- Petro de Luanda wapinzani wa Simba SC wanatarajiwa kuwasili Tanzania Novemba 18,2025.
- Simba SC vs Petro de Luanda CAF Champions League ni Novemba 23,2025 , Uwanja wa Mkapa saa 10:00 jioni.
- Moussa Camara taarifa mpya imetolewa na Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC.
Simba SC vs Petro de Luanda CAF Champions League ni Novemba 23,2025 badala ya Novemba 22. Awali ulitarajiwa kuchezwa saa 1:00 usiku rasmi mchezo huo utachezwa saa 10:00 jioni. Ni mchezo wa kwanza hatua ya makundi ambapo timu hizi mbili zipo kundi D zitakuwa kwenye msako wa tiketi ya kutinga robo fainali.
SOMA HII: Simba SC vs Petro de Luanda CAF Champions League 2025/26/ Live score, H2H
Shinda na ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa hivi
Zamu yako kushinda na SportPesa, unaweza kushinda mamilioni sasa hivi. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kupitia Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa bonyeza picha hii chini.

Simba SC vs Petro de Luanda CAF Champions League ni Novemba 23,2025

Rasmi wababe wawili Simba SC vs Petro de Luanda CAF Champions League ni Novemba 23,2025 siku ya Jumapili. Mnyama atakuwa kwenye kazi ya kusaka ushindi wa kwanza msimu wa 2025/26 nyumbani. Rekodi zinaonyesha kuwa katika mechi mbili za kimataifa timu hiyo ilikwama kupata ushindi.
Wachezaji muhimu watakaokosekana Simba SC

Kuelekea kwenye mchezo huo wenyeji Simba SC watakosa huduma za wachezaji wake muhimu. Ni mlinda mlango namba moja na beki wa kati. Hawa wote wapo nje kutokana na kutokuwa fiti baada ya kuumia. Mousa Camara alipata maumivu kwenye mchezo dhidi ya Gaborone United na Hamza alipata maumivu kwenye Kariakoo Dabi.
Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC amethibitisha kuhusu suala hilo. Aliongeza kwa kuwaomba mashabiki kuwaombea wachezaji warejee katika ubora.
“Mchezo wa Jumapili tutamkosa Moussa Camara yupo Morocco alipokwenda kufanyiwa matibabu. Lakini tutamkosa beki Abdulrazack Hamza ambaye na yeye anasafiri kwenda Morocco kwa matibabu zaidi. Taarifa njema ni kuwa Mohamed Bajaber amepona na hata mchezo wa kirafiki dhidi ya JKT Tanzania alianza na kucheza dakika 30.
SOMA HII: Simba SC vs Petro de Luanda nani atachukua pointi tatu CAF Champions League? Stats, prediction

Hii hapa ratiba ya Petro de Luanda kutua Bongo
Ahmed Ally alitaja ratiba ya wapinzani wao kutoka Angola kuwasili Tanzania. “Wapinzani wetu Petro Atletico watawasili nchini Novemba 19, 2025 na watakuwepo hapa hadi siku ya mchezo. Waamuzi wa mchezo huo wanatoka Congo Brazzaville.
“Viingilio vya mchezo ni Tanzanite – Tsh. 250,000, Platinum – Tsh. 150,000, VIP A – Tsh. 30,000, VIP B – Tsh. 20,000, VIP C – Tsh. 10,000 na Mzunguko – Tsh. 5,000,” alisema Ahmed Ally.
Mbadala wa Moussa Camara huyu hapa

Kutokana na Camara kutokuwa langoni mikoba yake ipo mikononi mwa Yakoub Suleman. Kipa huyo ni kipa namba mbili wat imu hiyo. Kwenye mchezo uliopita dhidi ya JKT Tanzania alianza kikosi cha kwanza.
Alianza kikosi cha kwanza kwenye mechi dhidi ya Nsingizini Hotspurs nje ndani na hakufungwa. Hivyo ameanza kupata uzoefu katika mechi za kimataifa. Kipa mwingine ni Hussen Abel ambaye ni kipa namba tatu wa mnyama.
Matokeo ya mechi 3 za Yakoub akiwa langoni
Novemba 8,2025, JKT Tanzania 1-2 Simba SC, NBC Premier League.
Oktoba 26,2025, Simba SC 0-0 Nsingizini Hotspurs, CAF Champions League.
Oktoba 19,2025, Nsingizini Hotspurs 0-3 Simba SC, CAF Champions League
SOMA HII: Mechi za Simba SC 2025/26 CAF Champions League, NBC Premier League ni moto| Matokeo na wafungaji
Hitimisho
Simba SC vs Petro de Luanda CAF Champions League ni Novemba 23,2025 Uwanja wa Mkapa.Ni mchezo wa kwanza hatua ya makundi kwa wababe hawa wawili. Mnyama atakuwa nyumbani kusaka pointi tatu ambazo vijana wa Angola wanazihitaji.

