Yanga SC vs Silver Strikers
  • Uongozi wa Wananchi umetangaza rasmi mchezo wao wa kimataifa katika Uwanja wa Mkapa utakuwa bure hakuna kiingilio.
  • Yanga SC vs Silver Strikers CAF Champions League mchezo wa kusaka mshindi atakeyekata tiketi ya kutinga hatua ya makundi.
  • Patrick Mabedi kocha msaidizi amekabidhiwa jahazi lililokuwa linaongozwa na Romain Folz.
  • Mchezo unaodhamiriwa kuchezwa Jumamosi, baada ya Yanga kuzwabwa bao moja bila- mkondo wa kwanza na Silver Strikers.

 Yanga SC vs Silver Strikers CAF Champions League ni bure. Hii ni kuelekea mchezo wa marudiano utakaochezwa Oktoba 25, 2025 Uwanja wa Benjamini Mkapa. Sababu kubwa ya kuondoa viingilio na kufanya iwe ni bure kuruhusu mashabiki kujitokeza kwa wingi. Wananchi wanahitaji kuona uwanja unajaa mapema.

SOMA HII: Yanga SC vs Silver Strikers CAF Champions League 2025 ni leo October 18, 2025,lineup, H2H

Unasubiri nini? Vuna mamilioni sasa hivi

Kuna jambo umekwama kwa sasa kuhusu mkwanja? Usiogope, rubani ni jasiri na kazi yake ni kupaisha kindege cha SportPesa. Cheza sasa hivi Aviator uvune mamilioni bofya hapa chini.

image

Yanga SC vs Silver Strikers CAF Champions League ni bure

Yanga SC vs Silver Strikers CAF Champions ni bure
Dube Prince kwenye muonekano mpya. Source: Yanga SC.

Kwenye mchezo uliochezwa Oktoba 18,2025 Uwanja wa Bingu-Malawi wenyeji waliwapata matokeo mazuri. Yanga SC vs Silvers Strikers CAF Champions League ni bure Uwanja wa Mkapa. Wenyeji wana kibarua cha kupata ushindi wa angalau magoli 2-0 ili kusonga hatua ya makundi.

Mshindi wa jumla kwenye mchezo ujao utatoa maamuzi ya nani atasonga mbele. Matokeo ya Silver Strikers 1-0 Yanga SC ni faida kwa wageni kwa kuwa sare ya kufungana 1-1 itawavusha.Wananchi wanachotakiwa ni kupata ushindi.

Kutokana na umuhimu wa mchezo huo, wanachama wameomba waachiwe mechi. Utaratibu umetolewa rasmi na uongozi wa Yanga SC kwa kuondoa viingilio hivyo itakuwa ni bure.

Taarifa mpya kuhusu Clement Mzize

Mshambuliaji wa Yanga SC, Clement Mzize taarifa mpya ni njema. Baada ya kukosekana mchezo uliopita ugenini kwa sasa ametengamaa. Kuna uwezekano akawa miongoni mwa wachezaji watakaoikabili Silver Strikers Uwanja wa Mkapa.

Nyota huyo hakuwa kwenye mchezo wa ugenini nchini Malawi kwa kuwa hakuwa fiti. Tayari ameanza mazoezi na wachezaji wenzake. Kwenye mchezo huo Yanga SC ilipoteza kwa kufungwa goli 1-0.

SOMA HII: Yanga SC vs Silver Strikers CAF Champions League 2025| Lineup, H2H

image

H2H

Yanga SC vs Silver Strikers CAF
Pacome kiungo mshambuliaji wa Yanga SC kwenye mchezo dhidi ya Silvers Strikers. Source: Yanga SC.

Silver Strikers FC 1-0 Yanga SC CAF Champions League, Oktoba 18, 2025 Uwanja wa Bingu, Malawi.

Yanga SC vs Silver Strikers FC, Uwanja wa Benjamin Mkapa, Oktoba 25, 2025.

Yanga SC wameanza mazoezi

Tayari wachezaji wa Yanga SC wameanza mazoezi. Hiyo ni muda mfupi baada ya kurejea Dar wakitokea Eswatini. Kikosi hicho kipo chini ya kocha msaidizi Patrick Mabedi. Huyu amechukua mikoba ya Romain Folz ambaye alivunjiwa mkataba wake. Mchezo wa mwisho Folz kukaa kwenye benchi ilikuwa dhidi ya Silver Strikers ugenini.

Ali Kamwe kuhusu mchezo wa marudio maoni

Kamwe (-)
Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga SC.Source: Yanga SC.

Ofisa Habari wa Yanga SC amesema ombi la wanachama kupewa mechi limekubaliwa. Wanapaswa kuwa watulivu na kushangilia mwanzo mwisho. Kwa mashabiki ambao walikwenda Malawi watakuwa nae neo maalumu.

“Kupoteza mchezo wa kwanza kumeibua maneno mengi lakini tutajibu kwa vitendo. Mchezo wetu wa nyumbani ni nafasi kwetu kupata matokeo mazuri.Ombi la wanachama kuachiwa mechi limekubaliwa.

“Hakutakuwa na kiingilio kwenye mchezo wetu na utaratibu maalumu utafuatwa. Kwenye maeneo ya VIP huku wageni watakuwa na mialiko. Ila upande wa mzunguko huko mashabiki ni sehemu yao.

“Tunataka kuona mashabiki ambao wanakuja uwanjani wanapata burudani. Hivyo ni jukumu kushangalia mwanzo mwisho. Huu ni wakati wa vita kuipelekea timu katika hatua ya makundi,” alisema Kamwe.

SOMA HII: Yanga SC vs Silver Strikers CAF Champions League Oktoba 25 |Mbeba mikoba ya Folz kazini

Goal-Rush

Hitimisho

Yanga SC vs Silver Strikers CAF Champions League wenyeji wanapewa nafasi kupata matokeo. Mtihani huo utajibiwa baada ya dakika 90. Silver Strikers wanatarajiwa kuwasili alhamisi saa 2 usiku.

Shinda mamilioni na Supa Jackpot 17 kwa kubofya hapa

image

Share this: