- Yanga SC vs Silver Strikers CAF Champions League kituo kinachofuata Oktoba 18,2025 Uwanja wa Bingu.
- Clement Mzize amejumuishwa kwenye kikosi cha Yanga SC kilichoondoka kuelekea Malawi.
- Silver Strikers ilipata ushindi wa jumla dhidi ya Elgeco Plus inawakaribisha Yanga SC iliyopata ushindi wa magoli 5-0 Wiliete SC.
Yanga SC vs Silver Strikers CAF Champions League ni mchezo mkubwa unaofuata kwenye ratiba utachezwa Oktoba 18, 2025 Uwanja wa Bingu-Malawi. Silver Strikers mechi 6 zilizopita ilipata ushindi 3, haikupoteza ilipokuwa nyumbani. Yanga SC mechi 6 zilizopita ushindi mechi 5. Katika Ligi ya Malawi, Silver Strikers ipo nafasi ya tatu inakutana na Yanga SC ambayo katika ligi ya NBC ipo nafasi ya nne.
SOMA HII: Kuelekea Yanga SC vs Silver Strikers CAF Champion League 2025 | Timu hizo zilifikaje hapo?
Unasubiri nini? Vuna mamilioni sasa hivi
Kuna jambo umekwama kwa sasa kuhusu mkwanja? Usiogope, rubani ni jasiri na kazi yake ni kupaisha kindege cha SportPesa. Cheza sasa hivi Aviator uvune mamilioni bofya hapa chini.

Yanga SC vs Silver Strikers CAF Champions League nani anapewa nafasi ya ushindi?

Kuelekea kwenye mchezo wa Yanga SC vs Silver Strikers CAF Champions League wataalamu wanasema kuna uwezekano mdogo wa sare. Mrisho Ngasa mchezaji wa zamani wa Yanga SC, Simba SC ameipa nafasi kubwa Yanga SC kushinda kutokana na uzoefu. Ni asilimia 47 zinatajwa kuwa mchezo huo utakuwa sare. Licha ya Yanga SC kupewa nafasi kubwa bado mpinzani ana nafasi kupata matokeo nyumbani.
Romain Folz Kocha Mkuu wa Yanga SC kuhusu mchezo ujao
“Kikubwa ni kwamba tunamuheshimu mpinzani wetu na malengo makubwa ni kupata matokeo mazuri kwenye mchezo wetu. Tunajitahidi kuona kwamba tunakuwa imara katika kila Idara. Kila timu kwenye hatua hii ni bora, ninaamini hautakuwa mchezo kama ilivyokuwa dhidi ya Wiliete SC,” amesema Folz.
Mechi 6 za Yanga SC

Septemba 12,2025 – Yanga 1-0 Bandari ya Kenya. (Mechi ya kirafiki).
Septemba 16, 2025 – Yanga SC 1-0 Simba SC, (Ngao ya Jamii).
Septemba 19, 2025 – Wiliete 0-3 Yanga SC, (Ligi ya Mabingwa Afrika
Septemba 24,2025 – Yanga SC 3-0 Pamba Jiji, (Ligi ya NBC).
Oktoba 27,2025 -Yanga 2-0 Wiliete SC, (Ligi ya Mabingwa Afrika).
Septemba 30,2025, Mbeya City 0-0 Yanga SC, (Ligi ya NBC).
SOMA HII: Wiliete SC 0-3 Yanga SC CAF Champions League 2025 | Magoli yote, takwimu muhimu, super sub

Mechi 6 za Silver Strikers
Silver Strikers 1-0 Chitipa United, mchezo wa League Agosti 27 2025.
Shire FC 1-4 Silver Strikers, Septemba 11 2025 Malawi Cup
Elgeco Plus 1-1 Silver Strikers, Septemba 21 2025, Ligi ya Mabingwa Afrika.
Silver Strikers 0-0 Elgeco Plus Septemba 27 2025, Ligi ya Mabingwa Afrika.
Blue Eagles 0-3 Silver Strikers Oktoba 2 2025, Malawi Cup.
Bullets 2-1 Silver Strikers Oktoba 5 2025, Malawi Cup.
H2H
Silver Strikers FC vs Yanga SC CAF Champions League, Oktoba 18, 2025 Uwanja wa Bingu, Malawi.
Yanga SC vs Silver Strikers FC, Uwanja wa Benjamin Mkapa, Oktoba 25, 2025.
Orodha ya wachezaji wa Yanga SC waliolekea Malawi

Msafara wa wachezaji 24 wa kikosi cha Yanga SC umeanza safari Oktoba 16 2025 kuelekea Malawi kwa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Silver Strikers.
Djigui Diarra, Aboutwalib Mshery, Khomein, Israel Mwenda, Kouma, Boka, Mohamed Hussein, Dickson Job, Assinki, Bakari Nondo, Ibrahim Bacca.
Aziz Andambwile, Balla Conte, Mudathir Yahya, Duke Abuya, Doumbia, Pacome, Edmund John, Chikola, Clement Mzize, Ecua, Maxi Nzengeli, Prince Dube na Boyeli.
SOMA HII: Usajili wa Yanga SC orodha ya wapya 11 msimu wa 2025/26 | Rekodi, magoli na timu walizotoka

Hitimisho
Yanga SC vs Silver Strikers CAF Champions League ni mwanzo wa safari kuelekea hatua ya makundi. Wananchi waliwapata ushindi wa jumla ya magoli 5-0 dhidi ya Wiliete hatua iliyopita. Je, watawezana na wapinzani wao Silver Strikers iliyowaondoa Elgeco Plus kwa faida ya goli la ugenini? Matokeo na takwimu zote utazipata hapa.
Bonyeza hapa chini na ujishindie mamilioni kwa kucheza SportPesa Supa Jackpot 17


