Depu Mtambo wa mabaoDepu Mtambo wa mabao
  • Straika mpya wa Yanga SC, Laurindo Depu ameendelea kuitikisa Bongo.
  • Takwimu na namba zake tangu atue ndani ya kikosi hiko zinaogopesha, na hautakosea ikiwa utamuita Depu mtambo wa mabao.
  • Nyota huyo ameendeleza rekodi ya kuweka kambani kwa kuiongoza Yanga SC kuichapa Namungo FC bao 1-0.
  • Makala hii inakuletea dondoo muhimu kumhusu Laurindo Depu ‘Mtambo wa mabao’.

Nyota mpya wa Yanga SC, Laurindo Depu ameendelea kuitikisa Bongo. Takwimu na namba za straika huyo tangu atue ndani ya kikosi cha Wananchi zinaogopesha, na tayari mashabiki wamempachika jina la ‘Depu mtambo wa mabao’. Nyota huyo ameendeleza rekodi ya kucheka na nyavu baada ya Jumapili hii kuiongoza Yanga SC kuichapa Namungo FC bao 1-0.

SOMA HII PIA: Deal done Allan Okelo asaini miaka miwili Yanga SC/ Orodha ya wanaofuata

Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa

Hujashinda na SportPesa? Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

image

Laurindo Depu mtambo wa mabao ni nani?

Depu Ulaya
Depu Ulaya

Alizaliwa kwenye ardhi ya Angola miaka 25 iliyopita, akakulia kwenye mazingira ya soka la mitaani lililojaa ndoto na ushindani. Tangu akiwa mdogo, Laurindo Dilson Maria Aurélio maarufu kama ‘Depu’ alionyesha dalili za kuwa tofauti. Alikuwa na nguvu, kasi na jicho kali la lango, hali iliyomfanya mapema kuwekeza kwenye nafasi ya ushambuliaji.

Amefanikiwa kupitia safari ndefu ya soka la kulipwa barani Ulaya, akicheza Ureno, Serbia na Poland. Hii imemfanya kujifunza soka la ushindani mkubwa, nidhamu na uimara wa kimwili. Hii ilizidi kumboresha licha ya kwamba hakupata nafasi kubwa mara zote, na hili halikumkatisha tamaa, aliendelea kupambana akijenga jina lake taratibu.

SOMA HII ZAIDI: Yanga SC vs Simba SC joto linazidi kupanda/ Ratiba, msimamo

Mafanikio yake makubwa binafsi

Depu na ubingwa wa COSAFA
Depu na ubingwa wa COSAFA

Msimu wa 2024/25 – Mshindi wa COSAFA Cup

2024/25 – Mfungaji Bora COSAFA Cup

2025 – Mchezaji Bora COSAFA Cup

Haya yote Depu aliyafanya akiwa na kikosi cha timu ya Taifa ya Angola na hapo jina lake likaanza kutetemesha ulinzi wa timu nyingi Afrika.

Kutua kwake Yanga SC

Kutokana na rekodi nzuri za misimu yake miwili iliyopita, hapo ndipo Yanga SC wakaamua kuchukua hatua ya kumsajili. Yanga SC walikamilisha usajili wa Depú kwa Mkataba wa miaka miwili na nusu, huku dau la usajili likitajwa ni zaidi ya Shilingi Milioni 600 za Kitanzania. Depu ni mshambuliaji aliyekuja na wasifu wa ushindi, mabao na ubingwa. Waangola wengi walitamani kumuona Depú akiendelea Ulaya, lakini Yanga wakawa na lengo lao.

SOMA HII PIA: Usajili wa Simba SC dirisha dogo balaa! Gueye, Kibabage, Loemba

Takwimu zake tangu ametua bongo

Takwimu za Depu mtambo wa mabao
Takwimu za Depu

 Mpaka sasa kwenye Ligi Kuu Bara Depu amecheza mechi 3, ambapo amefanikiwa kufunga mabao 4 na kuasisti bao moja. Hii inamfanya kuwa amehusika katika mabao 5 katika mechi 3 tu. Kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika Nyota huyo amecheza mechi 4 na kufanikiwa kufunga mabao 2. Kwa ujumla mpaka sasa Depu amehusika katika mabao 7 katika michezo saba. Ikumbukwe hapa rekodi za Kombe la Shirikisho la CRDB na Kombe la Mapinduzi hazijawekwa kwenye rekodi.

Ataweza kuziba pengo la Mayele?

Mayele Yanga SC
Mayele Yanga SC

Kasi aliyoanza nayo Depu imeanza kuwapa jeuri baadhi ya mashabiki wa timu hiyo ambao wanaamini nyota huyo huenda akaziba pengo la aliyekuwa straika wao, Fiston Mayele. Tangu kuondoka kwa Mayele Yanga SC bado timu hiyo haijapata mrithi sahihi, ambaye angalau anakaribia uwezo wa mkongomani huyo aliyetimkia Pyramid FC ya Misri. Swali linabaki kuwa ni kweli Depu ataweza kufikia rekodi na ubora wa Mayele Yanga SC?

Hitimisho

Depu mtambo wa mabao bila shaka ni balaa jipya bongo. Kwa mwendo alioanza nao kama ataendelea na kasi hiyo, basi haitashangaza kuona akiwa sehemu ya nyota watakaokuwa wanapigania kubeba kiatu cha ufungaji bora msimu huu. Swali kubwa ni je, ataweza kuziba pengo la Mayele?  

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.