DiarraDiarra
  • Simba SC yamtaja beki Rushine De Reuck kiwango chake alichoonyesha na magoli aliyofunga kwenye ligi.
  • Djigui Diarra tuzo ya Septemba yazua gumzo ikiwa ni mara ya kwanza kuitwaa ndani ya ligi ya NBC 2025/26.
  • Romain Folz, Kocha Mkuu wa Yanga SC alikuwa katika kinyangiro cha kuwania tuzo iliyochukuliwa na Ahmad wa JKT Tanzania.

Mlinda mlango namba moja wa Yanga SC, Djigui Diarra tuzo ya Septemba yazua gumzo kama alistahili au hakustahili kuwa mchezaji bora. Kipa huyo ni chaguo la kwanza chini ya Kocha Mkuu, Romain Folz amekaa langoni kwenye mechi mbili. Hii inakuwa tuzo ya kwanza kutolewa msimu wa 2025/26.

SOMA HII: Kariakoo Dabi vita ya Diarra na Camara inaanza | Takwimu, mechi, magoli | Septemba 16 2025

Shinda sasa na ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni muda huu

Muda wa kushinda na SportPesa, unaweza kushinda mamilioni sasa hivi. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kupitia Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa bonyeza picha hii chini.

image

Djigui Diarra alistahili ama hakustahili kutwaa tuzo?

Djigui Diarra tuzo
Diarra Twakimu

Djigui Diarra tuzo ya Septembe yazua gumzo kutokana na aina ya mechi ambazo walicheza na matokeo. Katika mchezo dhidi ya Pamba Jiji rekodi zinaonyesha kuwa Pamba Jiji FC hawakupiga shuti ambalo lililenga lango. Mchezo wa pili ugenini dhidi ya Mbeya City bado hakukuwa na mashambulizi mengi kutoka kwa wapinzani wao.

Jina ambalo limekuwa likitwaja ni Rushine De Reuck. Huyu ni beki wa Simba SC ambaye katika mechi mbili alifunga magoli mawili. Mbali na kufunga magoli hayo timu hiyo ilivuna pointi sita wakati Yanga SC ikivuna pointi nne.

Ndani ya Desemba 2025, mchezo wa ufunguzi ilikuwa Yanga SC 3-0 Pamba Jiji FC ulichezwa Uwanja wa Mkapa. Mchezo wa pili ilikuwa Mbeya City 0-0 Yanga SC. Huu ulichezwa Uwanja wa Sokoine Mbeya.

Katika mechi mbili ambazo ni dakika 180 Diarra aliokoa hatari moja mchezo dhidi ya Mbeya City. Mechi ilichezwa Uwanja wa Sokoine dakika ya 89 Vitalis Mayanga wa Mbeya City jaribio lake lilizuiwa. Katika dakika nyingine hakukuwa na shambulizi la hatari.

SOMA HII: Tuzo ya kipa bora 2024/25 Camara wa Simba SC na Diarra wa Yanga SC vitani

image

Wachezji aliowashinda Diarra

Taarifa iliyotolewa na Idara ya Habari na Mawasiliano ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara, (TPLB) ilimtaja Diarra kuwa mchezaji bora. Ni Anthony Tra Bi wa Singida Black Stars na Mohamed Bakari wa JKT Tanzania. Wawili hawa waliingia fainali na Diarra kuchaguliwa kuwa mshindi.

Diarra katika mechi mbili alitumia dakika 180. Timu ya Yanga SC ilikusanya pointi nne kati ya sita ambazo ilikuwa ikisaka.Kwenye msimamo ipo nafasi ya 4 ikiwa na pointi 4 baada ya mechi mbili.

Tuzo ya kocha bora Septemba

Ahmad Coach
Ahmad Kocha Mkuu wa JKT Tanzania mwenye tuzo ya kocha bora Septemba. Source: Ligi Kuu.

Wakati Diarra akitwaa tuzo ya mchezaji bora kwa Septemba, kocha bora ni Ahmad Ali. Huyu anakinoa kikosi cha JKT Tanzania. Ni Romain Folz wa Yanga SC na Miguel Gamondi wa Singida Black Stars alikuwa akishindana nao.

Kwenye mechi mbili za Septemba, JKT Tanzania ilifungana goli 1-1 dhidi ya Coasta Union. Mchezo wa pili ilikuwa Coastal Union 1-2 JKT Tanzania. Mechi zote ilikuwa ugenini.

Huyu hapa Ahmed Ally kuhusu Rushine

Mpanzu atua kwa kishindo Misri
De Reuck beki wa Simba SC 2025/26. Source: Simba SC.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC ameweka wazi kuwa Septemba walicheza mchezo mmoja. Aliongeza kuwa kwenye mechi hiyo walipata ushindi na kuonyesha kiwango bora. Miongoni mwa wachezaji waliofanya vizuri ni beki Rushine De Reuck ambaye ni beki raia wa Afrika ya Kusini.

“Hii tuzo iliyotolewa ni ya Septemba. Simba SC tulicheza mchezo mmoja dhidi ya Fountain Gate tukapata ushindi. Oktoba tukacheza mchezo mmoja dhidi ya Namungo tukapata ushindi.

“Kwenye mechi ambazo tumecheza Rushine alikuwa katika kiwango bora. Yeye alifunga na kulinda kwa kuwa timu haikufungwa. Hivyo hakuwa na vigezo kuingia kwenye tuzo kwa kuwa kuna timu Septemba zilicheza michezo miwili.

“Ila kama ingekuwa ni tuzo za mzunguko wa kwanza basi alifanya vizuri. Na Seleman Matola ambaye ni kocha alifanya vizuri. Timu ilishinda mechi zote na kuonyesha kiwango kizuri,”.

SOMA HII: Wiliete SC 0-3 Yanga SC CAF Champions League 2025 | Magoli yote, takwimu muhimu, super sub

Hitimisho

 Djigui Diarra tuzo ya Septemba yazua gumzo ikiwa ni mwanzo wa msimu mpya wa 2025/26. Kwenye ligi ya NBC Yanga SC ilishuka uwanjani kwenye mechi mbili na alikusanya hati safi zote. Watani zao wa jadi Simba SC walishuka uwanjani kwenye mchezo mmoja.

image
Share this: