Matokeo ya Simba SCSeleman Mwalimu vs Namungo FC
  • Namungo FC imepoteza jumla ya mechi 8 dhidi ya Simba SC kati ya 13 walizokutana uwanjani
  • Simba SC 3-0 Namungo FC, Oktoba 1 2025 kwenye mchezo wa ligi ya NBC ambayo ni namba nne kwa ubora
  • De Reuk kinara wa ufungaji atwaa tuzo ya mchezaji bora

Simba SC 3-0 Namungo FC ni matokeo ya mchezo wa mzunguko wa pili Ligi Kuu Bara ya NBC Uwanja wa Mkapa. Ushindi huo unampaisha mnyama mpaka kuongoza ligi. Baada yakucheza mechi mbili za ligi wanafikisha pointi sita na wapinzani wao Namungo FC nafasi ya 9 wakiwa na pointi 4.

SOMA HII: Simba SC vs Namungo FC Oct 1, 2025 – Live Scores, vikosi, h2h, Takwimu na taarifa mpya za vikosi

Paisha Kindege cha SportPesa uvune mamilioni

image

Ni muda wa rubani kuwa katika mavuno. Unapaisha Kindege na kushinda haraka na rahisi mno. Cheza Aviator upate mgao wako.

Simba SC 3-0 Namungo FC magoli yote

Simba SC 3-0 Namungo FC
Beki wa Simba SC Chamou akishangilia goli dhidi ya Namungo FC, Uwanja wa Mkapa. Source: Simba SC.

Ubao wa Uwanja wa Mkapa Oktoba Mosi ulisoma Simba SC 3-0 Namungo FC. Magoli ya mnyama yalifungwa na mabeki wawili na mshambuliaji mmoja. Kipindi cha kwanza lilifungwa goli moja na kipindi cha pili yalifungwa magoli mawili.

Karabou Chamou beki wa Simba SC alifunga goli la kwanza dakika ya 43. Chamou alimalizia pigo la kona iliyopigwa na Joshua Mutale akiwa ndani ya 18. Mpira wake wa kichwa ulikwenda kujaa nyavuni na kumshinda mlinda mlango Jonathan Nahimana.

 Rushine De Reuck raia wa Afrika Kusini alifunga goli lake la pili kwenye ligi. Ikumbukwe kwamba kwenye ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Fountain Gate alifungua akaunti yake ya mabao. Huyu ni mchezaji wa zamani wa Mamelod Sundowns pendezo la Fadlu Davids. Kwenye mchezo dhidi ya Namungo FC alitumia mpira wa faulo iliyopigwa na Neo Maema dakika ya 60.

Mshambuliaji Seleman Mwalimu alifunga bao la tatu dakika ya 84. Mwalimu alimpora mpira beki Hussen Kazi na kuingia haraka ndani ya 18 akitumia mguu wa kushoto kupachika goli hilo. Unakuwa ni ushindi wa pili mfululizo kwa Simba SC, Uwanja wa Mkapa.

SOMA HII: Namungo FC—Muhtasari, Kikosi, Ratiba, Matokeo, Takwimu, Tuzo na Habari Mpya

image

Rushine De Reuck mchezaji bora

Nyota wa mchezo ni Rushine ambaye alikuwa kwenye siku nzuri kazini. Katika dakika 90 alizocheza alikuwa na uwezo wa kutoa pasi ndefu na fupi kwa usahihi. Mbali na hilo ni kuokoa hatari za Namungo FC zilizokuwa zinakwenda katika lango la Simba SC.

Mpanzu atua kwa kishindo Misri
De Reuck beki wa Simba SC aliyefunga magoli mawili msimu wa 2025/26. Source: Simba SC.

Anakuwa ni kinara kwenye upande wa kufunga magoli akiwa nayo mawili. Alifungua ukurasa kwenye mchezo dhidi ya Fountain Gate ilikuwa dakika ya 5. Magoli yote aliyofunga beki huyo yametokana na adhabu ya mapigo huru.

Beki huyo amebainisha kuwa sio kazi rahisi kuwa kwenye mwendelezo huo. Hiyo inatokana na ugumu wa ligi ila kwa ushirikiano watafanya vizuri. Ameongeza kuwa kila mchezo kwao ni muhimu kupata matokeo mazuri.

“Sio rahisi kwangu kufunga na kuwa katika ubora. Unajua ligi ina ushindani mkubwa na kila timu inahitaji ushindi. Kilichopo ni kuona tunakuwa kwenye mwendelezo wa bora hivyo mashabiki wazidi kuwa nasi.”

SOMA HII: Simba SC 3-0 Fountain Gate FC | Rushine afungua akaunti ya magoli Uwanja wa Mkapa

image

Kikosi cha Simba SC kilichoanza  dhidi ya Namungo FC

Mlinda mlango

Yakoub Suleiman

Mabeki

Shomari Kapombe

Anthony Mligo

Rushine De Ruck

Karabou Chamou

Viungo

Kante Allasane

Yusuph Kagoma

Joshua Mutale

Elie Mpanzu

Mshambuliaji

Steven Mukwala

Morice Abraham

Wachezaji wa akiba

Jonathan Sowah

Jean Ahoua

Naby Camara

Semfuko

David Kameta

Kibu Dennis

Hussen Abel

Wilson Nangu

Neo Maema

Seleman Mwalimu

Kikosi cha Namungo FC kilichoanza dhidi ya Simba SC

Nahimana kazini
Nahimana Jonathan kipa namba moja wa Namungo FC. Source: Simba SC.

Mlinda mlango

Jonathan Nahimana

Mabeki

Ali Ahmed

Daniel Amoah

Bakari Hussein

Faria Ondongo

Viungo

Jacob Masawe

Hassan Kabunda

Geofrey Julius

Abdulkarim Kiswanya

Abdallah Mfuko

Mshambuliaji

Heritier Makambo

Wachezaji wa akiba

Pius Buswita

Rodgers Gabriel

Ayoub Semtawa

Herbert Lukindo

Abubakar Mfaume

Abdallah Denis

Fabrice Ngoy

Aziz Said

Mussa Mussa

Frank Mathew

Hitimisho

Simba SC 3-0 Namungo FC ni mchezo wa 13 kwa wababe hawa kukutana kwenye ligi. Katika mechi hizo Simba SC imepata ushindi mara 8. Sare ni 5 pekee huku Namungo FC ikiwa haijapata ushindi.

image
Share this: