- Yanga SC yashusha mashine hii nyingine usiku: Kuuwasha moto Tetesi, usajili Ligi Kuu ya NBC 2025/26.
- Ni Mohamed Doumbia ambaye amesajiliwa kutoke FC Slovan Liberec ya Jamuhuri ya Czech.
- Nyota huyo mwenye umri wa miaka 26, anatajwa kuwa Balaa jipya kwa walinzi na makipa Ligi Kuu ya NBC 2025/26.
Uongozi wa Yanga usiku huu umemtambulisha rasmi kiungo, Mohamed Doumbia. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 26 amejiunga na Yanga kutokea FC Slovan Liberec ya Jamuhuri ya Czech. Staa huyo ana uwezo mkubwa wa kucheza kwenye maeneo finyu, kupiga mashuti ya mbali na kutengeneza nafasi kwa wengine.
Cheza sasa ‘Kindege’ SportPesa uvune mamilioni muda huu
Wakati ukihabarika na utamu wa makala hii, kumbuka unaweza kushinda mamilioni muda huu. Cheza sasa mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kupitia Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa bonyeza picha hii chini.

Kuhusu usajili wa Doumbia Yanga

Licha ya kumtambulisha rasmi leo, imethibitishwa kuwa Yanga tayari walimalizana na Doumbia tangu mwezi Mei mwaka huu. Doumbia anakuja kurithi mikoba ya Stephanie Aziz Ki. Hii ni kutokana na akili, nguvu na uwezo wa kucheza nafasi mbalimbali uwanjani zikiwemo 8 na 10.
SOMA HII PIA: Balla Conte amesaini rasmi Yanga SC na kutambulishwa kuelekea Ligi Kuu NBC 2025/26
Bado Yanga hawajamaliza, mashine hizi zinasubiri utambulisho.
Licha ya kutangaza kumalizana na mastaa zaidi ya watano wapya mpaka sasa. Uongozi wa Yanga SC umeendelea na ujenzi wa kikosi chao. Bado kuna listi ya mastaa wengine wakubwa wanasubiri utambulisho akiwemo nahodha wa zamani wa Simba Mo Hussein.
Ogopa matapeli Pacome, Maxi, Abuya mpaka 2027

Yanga pia imeendelea kuwapa mikataba mipya baadhi ya mastaa wao. Viungo Maxi na Abuya ni wote wameongeza mikataba ya miaka miwili kuendelea kusalia ndani ya Yanga. Hivyo mastaa hao wanatarajia kumaliza rasmi mikataba yao mwaka 2027.
SOMA HII ZAIDI: Yanga SC imetambulisha wapya 10 dirisha la usajili Ecua afungua Agosti / Walioongeza mikataba/ Usajili
Wengine walioongezewa mikataba Yanga mpaka sasa
Mpaka sasa Yanga SC tayari imefanikiwa kuwaongezea mikataba baadhi ya mastaa wao kadhaa. Miongoni mwa mastaa hao ni Pamoja na nahodha wao msaidizi, Dickson Job, Kiungo Denis Nkane na Mudathir Yahya. Imeelezwa kuwa Yanga wanaendelea kufanya maboresho ya mikataba ya mastaa wengine.
Mohamed Hussein ‘Tshabalala’

Yanga na Tshabalala wamemalizana na kilichobaki ni Yanga kumtangaza staa huyo. Hii ni baada ya kuwepo mazungumzo ya muda mrefu kutoka kwa pande zote mbili. Tshabalala amesaini mkataba wa miaka miwili kucheza Yanga.
Kufuatia hatua hiyo, Tshabalala amewaaga rasmi Simba na familia nzima ya timu hiyo kwa barua yake rasmi. Barua hiyo aliiweka katika kurasa za mitandao yake ya kijamii. Kama Sehemu ya kuheshimu mchango wa familia hiyo katika maisha yake kwa kipindi cha miaka 11 aliyodumu na kikosini.
SOMA HII ZAIDI: Yanga SC yatambulisha wapya 9 Andy Boyeli ndani/ Wengine bado wanashushwa 2025/26 balaa
Kikosi kipya kusukwa chini ya kocha mpya Msauzi,
Kikosi hiko kipya cha Wananchi kinakuja kuanza kusukwa na aliyewahi kuwa kocha msaidizi wa Mamelodi Sundowns, Roman Folz. Kocha huyo ni miongoni mwa wakufunzi wenye wasifu mkubwa na uzoefu na sola la Afrika. Hali hii inaonekana kutarajiwa kuwapa faida Yanga katika kuunda kikosi kuelekea msiomu ujao wa 2025/26.
Folz kuanza na Pre-Season nzito
Kocha huyo anatarajiwa kuanza rasmi majukumu yake ndani ya kikosi cha Yanga, kupitia kambi ya maandalizi kabla ya msimu ‘Pre-season’. Kuhusu wapi kambi ya timu hiyo itakuwa kwa ajili ya pre-season, Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe ameweka wazi kuwa tayari wamepokea mialiko kadhaa. Kati ya mialiko hiyo Yanga wamethibitisha mmoja tu, watakapoenda Rwanda kuwavaa Rayon Sports.

Hitimisho: Msimu wa 2025/26 moto utawaka
Kwa namna ambavyo timu zinasajili, hususani Yanga inaonekana kudhamiria kuendelea pale ilipoishia msimu uliopita. Hii ikiwa ni Pamoja na kwenda mbali zaidi kwenye kukusanya makombe msimu ujao. Hii inaweza kuonekana katika namna ambavyo wamefanikiwa kuzuia mastaa wao muhimu kuondoka. Mpaka sasa ni Aziz Ki pekee ndio staa muhimu wa Yanga ambaye ameondoka hivyo ni wazi wapinzani wanapaswa kujipanga vizuri kwa moto

