Dabi ya Kariakoo Yanga SC vs Simba SCBoyel vs KMC
  • NBC Premier League 2025/26 ratiba ya dabi imetangazwa upya kwa wanaume 22 kushuka uwanjani.
  • Dabi ya Kariakoo Yanga SC vs Simba SC ni Machi Mosi 2026, Uwanja wa Mkapa awali ilipangwa Desemba 13,2025.
  • Yanga SC 1-0 Simba SC matokeo ya mchezo Ngao ya Jamii 2025 walipokutana wababe hawa wawili.

Dabi ya Kariakoo Yanga SC vs Simba SC ni Machi Mosi 2026, Uwanja wa Mkapa. Ratiba awali ilipangwa kuchezwa Desemba 13, 2025.Mabadiliko hayo yanatokana na maboresho ya ratiba yaliyofanywa na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara, (TPLB).

Shinda sasa na ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa hivi

Zamu yako kushinda na SportPesa, unaweza kushinda mamilioni sasa hivi. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kupitia Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa bonyeza picha hii chini.

SOMA HII: Yanga SC vs Simba SC wachezaji hawa ni Kariakoo Dabi yao ya kwanza | H2H, matokeo, rekodi

image

Dabi ya Kariakoo Yanga SC vs Simba 2025/26 ratiba mpya

Dabi ya Kariakoo Yanga SC vs Simba SC
Pacome mchezaji aliyeifunga Simba SC kwenye mchezo wa Kariakoo Dabi, Ngao ya Jamii. Source: Simba SC.

Watani hawa wa jadi kwenye hii Dabi ya Kariakoo Yanga SC vs Simba SC 2025/26 wapo kwenye ratiba mpya. Hii ni kutokana na maboresho yaliyofanyika na TPLB, watakutana baada ya miezi miwili kupita. Mchezo wa mzunguko wa kwanza utapigwa Machi na ule mzunguko wa pili itakuwa Mei.

Ratiba ipo namna hii:-

Yanga SC vs Simba SC, Machi Mosi 2026, Uwanja wa Mkapa.

Simba SC vs Yanga SC, Mei 3,2025, Uwanja wa Mkapa.

Matokeo ya mechi 11 za Dabi ya Kariakoo

16/09/2025 Yanga SC 1-0 Simba SC, Ngao ya Jamii.
26/06/2025 Yanga SC 2-0 Simba SC, NBC Premier League.
19/10/2024 Simba SC 0-1 Yanga SC, NBC Premier League.
08/08/2024 Yanga SC 1-0 Simba SC, Ngao ya Jamii.
20/04/2024 Yanga SC 2-1 Simba SC, NBC Premier League.
05/11/2023 Simba SC 1-5 Yanga SC, NBC Premier League.
16/04/2023 Simba SC 2-0 Yanga SC, NBC Premier League.
23/10/2022 Yanga SC 1-1 Simba SC, NBC Premier League.
39/04/2022 Yanga SC 0-0 Simba SC, NBC Premier League.
11/12/2021 Simba SC 0-0 Yanga SC, NBC Premier League.
03/07/2021 Simba SC 0-1 Yanga SC, NBC Premier League.

SOMA HII: Yanga SC 1-0 Simba SC: Highlights, magoli yote, h2h – Ngao ya jamii 2025

image

Ijue ratiba ya dabi nyingine 2025/26 NBC Premier League

Dar Dabi

Azam FC vs Yanga SC, tarehe itatajwa, Uwanja wa Azam FC

Yanga SC vs Azam FC, Mei 19,2025, Uwanja wa KMC Complex

Mzizizima Dabi

Fei Toto
Fei Toto kiungo wa Azam FC 2025/26. Source: Azam FC.

Simba SC vs Azam FC, Desemba 6,2025, Uwanja wa Mkapa

Azam FC vs Simba SC, itapangiwa tarehe, Uwanja wa Azam Complex

Mbeya Dabi

Mbeya City 1-2 Tanzania Prisons, Oktoba 21,2025. Uwanja wa KMC Complex.

Tanzania Prisons vs Mbeya City, Machi 18,2026, Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

SOMA HII: Uchambuzi wa Yanga SC vs Simba SC itakayochezwa Septemba 16 | H2H, vikosi, matokeo, wafungaji

Burudani kusimama kwa siku 46

Mukwala vs JKT Tanzania
JKT Tanzania vs Simba SC kwenye mchezo wa ligi msimu wa 2025/26. Source: Simba SC.

Ligi Kuu Tanzania Bara itasimama kwa muda wa siku 46. Hii ni kutokana na fainali za Mataifa ya Afrika, (AFCON) zitakazofanyika Morocco kuanzia Desemba 21,2025 mpaka Januari 18,2026. Mechi za mwisho zinatarajiwa kuchezwa kuanzia Desemba 3 mpaka Desemba 7,2025.

Kutokana na maboresho ya ratiba ya ligi yaliyofanywa na TPLB ni Mei 29,2025 ligi itafika tamati kwa mechi za raundi 30 na tuzo za 2024/25 zinatarajiwa kutolewa Desemba 5,2025. Bingwa mtetezi ni Yanga SC aliyetwaa taji hilo 2024/25.

Hitimisho

Dabi ya Kariakoo Yanga SC vs Simba SC mara ya mwisho kwenye ligi mnyama alipoteza. Kwenye mechi za hivi karibu watoto wa Jangwani wamejenga utawala wa ushindi. Je mnyama atakubali unyonge Machi Mosi 2026? Itafahamika watakapokutana baada ya dakika 90.

Share this: