- Nsingizini Hotspurs 0-3 Simba SC yalikuwa matokeo rasmi mchezo wa kwanza katika anga la kimataifa, Oktoba 19,2025.
- Simba SC vs Nsingizini Hotspurs CAF Champions League, Oktoba 26,2025 utaamua mshindi wa jumla atakayekata tiketi kutinga hatua ya makundi.
- Zitambue rekodi muhimu, wachezaji hatari kuelekea mchezo huo utakaopigwa Uwanja wa Mkapa.
Simba SC vs Nsingizini Hotspurs CAF Champions League utakuwa mchezo wa pili wababe hawa kukutana uwanjani. Kwenye mchezo wa ugeni mnyama aliunguruma kwa kuibuka na ushindi wa magoli 3-0. Mechi ya Jumapili Oktoba 26,2025 itaamua nani atakata tiketi kutinga hatua ya makundi Afrika.
SOMA HII: Nsingizini Hotspurs 0-3 Simba SC | CAF Champions League | Highlights | Magoli yote |
Shinda sasa na ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni muda huu
Zamu yako kushinda na SportPesa, unaweza kushinda mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kupitia Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa bonyeza picha hii chini.

Simba SC vs Nsingizini Hotspurs CAF Champions League utachezwa wapi?

Simba SC vs Nsingizini Hotspurs CAF Champions League mchezo wa marudiano utachezwa Tanzania, Uwanja wa Mkapa. Mchezo uliopita kwa Simba SC kimataifa ililazimisha sare ya kufungana goli 1-1 dhidi ya Gaborone United. Ikumbukwe kwamba huo mashabiki hawakuingia lakini Jumapili adhabu imekwisha watakuwepo uwanjani.
Jonathan Sowah mshambuliaji wa Simba SC maoni yake
Mshambuliaji Jonathan Sowah amesema kuwa wanaamini watapambana kufika hatua ya makundi. Nyota huyo aliongeza kuwa mashabiki wajitokeze kwa wingi Uwanja wa Mkapa.Ikumbukwe kwamba kwenye mchezo uliopita alitoa pasi moja ya goli lililofungwa na Kibu Dennis.
“Tuna mchezo mgumu ambao upo mbele yetu. Mashabiki wajitokeze kwa wingi ili kutushangalia. Imani yetu ni kuona kwamba tunakwenda hatua ya makundi licha ya kwamba haitakuwa rahisi,”.
Mechi 7 za Simba SC

Nsingizini Hotspurs 0- 3 Simba SC, Oktoba 19,2025. Ligi ya Mabingwa Afrika.
Oktoba Mosi 2025, Simba SC 3-0 Namungo FC, mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Septemba 28 2025, Simba SC 1-1 Gaborone United, Ligi ya Mabingwa Afrika.
Septemba 25 2025, Simba SC 3-0 Fountain Gate mchezo wa Ligi Kuu Bara.
Septemba 20 2025, Gaborone United 0-1 Simba SC, Ligi ya Mabingwa Afrika.
Septemba 16 2025, Yanga SC 1-0 Simba SC, Ngao ya Jamii.
Septemba 10 2025, Simba SC 2-0 Gor Mahia mchezo wa kimataifa wa kirafiki.
SOMA HII: Nsingizini Hotspurs vs Simba SC CAF Champions League| Mtihani wa kwanza wa Meneja Mkuu Pantev

Rekodi za Simba SC mechi za nyumbani
Simba SC katika mechi 4 ilizocheza ikiwa nyumbani, ushindi ni mechi 3. Ilipata sare mchezo mmoja wa kimataifa dhidi ya Gaborone United. Imekuwa bora inapocheza nyumbani kwa wachezaji kufunga.
Rekodi zinaonyesha kuwa ni magoli 9 ilifunga ilipokuwa nyumbani. Safu ya ulinzi iliruhusu goli moja. Hivyo wapinzani wana kazi kuvunja rekodi hiyo.
Rekodi za Nsinginzini Hotspurs ugenini
Wapinzani wa Simba SC katika mechi 4 walizocheza ugenini walipata ushindi mchezo mmoja. Ni mechi tatu walipoteza. Safu ya ushambuliaji ugenini ilifunga jumla ya magoli 6, sio timu yakubeza.
Wachezaji muhimu kwa Simba SC
Ellie Mpanzu huyu ni winga mwenye spidi uwanjani ana uwezo wa kufunga na kutoa pasi za magoli.
Morice Abraham kiungo mshambuliaji mwenye spidi akiwa uwanjani, uwezo wa kutoa pasi muhimu.
Kibu Dennis, kiungo mshambuliaji mwenye nguvu na spidi akiwa uwanjani.
Jean Ahoua, kiungo mshambuliaji mwenye akili linapofika suala la kupiga mapigo huru.
Wachezaji muhimu kwa Nsingizini Hotspurs
Mlinda mlango namba moja ni Shabala ambaye aliitwa timu ya taifa ya Eswatini. Nyota wengine ni Neliswa Dlamini, Thunehile Mavuso, Swizwe Khumalo na Nkosingiphile Shongwe.
Mechi 7 za Nsingizini Hotspurs

Nsingizini Hotspurs 0- 3 Simba SC, Oktoba 19,2025. Ligi ya Mabingwa Afrika.
Nsingizini Hotspurs 1-0 Simba Bhora, ilishinda kwa penalti 4-2, Septemba 28,2025 mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.
Simba Bhora 1-0 Nsingizini Hotspurs, Septemba 21 2025, Ligi ya Mabingwa Afrika.
Black Bulls 1-0 Nsingizini Hotspurs, Septemba 19,2025, mchezo wa kirafiki.
Sidvwashini United 0-5 Nsingizini Hotspurs, Mei 25 2025, mchezo wa MTN Premier League.
Nsingizini Hotspurs 2-1 Rangers Shiselweni, Mei 17 2025, MTN Premier League.
Mbabane Highland FC 2-1 Nsingizini Hotspurs, MTN Premier League, Mei 11 2025.
SOMA HII: Simba SC vs Nsingizini Hotspurs CAF Champions League | H2H, kikosi kilichosafiri, utabiri

H2H
Nsingizini Hotspurs 0-3 Simba SC, Oktoba 19 2025, CAF Champions League.
Simba SC vs Nsingizini Hotspurs, Oktoba 24,2025, CAF Champions League.
Hitimisho
Simba SC vs Nsingizini Hotspurs CAF Champions League ni mchezo ulioshikilia tiketi kwa timu zote kutinga hatua ya makundi. Mnyama ana rekodi ya kutinga zaidi ya mara tatu kwenye hatua ya makundi. Je Nsingizni Hotspurs kutoka Eswatini wataizuia Simba SC ikiwa nyumbani?
Shinda mamilioni kwa kucheza Supa Jackpot 17, bofya hapa chini


