Simba SC kuwakosa wachezaji muhimu watatu wakiikabili Petro de Luanda CAF Champions LeagueCamara -
  • CAF Champions League Jumapili Novemba 23,2025 saa 10:00 jioni, Uwanja wa Benjamini Mkapa.
  • Simba SC kuwakosa wachezaji muhimu watatu wakiikabili Petro de Luanda CAF Champions League.
  • Mchezo wa kwanza kati ya sita hatua ya makundi timu hizi zikiwa ni kundi D.

Simba SC kuwakosa wachezaji muhimu watatu wakiikabili Petro de Luanda CAF Champions League Novemba 23,2025. Sababu kubwa za Nyota hao kukosekana kwenye mchezo huo wa makundi ni kusumbuliwa na majeraha. Licha ya mnyama kukosa huduma za wachezaji hao bado yupo imara kwa ushindani.

SOMA HII: Simba SC vs Petro de Luanda CAF Champions League 2025/26/ Live score, H2H

Shinda sasa na ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa hivi

Zamu yako kushinda na SportPesa, unaweza kushinda mamilioni sasa hivi. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kupitia Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa bonyeza picha hii chini.

image

Simba SC kuwakosa wachezaji muhimu watatu wakiikabili Petro de Luanda CAF Champions League majina haya hapa

Simba SC kuwakosa wachezaji muhimu watatu wakiikabili Petro de Luanda CAF Champions League
Bajaber kiungo mshambuliaji wa Simba SC akiwa na wachezaji wengine. Source: Simba SC.

Kwenye mchezo wa kwanza Simba SC kuwakosa wachezaji muhimu watatu wakiikabili Petro de Luanda CAF Champions Uwanja wa Benjamini Mkapa. Wachezaji hao wamekuwa nje kwa muda wakipewa matibabu ili warejee katika ubora. Kuelekea mchezo wa Jumapili Meneja Mkuu wa Simba SC, Dimitar Pantev atakuwa na mpango kazi mwingine katika nafasi zao.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC aliwataja wachezaji watakaokosekana. Moussa Camara na Abdulrazack Hamza. “Mchezo wa Jumapili tutamkosa Moussa Camara yupo nchini Morocco alipokwenda kufanyiwa matibabu. Tutamkosa beki Abdulrazack Hamza. Taarifa njema ni kuwa Mohamed Bajaber amepona na hata mchezo wa kirafiki dhidi ya JKT Tanzania alianza kucheza dakika 30,”.

Licha ya Bajaber ambaye ni kiungo raia wa Kenya kurejea uwanjani taarifa zinaeleza hatakuwa sehemu ya kikosi. Sababu kubwa ya kiungo huyo kuondolewa ni kutokuwa fiti kwa asilimia 100. Hajacheza mchezo wa ushindani kwa muda mrefu hivyo anatajwa kutokuwa kwenye mpango wa benchi la ufundi kwa mchezo ujao.

SOMA HII: Simba SC vs Petro de Luanda CAF Champions League ni Novemba 23,2025/ Taarifa kuhusu Camara na Hamza

image

Mechi ambazo Bajaber alikosekana 2025/26 hizi hapa:-

Bajaber Kambini
Bajaber kiungo wa Simba SC 2025/26. Source: Simba SC.

Novemba 8,2025, JKT Tanzania 1-2 Simba SC, NBC Premier League.

Oktoba 26,2025, Simba SC 0-0 Nsingizini Hotspurs, CAF Champions League.

Oktoba 19,2025, Nsingizini Hotspurs 0-3 Simba SC, CAF Champions League

Oktoba Mosi 2025, Simba SC 3-0 Namungo FC, mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Septemba 28 2025, Simba SC 1-1 Gaborone United, Ligi ya Mabingwa Afrika.

Septemba 25 2025, Simba SC 3-0 Fountain Gate mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Septemba 20 2025, Gaborone United 0-1 Simba SC, Ligi ya Mabingwa Afrika.

SOMA HII: Simba SC vs Petro de Luanda nani atachukua pointi tatu CAF Champions League? Stats, prediction

image

Taarifa muhimu kuhusu Petro de Luanda

Petro de Luanda ni timu yenye rekodi nzuri kwenye eneo la ushambuliaji. Katika mechi zake 7 zilizopita safu ya ushambuliaji ilifunga magoli 12. Ukuta wa timu hiyo uliruhusu kufungwa magoli 4. Hivyo wapinzani hawa sio wepesi hata kidogo.

Ushindi umekuwa sehemu ya matokeo yao wayapaendayo. Katika mechi 7 za hivi karibuni walipoteza mechi mbili. Ushindi ilikuwa ni kwenye mechi 5.

Matokeo ya mechi 7 Petro de Luanda

Petro
Petro de Luanda 2025/26. Source: Petro de Luanda.

05/10/2025, Wiliete SC 0-2 Petro de Luanda mchezo wa ligi ya Angola.

18/10/2025, Stade d’Abdjan 0-2 Petro de Luanda, CAF Champions League.

25/10/2025, Petro de Luanda 2-0 Stade d’Abdjan Caf Champions League.
29/10/2025 Sao Salvador 2-1 Petro de Luanda, mchezo wa ligi ya Angola.
01/11/2025, Petro de Luanda 4-1 Libolo, mchezo wa ligi ya Angola.
05/11/2025, Petro de Luanda 1-0 Interclube, mchezo wa ligi ya Angola.
09/11/2025, Petro de Luanda 0- 1 de Agosto, mchezo wa ligi ya Angola.

Msimamo wa kundi D

1. Petro de Luanda
2.Esperance
3. Simba SC
4. Stade Malien

Hitimisho

Simba SC kuwakosa wachezaji muhimu watatu wakiikabili Petro de Luanda CAF Champions League. Camara tayari amefanyiwa upasuaji atakuwa nje ya uwanja kwa wiki 8-9. Ni Yakoub Suleman kipa namba mbili wa timu hiyo amebeba mikoba yake.

Share this: