyaruzi

Haroun Evod

Omar Selemani

Ibrahim Imoro

Kassim Msafiri

Twalibu Muhenga

Omary Marungu

Abdul Hilary

Datius Peter

Nassor Kiziwa

Wachezaji wa akiba

Ezekia Mwashilindi

Omary Manga

Chkwuemeka Collins

Ismail Mhesa

Juma Nyangi

Toba Kutisha

Onesmo Mayaya

George Chota

Laurent Alfred

Samuel Martin

SOMA HII: Beki Ibrahim Bacca wa Yanga SC amefungiwa mechi 5 na TPLB

image

Hitimisho

Yanga SC 2-0 Mtibwa Sugar NBC Premier League kila timu ilikuwa inazitolea macho pointi tatu. Ikumbukwe kwamba mchezo uliopita wa ligi Yanga SC ilivuna pointi moja ugenini kwa Mbeya City. Mtibwa Sugar katika mechi 5 imeambulia ushindi mchezo mmoja, kipigo mechi 2 na sare mechi 2.

Share this: