- Moto unazidi kuwaka ndani ya Ligi Kuu Bara yaani NBC Premier League.
- Baada ya matokeo ya Singida Big Stars 1-2 Simba SC leo Jumatano, kesho Alhamisi utapigwa mchezo mwingine mgumu.
- Ni Tanzania Prisons vs Yanga SC, mchezo ambao unatarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Mambo yanazidi kuwa moto ndani ya NBC Premier League. Baada ya Simba SC kuibuka na ushindi muhimu vs Singida black Stars, Alhamisi hii ni zamu ya Tanzania Prisons vs Yanga SC. Mchezo huu muhimu unatarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma. Makala hii inakuchambulia dondoo muhimu kuhusu mchezo huo.
SOMA HII PIA: Tanzania Prisons 0-5 Yanga SC dakika 180 wapigwa nje ndani/ Kariakoo Dabi inakuja
Bado hujashinda? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa
Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Tanzania Prisons vs Yanga SC h2h
Rekodi zinaonyesha Yanga SC na Tanzania Prisons zimekutana katika michezo 27, ya mashindano tofauti. Yanga SC wamekuwa na rekodi bora dhidi ya wapinzani wao, hii ni baada ya kufanikiwa kuandikisha ushindi mara 19. Tanzania Prisons hawajawahi kuibuka na ushindi mbele ya Yanga SC, ambapo mechi 8 zilizosalia ziliisha kwa matokeo ya sare.
Kikosi cha Yanga SC kinachotarajia kuanza mchezo huu

Kuelekea katika mchezo huu Yanga SC itaendelea kukosa baadhi ya mastaa wao. Kuendana na mazoezi ya mwisho yaliyofanyika leo, Yanga SC wanatarajia kuanza na kikosi hiki;
Kipa: Djigui Diarra
Walinzi: Mwenda, Baka, Mwamnyeto, Mohammed Hussein
Viungo: Duke, Pacome, Maxi, Damaro na Okello
Mshambuliaji: Depu
SOMA HII ZAIDI: Seleman Mwalimu ametambulishwa Simba SC kwa mkopo akitokea Wydad | Takwimu zake, magoli
Kocha Yanga SC ataja wachezaji walio majeruhi

Kuelekea mchezo huo, kocha mkuu wa Yanga Pedro amesema: “Tumekuwa na mazoezi ya mwisho kujiandaa dhidi ya Tanzania Prisons, akili zetu zinawaza kufanya vizuri tu. Tunajua nini tunataka, kesho tunacheza na timu ngumu ambayo imetoka kupoteza na Simba kisha wakapata Sare dhidi ya Azam. Tuna uhakika kwamba mchezo utakuwa mgumu, lakini tupo hapa kwaajili ya alama tatu na tuna imani tutazipata.
“Licha ya changamoto mbalimbali za majeruhi, mfano Job, Mzize na wengine, timu nzima ina lengo la kupata matokeo mazuri. Hivyo kila mtu anafanya jitihada kubwa kutimiza malengo ya klabu. Tunawashukuru sana Wananchi kwa kuwa nasi katika kila hali, ratiba yetu ni ngumu. Kila baada ya siku mbili tuna mechi ya kucheza lakini mashabiki wetu hawajawahi kuwa nyuma, wanakuja kutupa sapoti.
“Licha ya majeruhi tulionao, tuna wachezaji wengi wenye uwezo mkubwa sana lakini wanaopaswa kuanza ni 11 pekee. Nafurahi kuwa wachezaji wote wana uelewa mkubwa kuhusu mawazo yetu na mbinu tunazowapa. Naamini kila mmoja yupo tayari kwa ajili ya kuisaidia timu, naamini kesho itakuwa siku ngumu lakini nzuri kwasababu tumekuja kusaka ushindi”
Masalanga atuma ujumbe wa wachezaji

Naye kip awa Yanga SC, Hussein Masalanga kwa niaba ya wachezaji amesema: “Sisi kama wachezaji tumejiandaa vizuri na tunajua umuhimu wa mchezo huu. Tunajua tunakwenda kucheza na timu ngumu na yenye wachezaji wazuri. Tunawaheshimu wapinzani, lakini kilichotuleta hapa ni pointi tatu na tunaamini tutazipata. Sisi ni kama wanajeshi, hatuchagui eneo la vita, hatuchagui kiwanja cha kucheza. Uwanja wowote tutakapopangiwa ndiyo hapo tutakapocheza. Tupo tayari kucheza kesho kwa kujitoa ili tutimize malengo yetu.”
SOMA HII PIA: Wachezaji wa Simba SC watakao achwa msimu wa 2025/26 | Aishi Manula, Che Malone, Hussein Kazi
Ishu ya Uwanja kubadilishwa
Machi 10, 2026 yaani jana Jumanne, Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) ilitoa tangazo kwa Umma juu ya mabadiliko ya Uwanja ambao mchezo huu ulipangwa kupigwa. Hapo awali mchezo huu ulipangwa kupigwa kwenye Uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya, lakini ratiba imebadilika. Mchezo huu sasa unatarajiwa kupigwa Uwanja wa Jamhuri Dodoma. Sakata hili limelalamikiwa na baadhi ya wadau na wachambuzi wa michezo, huku ikielezwa Tanzania Prisons walitaka kucheza Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi Tabora.
Hitimisho na utabiri
Tanzania Prisons vs Yanga SC kwa kuangalia rekodi za michezo iliyopita, ni rahisi kusema Wananchi wana nafasi kubwa ya ushindi. Lakini hii ni nafasi kwa Prisons kuonyesha utofauti na kuandika rekodi mpya. Uchovu wa ratiba kutokana na msongamano wa michezo huenda ukaiathiri Yanga lakini bado matarajio ya wengi ni ushindi kwa Yanga SC.

