- Mchezaji wa zamani wa Mamelod Sundowns ya Afrika mwenye uwezo mkubwa kutimiza majukumu yake uwanjani.
- Rushine De Reuck kinara wa ufungaji kwa mabeki ndani ya NBC 2025/26 namba nne kwa ubora Afrika.
- Ahmed Ally azungumzia ubora wake na faida ambayo anawapa Simba SC.
Rushine De Reuck kinara ufungaji kwa mabeki ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara ya NBC. Huyu ni mchezaji wa kwanza kutambulishwa ndani ya kikosi hicho. Kwenye mechi mbili kafunga magoli mawili. Alitambulishwa kwa kishindo Julai 29 2025.
SOMA HII: Simba SC yamtambulisha mrithi wa Zimbwe Jr 2025/26 Naby Camara/ Orodha ya wachezaji wapya hii hapa
Shinda mamilioni na Kindege cha Sportpesa

Ni muda wa kushinda mamilioni kupitia mchezo wa aviator. Huu ni maarufu kama Kindege kutoka Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa. Cheza sasa upate mgao wako.
Rushine De Reuck kinara wa ufungaji NBC 2025/26

Beki huyu amekuwa imara kwenye kuokoa hatari na kupiga pasi ndefu. Rushine De Reuck ni kinara wa ufungaji ndani ya NBC 2025/25 kwa upande wa mabeki. Ikumbukwe kwamba alifungua akaunti ya magoli kwenye mchezo wake wa kwanza dhidi ya Fountain Gate.
Huyu ni mchezaji wa zamani wa Mamelodi Sundowns. Ameonyesha uwezo wa kucheza kwa ufasaha nafasi tatu za ulinzi. Kiasili yeye ni mlinzi wa kati, lakini ana uwezo mkubwa wa kucheza kama mlinzi wa pembeni na kiungo wa ulinzi. Kwenye mechi ambazo amecheza kaonyesha kiwango kikubwa.
Magoli ya Rushine De Reuck

Akaunti ya magoli alifungua kwenye mchezo dhidi ya Fountain Gate, Uwanja wa Mkapa. Katika mchezo huo alitumia pasi ya kiungo Jean Ahoua ambaye alipiga kona. Ni goli la mapema kufungwa ilikuwa dakika ya 5.
Alifunga goli la pili kwenye mchezo dhidi ya Namungo FC. Katika mchezo huo alitumia pasi ya Maema ambaye alipiga faulo. Alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo.
Magoli yake yote mawili ambayo yanamfanya awe kinara wa ufungaji kwa mabeki yalitokana na mapigo huru. Kasi yake kwenye kumalizia mapigo huru yanamfanya awe tishio. Mguu wake wenye nguvu ni ule wa kulia.
Mechi zote ambazo alifunga Simba SC ilipata ushindi wa magoli 3-0. Ilikuwa Simmba SC 3-0 Fountain Gate na Simba SC 3-0 Namungo FC. Mechi zote hizi zilichezwa Uwanja wa Mkapa.
SOMA HII: Mpanzu atua kwa kishindo Misri, Simba watoa tamko zito

Huyu hapa beki mwenyewe kuhusu
“Kikubwa ambacho tunakifanya ni kuona tunapata matokeo mazuri. Ushirikiano ambao upo unatufanya tuwe imara. Kila mchezaji anapenda kuona tunapata ushindi.
“Ushindani ni mkubwa kutokana na kila timu kujipanga. Ambacho tunafanya ni kuhakikisha tunakuwa kwenye furaha. Mashabiki waendelee kuwa pamoja nasi,”.
Ahmed Ally kuhusu Rushine

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari Simba SC amesema beki huyo ana akili kubwa. Uwepo wake unafanya kuwe na idadi kubwa ya washambuliaji wakati wa mapigo huru. Kutokana na uwepo wake anaongeza hali ya hatari kwa wapinzani.
“Unapomzungumzia Rushine hapa unamzungumzia kinara wa ufungaji. Ana magoli mengi kuliko wachezaji wa timu nyingine. Anakupa utulivu akiwa kwenye eneo lake la ulinzi.
“Mbali na kuwa makini ana uwezo wakufunga magoli yanayotokana na mipira yakutengwa. Hili linafanya kuwa na idadi kubwa ya washambuliaji langoni kwa mpinzani. Hapa bado hajachanganya ujue, mazuri yanakuja Wanasimba,”.
Hitimisho
Simba SC kwenye ligi imecheza jumla ya mechi sita. Katika dakika 180 imefunga magoli 6 huku Rushine De Reuck kinara ufungaji akiwa nayo mawili. Kwenye msimamo mnyama anaongoza ligi ya NBC 2025/26.


