- Vita ya kisasi na rekodi itapigwa usiku wa leo kwenye hatua ya 16 bora ya mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA Champions League).
- Ni mchezo mkali wa mabingwa watetezi wa mashindano hayo Paris Saint-Germain vs Chelsea.
- Hii ni mara ya kwanza timu hizi zinakutana tangu fainali ya ‘club world cup’, yaani mashindano ya kombe la dunia la klabu kule USA.
- Je, PSG watalipa kisasi, au Chelsea wataendeleza rekodi? Makala hii inakupa dondoo muhimu kuhusu mechi hiyo.
Paris Sait-Germain vs Chelsea Kitaumana leo! ni katika vita ya kisasi na rekodi kwenye hatua ya 16 bora ya mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA Champions League). Mchezo huu utapigwa kwenye Uwanja wa Parc des Princes, jijini Paris-Ufaransa. Hii ni mara ya kwanza kwa timu hizi kukutana tangu fainali ya ‘club world cup’, yaani mashindano ya kombe la dunia la klabu kule USA. PSG watalipa kisasi cha kufungwa mabao 3-0? Makala hii inakupa dondoo muhimu kuhusu mechi hiyo.
SOMA HII PIA: Chelsea FC: Habari za Hivi Karibuni, Ratiba, Taarifa ya Kikosi na Maarifa ya Kubashiri
Je, hujashinda mamilioni ya SportPesa?
Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Bashiri na SportPesa uvune mkwanja sasa hivi kwa kubonyeza picha hapo chini.

Paris Saint-Germain vs Chelsea h2h

Kama ilivyo kwa Real Madrid na Manchester City, hakuna mbabe wa rekodi kati ya Paris Saint-Germain na Chelsea. Hii ni baada ya kukutana mara 9, ambapo kila timu imeshinda mechi 3. Mechi tatu zilizosalia ziliisha kwa matokeo ya sare, hivyo matokeo yoyote ya leo yanatarajiwa kuandika historia mpya ya timu hizi.
Vikosi vinavyotarajia kuanza Paris Saint-Germain vs Chelsea
Paris Saint-Germain

Kipa: Safonov
Walinzi: Hakimi, Zabarnyi, Pacho, Mendes
Viungo: Neves, Vitinha, Zaire-Emery
Washambuliaji: Doue, Dembele, Kvaratskhelia
Chelsea

Kipa: Sanchez
Walinzi: James, Fofana, Chalobah, Cucurella
Viungo: Caicedo, Santos, Palmer, Fernandez,
Washambuliaji: Neto, Pedro
SOMA HII ZAIDI: FIFA Club World Cup 2025 yatikisa kwa matukio | Cole Palmer gumzo | Kocha PSG afungukia vurugu
Taarifa za timu kuelekea mechi ya Paris Saint-Germain vs Chelsea

Chelsea wanavaana na Paris Saint‑Germain, katika mechi ya mkondo wa kwanza hatua ya 16 bora itakayochezwa leo Jumatano usiku Uwanja wa Parc des Princes. Hii ni mara ya kwanza kwa timu hizi mbili kukutana, tangu fainali ya FIFA Club World Cup ya 2025 kule USA. Kumbukumbu iliyowashuhudia Chelsea ikiwaduwaza PSG kwa kuifunga mabao 3-0, ambapo Cole Palmer alifunga mabao 2 na kuasisti bao 1.
Kama ilivyokuwa msimu uliopita walipokuwa wakielekea kushinda taji lao la kwanza kabisa la Champions League, Paris Saint-Germain hawakufuzu moja kwa moja hatua ya 16 bora. Msimu huu wamemaliza nafasi ya 11, katika hatua ya ligi na kulazimika kucheza hatua ya playoff ya mtoano.
Kwenye ligi PSG wanaongoza msimamo kwa tofauti ya pointi 1 tu, mbele ya RC Lens. Hali hiyo imewafanya PSG kuwa kwenye presha kubwa, kuelekea kutetea ubingwa wao wa ligi zikiwa zimebaki mechi tisa tu, kumaliza ligi.
PSG wana rekodi nzuri dhidi ya timu za England, wakiwa wamepoteza mechi moja tu kati ya nane za mwisho dhidi ya timu kutoka England. Katika mashindano ya UEFA wameshinda mara 5 na kupata sare 2, dhidi ya timu za EPL.
Kabla ya kujiunga na Chelsea mwezi Januari, kocha Rosenior aliiongoza RC Strasbourg kwa miezi 18. Katika kipindi hiko alipata matokeo mchanganyiko dhidi ya PSG, ushindi mmoja, sare moja na kipigo kimoja. Chelsea pia wana rekodi nzuri dhidi ya timu za Ufaransa, katika mashindano ya UEFA, wakishinda mechi zao sita za mwisho dhidi ya wapinzani wa Ligue 1.
SOMA HII ZAIDI: Fifa World Cup 2026: Bingwa kuzoa Bilioni 123
Taarifa za majeruhi
Paris Saint-Germain

Fabian Ruiz (goti), Quentin Ndjantou (misuli ya nyuma ya paja). Joao Neves ameanza kupona jeraha la kifundo cha mguu, na huenda akacheza ikiwa atafaulu vipimo vya mwisho vya afya. Kocha Luis Enrique pia anaweza kumrudisha nahodha Marquinhos, au kuendelea na mabeki wa kati Illia Zabarnyi na William Pacho. Ousmane Dembele, ambaye amefunga mabao 11 msimu huu, anaweza kuanza katika safu ya ushambuliaji pamoja na Desire Doue na Khvicha Kvaratskhelia.
Chelsea
Kwa upande wa Chelsea, Estevao Willian, Jamie Gittens, Levi Colwill na Mykhaylo Mudryk wanaendelea kuuguza majeraha. Wesley Fofana anatarajiwa kurejea na kucheza pamoja na Trevoh Chalobah, katika safu ya ulinzi. Viungo Enzo Fernandez na Andrey Santos wanaweza kuanza pamoja na Moises Caicedo, huku Cole Palmer akicheza upande wa kulia wa ushambuliaji.
Mshambuliaji, Joao Pedro ambaye yuko kwenye kiwango kizuri amefunga mabao 11 katika mechi 12 za mwisho anatarajiwa kuanza.
Hitimisho na Utabiri
Paris Saint-Germain vs Chelsea pale Parc des Princes moto utawaka. Swali ni je, nani atachanga karata zake vizuri. Upo uwezekano mkubwa wa mchezo huu kuisha kwa matokeo ya sare. Mchezo unatarajiwa kuwa na mabao kwani PSG hawajawahi kuwa na sare ya 0-0, katika hatua ya mtoano ya Champions League katika mechi 58 walizocheza.

