Cameroon vs MoroccoCameroon vs Morocco
  • Hayawi hayawi, sasa yamekua! Ni Ijumaa hii huko nchini Morocco.
  • Hatua ya Robo Fainali ya mashindano ya Kombe la Mataifa Afrika AFCON 2025 itaanza kupigwa rasmi.
  • Mchezo kati ya Cameroon vs Morocco ndio unatarajiwa kutolewa macho sana kesho Ijumaa.
  • Makala hii inaangazia baadhi ya dondoo muhimu za mchezo huo uliobeba tiketi ya nusu fainali.

Hatumwi mtoto dukani! Moto utawaka kesho Ijumaa nchini Morocco kwenye mashindano ya Kombe la Mataifa Afrika AFCON 2025. Ni Cameroon vs Morocco mechi inayotarajiwa kuwa na ushindani na presha hasa kwa wenyeji Morocco. Makala hii inaangazia baadhi ya dondoo muhimu za mchezo huo.

SOMA HII PIA: AFCON 2025: Matokeo na Ratiba ya Robo Fainali, hizi hapa timu zilizofuzu

Je, bado hujashinda pesa? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa

Changamka! sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

image

H2H, Cameroon vs Morocco

Cameroon vs Morocco (-)
Cameroon vs Morocco

Katika historia ya soka la ushindani Cameroon na Morocco zimekutana katika michezo 7. Cameroon imeshinda michezo 2 dhidi ya Morocco, huku Morocco pia wakishinda mechi 2. Mechi 3 zilizosalia ziliisha kwa matokeo ya sare.

Fomu ya Cameroon kwenye AFCON 2025

WDWW

Fomu ya Morocco kwenye AFCON 2025

WDWW

Vikosi tarajiwa Cameroon vs Morocco AFCON 2025

Cameroon

Kipa: Epassy

Walinzi: Kotto, Tolo, Malone

Viungo: Nagida, Namaso, Baleba, Ebong, Tchamadeu

Washambuliaji: Mbeumo, Kofane

Morocco

AFCON 2025
Celebrate

Kipa: Bono

Walinzi: A. Hakimi, N. Aguerd, A. Masina, N. Mazraoui

Viungo: N. El Aynaoui, El Khannouss, B. Díaz, I. Saibari, A. Ezzalzouli

Mshambuliaji: A. Kaabi

SOMA HII ZAIDI: AFCON 2025: Matokeo, hawa hapa wafungaji bora kabla ya Ratiba ya 16 bora, Feisal na Msuva wamo?

Habari za timu

Wenyeji wa michuano hiyo Morocco wanakabiliwa na mtihani mgumu mno, katika harakati zao za kushinda Kombe la AFCON. Morocco walio kwenye ardhi ya nyumbani watamenyana na Cameroon katika robo fainali. Morocco wamefika hatua hii baada ya kuwafurusha Tanzania.

Cameroon haijafuzu Kombe la Dunia la 2026 baada ya kushindwa kufuzu, lakini ushindi wao wa 2-1 dhidi ya Afrika Kusini umeipeleka Robo Fainali ya AFCON. Morocco haijawahi kuifunga Cameroon katika AFCON, na ilipoteza mbele yao katika nusu fainali mwaka 1988.

Walichosema makocha

Regragui
Regragui

Akizungumzia hilo kocha, Walid Regragui amesema: “Cameroon ilituondoa katika nusu fainali ya 1988, lakini yaliyopita ni ya nyuma. Leo sisi ni Morocco mpya. Pia tukifungwa kuna kitu cha kupoteza, kwa kuwa tunaandaa hafla hiyo nyumbani na ndani ya miezi minne tutacheza Kombe la Dunia.”

Naye kocha wa Cameroon, David Pagou alisema: “Historia ya yaliyopita haielezei kinachoweza kuja, hasa katika mpira wa miguu. Unaweza kufanikiwa sana jana na ukaanguka leo. Morocco imefuzu nusu fainali ya Kombe la Dunia, hivyo itakuwa mechi ngumu sana dhidi ya timu nzuri sana, tutajaribu kuwapa changamoto.

“Kinachowatambulisha Wacameroon ni ujasiri wao. Hata wakati tunapokutana na milima. Ni nguvu ya akili ambayo hufanya tofauti, tunajivunia kuwa hapa. Tuna umakini. Morocco ni bora ni timu ya kutisha. Changamoto haitakuwa rahisi, lakini tuko tayari kuikabili.”

SOMA HII PIA: AFCON 2025 hatua ya 16 bora ratiba/ Morocco vs Tanzania kuwashangaza wengi, msimamo

Hitimisho

AFCON 2025
Cameroon

Cameroon vs Morocco unatarajiwa kuwa mchezo wa kuvutia. Mchezo huu unatarajiwa kuwa na mnatokeo ya kushangaza kwa kila upande, lakini Morocco wanapewa nafasi kubwa. Nani ataenda Nusu Fainali ni Morocco au Cameroon.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.