Mpanzu atua kwa kishindo MisriDe Reuck
  • Rushine De Reuck rasmi asaini na kutambulishwa Simba SC, anaweza kuzima namba 3 uwanjani.
  • Huyu ni nyota wa zamani wa Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini na Maccabi Petah Tikva ya Israel.
  • Bosi atamba Mashine nyingine 7 kutangazwa, tetesi usajili Ligi Kuu NBC 2025/26.
  • Rushine ataungana na kikosi cha Simba SC kilichoelezwa kuondoka alfajiri kwenda kambini Ismailia, Misri kwa ajili ya ‘Pre-season’.

Kwa kishindo kikubwa Rushine De Reuck rasmi asaini na kutambulishwa Simba SC. Hii ni baada ya kimya cha muda kwa Wanamsimbazi kwenye dirisha hili la usajili hatimaye kumeanza kuchangamka. Baada ya kutambulishwa Rushine anatarajiwa kuungana na kikosi cha Simba SC, kinachoondoka alfajiri kwenda kambini Ismailia, Misri kwa ajili ya ‘Pre-season’.

Shinda mamilioni na ‘Kindege’ cha Sportpesa

Endelea kuhabarika na makala hii, huku pia ukicheza na kushinda mamilioni kupitia mchezo wa aviator maarufu kama Kindege kutoka Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa kwa kubonyeza picha hii chini.

image

Anacheza kwa ufasaha nafasi 3 za ulinzi

De Reuck
De Reuck

Staa huyo wa zamani wa Mamelodi Sundowns anaweza kucheza kwa ufasaha nafasi tatu za ulinzi. Kiasili yeye ni mlinzi wa kati, lakini ana uwezo mkubwa wa kucheza kama mlinzi wa pembeni na kiungo wa ulinzi. Hii inatarajiwa kuwapa Simba wigo mpana wa kumtumia katika maeneo mbalimbali uwanjani.

SOMA HII PIA: Simba SC yashtua na fumbo la jezi namba 6 ni Feisal au udhamini?

Kuhusu safari ya kwenda Misri

Kikosi cha Simba alfajiri ya kesho Jumatano kinatarajiwa kuondoka kuelekea nchini Misri. Safari hii ni kwa ajili ya kuweka kambi ya maandalizi ya kabla ya msimu wa mashindano (Pre Season) kwa takribani mwezi mmoja. Timu hiyo inatarajiwa kwenda kuweka kambi katika mji wa Ismailia.

Kambi hiyo ilitumiwa na Simba msimu uliopita. Pamoja na wachezaji ambao wamesalia ndani ya kikosi cha timu hiyo, mastaa wote wanatarajiwa kuwa sehemu ya kambi hiyo. Taarifa hii imethibitishwa na Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally.

Ahmed akizungumzia hilo amesema: “Kikosi chetu kitaondoka kesho alfajiri kuelekea Misri. Hii ni kwa ajili ya kuweka kambi ya maandalizi ya kabla ya msimu. Kambi inatarajiwa kuwa na nyota wetu wote isipokuwa waliopo kwenye majukumu ya timu ya Taifa inayojiandaa na michuano ya CHAN.

“Kikosi cha Simba kinatarajiwa kurejea nchini Agosti 28, mwaka huu. Mara baada ya kurudi Simba tutaanza msimu mpya wa mashindano 2025/2026 tukiwa na matumaini makubwa ya kufanya vizuri.”

Semaji la Simba SC Ahmed atangaza mashine 7 mpya

Ahmed Ally
Ahmed Ally

Kwenye mipango ya Simba kwenye dirisha hili la usajili. Meneja wa Habari na mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally ameweka wazi kuwa Simba SC imepania kufanya usajili mkubwa kuelekea msimu ujao. Ikumbukwe kwamba timu hiyo msimu wa 2024/25 ilikosa mataji yote jambo linaloelezwa kuwapa hasira kubwa.

“Kwa sasa viongozi wa Simba SC wametapakaa kila kona kwenye nchi za Afrika. Hii ni katika kuhakikisha wanamalizia usajili wa wachezaji wapya. Huu ni usajili mwingine wa kishindo na sitaongea sana safari hii nitaacha watu waone wenyewe. Tumekamilisha usajili wa wachezaji saba na bado tunaendelea,” amesema Ahmed.

SOMA HII ZAIDI: Jonathan Sowah rasmi asaini Simba SC: Ahmed atangaza mashine 7 mpya  tetesi usajili Ligi Kuu NBC 2025/26

Wachezaji walioachwa na Simba SC mpaka sasa

Kama sehemu ya maboresho ya kikosi chao Simba tayari wameachana na kundi kubwa la wachezaji. Baadhi ya mastaa ambao wamepewa ‘thank you’ na Simba ni Pamoja na Aishi Manula aliyeenda Azam FC. Wengine ni Pamoja na Omary Omary ambaye amepelekwa kwa mkopo Mashujaa FC.

Wengine ni, Fabrince Ngoma mkataba wake umeisha. Kelvin Kijili ametimkia Singida Black Stars. Valente Nouma naye ameachwa, nahodha Mohammed Hussein amemaliza mkataba na listi hii inatarajiwa kuongezeka. Hii ni pale Simba itakapoanza rasmi kutangaza mastaa wake.

Hitimisho: Hawa wanatajwa kuwa wachezaji wapya waliomalizana na Simba

Rushine De Reuck rasmi asaini na kutambulishwa Simba SC
Jonathan Sowah Simba

Ukiachana na Rushine ambaye ametangazwa leo, Simba inaelezwa kumalizana na baadhi ya mastaa. Baadhi ya majina ambayo yanatajwa kumalizana na Simba, na kuichezea timu hiyo msimu ujao ni; Sowah, kiungo Privat Djéssan Bi (21), Khadim Diaw (26), na Wilson Nangu (23). Nangu amesaini miaka miwili na Simba hivyo msimu ujao atavaa jezi nyekundu.

SOMA HII HAPA: Simba SC kuelekea msimu wa 2025/26 kupitisha panga kwa wachezaji/ Tamko latolewa/ Kupoteza Dabi 5

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.