- Chelsea FC 3-0 PSG FIFA Club World Cup dunia yapata ganzi kwa muda kutokana na maajabu ya mpira na matokeo ndani ya dakika 90.
- Cole Palmer kwenye mchezo mkubwa wa fainali afunga mabao mawili mbele ya PSG iliyowasambaratisha Real Madrid.
- Rais wa Marekani Donald Trump agawa zawadi, matukio yote alifuatilia mwanzo mwisho kwenye fainali.
Chelsea FC 3-0 PSG fainali ya FIFA Club World Cup 2025. Mabingwa wapya wa mashindano haya makubwa wanatoka England baada ya ushindi ulioshangaza dunia. Paris Saint Germain, (PSG) hawa walikuwa wanapewa chapuo kubwa kutwaa taji hilo.

Soma hii:Chelsea yarudi ‘Top Four’ kwa kishindo, ‘London is Blue’
Mamilioni yanakusubiri sasa.
Paisha kindege sasa uvune mamilioni. Ni rahisi ukicheza Aviator washindi kila saa wanavuna zawadi zao. Muda wako ni huu uwahi mgao wako.

Ikumbukwe kwamba mashindano haya yalianza kutimua vumbi Juni 14. Fainali ilikuwa Julai 13 2025 ambapo ni Chelsea kutoka England ilivaana na PSG. Ilikuwa ni fainali yenye maajabu kwa kazi kumalizwa dakika 45 za mwanzo kwenye mchezo huo.
Hawa hapa watupiaji kwenye fainali

Soma hii: Premier League kumechangamka 2024/25 Chelsea vs Everton
Cole Palmer alionyesha ubabe wake kwenye mchezo huo kwa kufunga mabao mawili dakika 22 na 30 na alisaidia kutoa pasi ya bao moja lilifungwa na Joao Pedro dakika 43. Kazi iliisha kabla ya mapumziko. Joao Neves wa PSG alipewa kadi nyekundu baada ya kumvuta nywele Marc Cucurella dakika za mwisho za mchezo.
Mbinu za Chelsea kupitia kocha wao Enzo Maresca ziliwapiku Wana PSG walionyesha weledi wakufunga bao tatu za haraka kipindi cha kwanza na kushikilia msimamo hadi mechi ikafika tamati. The Blues walifanikiwa kupata kitita cha takribani paundi milioni mia moja kwenye msururu wa World Club Cup Final ikiwa na timu 32.
Luis Enrique alipata makasiriko baada ya kupoteza mchezo huo. Ilionekana walikuwa kwenye mzozo na Joan Pedro wa Chelsea. Licha ya kuonekana kwenye makasiriko hayo bado mabingwa Chelsea walifanya sherehe zao za ubingwa.
Mashindano yalivyokuwa mwendo wake
Kulikuwa na makundi 8 katika mashindano na viwanja 12 vilitumika kwa ajili ya mechi 63. Mechi hizo zilichezwa nchini Marekani ambao walikuwa wenyeji wa mashindano haya makubwa. Ni Julai 13 2025 bingwa mpya alipatikana.
Fainali ilichezwa Uwanja wa MetLife na mchezo wa ufunguzi ulichezwa Uwanja wa Miami’s Hard Rock.
Bingwa alitwaa taji la FIFA Club World Cup ambalo ni jipya ubunifu wake umepita kwa wataalamu wakubwa. FIFA wakishirikiana na Global Luxury Jeweller Tiffany & CO walihusika kwenye ubunifu wa taji hilo.
Shughuli za ushindani ilikuwa ni kutoka timu 32 ambazo zilishiriki mashindano hayo makubwa. Bara la Afrika pia kulikuwa na timu ambazo zilishiriki. Miongoni mwa hizo ni Al Ahly kutoka Misri na Mamelod Sundowns kutoka Afrika Kusini.
Afrika ni timu nne ambapo tatu zilipatikana kutoka CAF Champions League na moja kutokana na raking yao. Asia timu 4, Europe 12, America ya Kati timu 4, Oceania timu moja, America ya Kusini timu 6 na timu mwenyeji alitoa timu moja.
Rais Trump alishuhudia mwanzo mwisho

Rais wa Marekani, Donald Trump hakuondoka baada ya kukabidhi Kombe kwa washindi Chelsea. Trump alibaki na kushangilia ubingwa pamoja na mabingwa hao wapya wa FIFA Club World Cup (kombe la dunia la klabu). Mapema alithibitisha uwepo na alikuwepo uwanjani.
Trump alikuwa miongoni mwa waliojitokeza kushuhudia fainali ya Kombe la Dunia la Klabu kati ya Chelsea na PSG. Ipo wazi kwamba kwenye mchezo huo Chelsea ilishinda mabao 3-0. PSG walipishana na taji hilo kubwa. Rais Trump alisikika akisema kwa utani kuwa: “Ninabaki kusherehekea na nyie” baada ya hapo akawa anapiga makofi nahodha wa Chelsea aliponyanyua Kombe.
Tuzo kwa Cole Palmer
Cole Palmer amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Michuano ya Kombe la Dunia iliyotamatika Julai 13 nchini Marekani. Kiungo huyo alikuwa katika ubora kwenye mchezo wa fainali. Nyota huyo alifunga kabla ya timu kwenda mapumziko.
Palmer alihusika kwenye mabao yote matatu Chelsea waliyopata. Mbele ya PSG kwenye fainali alikuwa na siku nzuri kazini. Alikifunga mabao mawili na kutoa pasi moja ya bao. Ikumbukwe kwamba Chelsea walitinga fainali baada ya kuiondosha Fluminense ya Brazil 2-0. PSG iliwasambaratisha Real Madrid 4-0. Kwenye fainali PSG wakasambaratishwa.
Makundi yalivyokuwa
Kundi A
SE Palmeiras (BRA)
FC Porto (POR)
Al Ahly FC (EGY)
Inter Miami CF (USA)
Kundi B
Paris Saint-Germain (FRA)
Atlético de Madrid (ESP)
Botafogo (BRA)
Seattle Sounders FC (USA)
Kundi C
FC Bayern München (GER)
Auckland City FC (NZL)
CA Boca Juniors (ARG)
SL Benfica (POR)
Kundi D
CR Flamengo (BRA)
Espérance Sportive de Tunis (TUN)
Chelsea FC (ENG)
Los Angeles FC (USA)
Kundi E
CA River Plate (ARG)
Urawa Red Diamonds (JPN)
CF Monterrey (MEX)
FC Internazionale Milano (ITA)
Kundi F
Fluminense FC (BRA)
Borussia Dortmund (GER)
Ulsan HD (KOR)
Mamelodi Sundowns FC (RSA)
Kundi G

Soma hii: Stephane Aziz Ki huyoo Marekani kuwavaa Manchester City ya Guardiola
Manchester City (ENG)
Wydad AC (MAR)
Al Ain FC (UAE)
Juventus FC (ITA)
Group H
Real Madrid C. F. (ESP)
Al Hilal (KSA)
CF Pachuca (MEX)
FC Salzburg (AUT)
Hitimisho
Baada ya wapinzani kubainisha kuwa watapata ushindi mkubwa mbele ya Chelsea hali ilikuwa tofauti ndani ya uwanja. Licha ya ushindi mkubwa PSG waliopata mbele ya Real Madrid kwa mabao 4-0 hawakufua dafu kwenye fainali. Taji FIFA Club World Cup 2025 lilinyakuliwa kibabe na watoto kutoka Darajani, maarufu kwa jina la The Blues.


