- Usiku wa kuamkia leo Novemba 20, 2025 hautasahaulika kwa straika wa kimataifa wa Tanzania, Clement Mzize.
- Hii ni baada ya nyota kutajwa mshindi wa tuzo ya CAF ya goli bora Afrika mwaka 2025.
- Haya ni mafanikio makubwa kwa Mzize hasa baada ya kuwa na msimu wa mafanikio makubwa. Ikumbukwe 2024/25 alihusika katika mabao 19 ya Yanga SC, alifunga mabao 14 na kutoa pasi 5 za mabao.
Usiku wa kuamkia leo Alhamisi hautasahaulika kwa straika wa kimataifa wa Tanzania na klabu ya Yanga SC, Clement Mzize. Hii ni baada ya Nyota huyo kushinda tuzo ya CAF ya goli bora Afrika mwaka 2025. Tuzo hiyo ilitolewa katika usiku wa tuzo ambao umefanyika nchini Morocco.
SOMA HII PIA: Clement Mzize anafuata kuondoka Yanga SC baada ya Aziz Ki, sababu zatajwa
Ushindi mzito wa ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni muda huu
Sasa ni zamu yako kushinda na SportPesa, unaweza kushinda mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kupitia Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa bonyeza picha hii chini.

Usiyoyajua kuhusu Clement Mzize na tuzo ya CAF ya goli bora la mwaka 2025

Ikumbukwe kuwa, Mzize alifunga goli hilo Uwanja wa Mkapa kwenye mchezo wa hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika, dhidi ya TP Mazembe Januari 4, mwaka huu. Katika mchezo huo Yanga SC iliibuka na ushindi wa mabao 3-1. Kutokana na matokeo hayo Yanga SC ilifufua matumaini ya kutinga Robo Fainali ya mashindano hayo.
Mzize akwama kwenda Morocco
Kama ambavyo ilitarajiwa na wengi, Mzize alishindwa kuhudhuria usiku wa tuzo hizo. Sababu kubwa ya mshambuliaji huyo kushindwa kwenda kwenye usiku wa tuzo ni ushauri wa jopo la madaktari ambao, walishauri asitembee umbali mrefu kutokana na upasuaji ambao amefanyiwa. Kutokana na changamoto hiyo, Mzize aliwakilishwa na Rais wa Yanga SC, Injinia Hersi Said.
Mayele azidi kuiteka Afrika

Mbali na Mzize kuwapa jeuri Tanzania katika tuzo hizo, wadau mbalimbali wa soka Tanzania wamejivunia mchezaji, Fiston Mayele. Straika huyo wa zamani wa Yanga SC naye alifanikiwa kutwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka, wa Mashindano ya Vilabu Barani Afrika (Men’s Interclub Player of the Year).
SOMA HII ZAIDI: Clement Mzize Waarabu waikomalia saini yake | Mkataba wake upo hivi | Takwimu, magoli
Kuhusu majeraha ya Mzize

Hivi karibuni uongozi wa Klabu ya Yanga SC ulitangaza kuwa Mzize anatarajiwa kuwa nje ya uwanja, kwa muda wa miezi miwili hadi na nusu. Hii ni baada ya kufanyiwa upasuaji mdogo wa goti. Upasuaji huo umekuja kutokana na majeraha ambayo Mzize aliyapata Septemba 19, 2025 katika mechi dhidi ya Wiliete ya Angola.
Takwimu za Clement Mzize
Msimu uliopita Mzize alihusika katika mabao 19 ya Yanga SC ambapo, alifunga mabao 14 na kutoa pasi 5 za mabao. Hii ilimfanya Mzize kuwa mchezaji mzawa aliyefunga mabao mengi akifuatiwa na Nassor Saadun wa Azam FC. Saadun yeye ameifungia Azam FC mabao nane, sawa na Paul Peter wa Dodoma Jiji.
Ukiachana na Klabu, Mzize pia alikuwa na wakati mzuri akiwa na kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania, msimu uliopita. Mzize alikuwa karata maalum ya kuibeba Stars katika safari ya kwanza ya kihistoria, ya kufuzu Robo Fainali ya mashindano ya CHAN 2024. Mabao yake mawili katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Madagascar yaliipeleka Stars Robo Fainali.
Katika mashindano hayo Tanzania walikuwa wenyeji na kuandika rekodi nzuri ya ushindi wa asilimia 100, katika michezo ya hatua ya makundi. Kiwango chake katika mashindano haya kilizivutia timu kubwa ndani na nje ya Tanzania.
Ofa zamiminika kusaka Saini ya Mzize
Kiwango bora ambacho staa huyo alikionyesha kwenye Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN 2024), kilifanya thamani ya mzize kuzidi kupaa. Baadhi ya timu kubwa kutoka ndani na nje ya Tanzania ziliingia vitani kusaka Saini yake.
Awali mchezaji huyo alihusishwa na klabu kutoka Ubelgiji, Misri, Afrika Kusini na Morocco kabla ya kuibuka taarifa ya ofa nyingine kutoka Qatar. Timu nyingine ambazo zimetajwa kusaka Saini ya Mzize ni pamoja na: Zamalek FC ya Misri, Esperance ya na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini.
Hitimisho

Ikiwa ni takribani mwaka mmoja na siku kadhaa zimepita tangu ‘saga’ za usajili wa Clement Mzize zishike kasi, na kushuhudia mshambuliaji huyo akisaini kandarasi ya miaka miwili hadi 2027. Mzize amechora mchoro mpya kwenye historia ya maisha yake, kwa tuzo hii ya kihistoria. Kila la kheri kwake straika wa mpira.

