- Pacome Zouzoua goli lake la pili limetosha kuivusha Yanga SC kwenye hatua ya makundi kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa.
- Yanga SC 2-0 Silver Strikers CAF Champions League Oktoba 25,2025 ushindi uliopindua meza ya matokeo ya awali ugenini.
- Ushindi wa jumla ya magoli 2-1 unaipeleka timu hiyo hatua ya makundi 2025/26.
Yanga SC 2-0 Silver Strikers CAF Champions League Oktoba 25,2025 ni ushindi uliowakikishia wananchi kutinga hatua ya makundi. Magoli yote ya Yanga SC yalifungwa kipindi cha kwanza kupitia Dickson Job dakika ya 6 na Pacome dakika ya 34. Kasi kwenye kipindi cha kwanza kwa watoto hao wa Jangwani, Uwanja wa Benjamini Mkapa ilitosha kupindua meza matokeo ya Oktoba 18 2025 mchezo uliochezwa Uwanja wa Bingu-Malawi walipofungwa goli 1-0.
SOMA HII: Yanga SC vs Silver Strikers CAF Champions League Oktoba 25 |Mbeba mikoba ya Folz kazini
Unasubiri nini? Vuna mamilioni sasa hivi
Kuna jambo umekwama kwa sasa kuhusu mkwanja? Usiogope, rubani ni jasiri na kazi yake ni kupaisha kindege cha SportPesa. Cheza sasa hivi Aviator uvune mamilioni bofya hapa chini.

Yanga SC 2-0 Silver Strikers CAF Champions League Oktoba 25 magoli yalifungwajwe?

Yanga SC 2-0 Silver Strikers CAF Champions League Oktoba 25 magoli yalifungwa kwa ushirikiano mkubwa wa wachezaji wa Yanga SC. Ukurasa ulifunguliwa na Dickon Job ambaye ni beki akimalizia kona iliyopigwa na Mo Doumbia. Kabla ya kona hiyo kiungo Duke Abuya alifanya jaribio nje kidogo ya 18 likaokolewa na kuleta kona.
Dakika ya 34 Pacome Zouzoua alipachika goli la pili. Kiungo Maxi Nzengeli alitoa pasi ya goli hilo.Silver Strikers walikuwa kwenye kasi ya kutafuta goli walikutana na kikwazo cha mlinda mlango Djigui Diarra.
Duke Abuya maoni yake baada ya kutinga hatua ya makundi

Duke Abuya kiungo wa Yanga SC amesema kuwa walikuwa wanahitaji ushindi kwa namna yoyote ile. Kuanza kikosi cha kwanza kulimpa nguvu kushirikiana na wengine katika kutafuta ushindi. Aliongeza kwa kusema uwepo wa mashabiki uliwaongezea hali ya kujiamini.
“Tulikuwa tunahitaji matokeo mazuri kwa namna yoyote ile. Kupoteza mchezo wetu wa kwanza kulitufanya tuongeze nguvu kwenye mchezo wa pili. Tunawashukuru mashabiki wamejitokeza kwa wingi na ushindi umepatikana. Bado kuna kazi ya kufanya mechi zijazo,”.
Kikosi cha Yanga SC kilichoanza dhidi ya Silver Strikers Uwanja wa Mkapa
Kipa
Djigui Diarra
Mabeki
Israel Mwenda
Zimbwe Jr
Dickson Job
Ibrahim Bacca
Viungo
Duke Abuya
Maxi Nzengeli
Mudathir Yahya
Pacome
Doumbia
Mshambuliaji
Dube
Wachezaji wa akiba
Aboutwalib Mshery, Bakari Nondo, Boka, Kibwana Shomari, Aziz Andambwile, Kouma, Chikola, Edmund John na Boyeli.
Mechi 8 za Yanga SC zilizopita

Septemba 12,2025 – Yanga 1-0 Bandari ya Kenya. (Mechi ya kirafiki).
Septemba 16, 2025 – Yanga SC 1-0 Simba SC, (Ngao ya Jamii).
Septemba 19, 2025 – Wiliete 0-3 Yanga SC, (Ligi ya Mabingwa Afrika)
Septemba 24,2025 – Yanga SC 3-0 Pamba Jiji, (Ligi ya NBC).
Oktoba 27,2025 -Yanga 2-0 Wiliete SC, (Ligi ya Mabingwa Afrika).
Septemba 30,2025, Mbeya City 0-0 Yanga SC, (Ligi ya NBC).
Oktoba 18,2025, Silvers Strikers 1-0 Yanga SC, (Ligi ya Mabingwa Afrika)
Oktoba 25,2025, Yanga SC 2-0 Silver Strikers, (Ligi ya Mabingwa Afrika)

Mechi 8 za Silver Strikers zilizopita
Silver Strikers 1-0 Chitipa United, mchezo wa League Agosti 27 2025.
Shire FC 1-4 Silver Strikers, Septemba 11 2025 Malawi Cup
Elgeco Plus 1-1 Silver Strikers, Septemba 21 2025, Ligi ya Mabingwa Afrika.
Silver Strikers 0-0 Elgeco Plus Septemba 27 2025, Ligi ya Mabingwa Afrika.
Blue Eagles 0-3 Silver Strikers Oktoba 2 2025, Malawi Cup.
Bullets 2-1 Silver Strikers Oktoba 5 2025, Malawi Cup.
Oktoba 18,2025, Silvers Strikers 1-0 Yanga SC, (Ligi ya Mabingwa Afrika)
Oktoba 25,2025, Yanga SC 2-0 Silver Strikers, (Ligi ya Mabingwa Afrika)
SOMA HII: Yanga SC vs Silver Strikers CAF Champions League H2H takwimu muhimu utabiri

H2H
Silver Strikers FC 1-0 Yanga SC CAF Champions League, Oktoba 18, 2025 Uwanja wa Bingu, Malawi.
Yanga SC 2-0 Silver Strikers FC, Uwanja wa Benjamin Mkapa, Oktoba 25, 2025.
Hitimisho
Yanga SC 2-0 Silver Strikers CAF Champions League Oktoba 25 ulikuwa mchezo wa maamuzi. Kila mbabe alishinda nyumbani kimataifa. Ushindi kwa wananchi imekuwa ni faida kubwa wakikata tiketi ya kutinga hatua ya makundi Afrika. Silver Striker ya Malawi kwenye anga la kimataifa ni mpaka wakati mwingine tena.

