Meneja Mkuu Simba SC Dimitar Pentev-Meneja Mkuu Simba SC Dimitar Pentev-
  • Hatimaye uongozi wa Simba SC umetoa taarifa kwa Umma kumhusu kocha anayemrithi, Fadlu Davis.
  • Dimitar Pantev kocha mpya Simba SC, ndivyo imeeleza taarifa hiyo.
  • Pantev amejiunga na Simba SC kwa mshtuko mkubwa akitokea Gaborone United ya Botswana.

Hatimaye Dimitar Pantev kocha mpya Simba SC. Hii ni kutokana na taarifa kwa Umma iliyotolewa usiku huu. Kocha huyo raia wa Bulgaria anakuja kuchukua majukumu yaliyoachwa na kocha, Fadlu Davis aliyetimkia Raja Casablanca. Dimitar Pantev amejiunga na Simba SC akitokea ndani ya kikosi cha Gaborone United.

SOMA HII ZAIDI: Kocha mpya Simba SC Hemed Morocco hana presha | Ameanza kazi tayari

Shinda sasa na ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni muda huu

Zamu yako kushinda na SportPesa, unaweza kushinda mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kupitia Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa bonyeza picha hii chini.

SEO Banner LV

Dimitar Pantev kocha mpya Simba SC ataiweza mikoba ya Fadlu?

mifumo
mifumo

Uteuzi wa kocha Pantev unakuja baada ya kuondoka kwa kocha, Fadlu Davids ambaye ametimkia nchini Morocco. Simba ilipata mafanikio makubwa na ya haraka chini ya kocha Fadlu. Mafanikio hayo ni pamoja na kuibuka washindi wa pili wa Kombe la Shirikisho Afrika msimu uliopita. Swali kubwa ni Je, kocha huyu ataiweza mikoba?

SOMA HII ZAIDI: Kocha Fadlu Davis kuondoka Simba SC? Utata waibuka! Simba watoa tamko hili

SEO Banner LV

Makubaliano ya Simba SC na kocha Dimitar Pantev

Dimitar Pantev kocha mpya Simba SC
Kocha Simba SC

Taarifa za kuaminika kutoka Botswana zimethibitisha kuwa Simba SC imelazimika kuilipa fidia Gaborone United, ili kumpata kocha Pantev. Hii ilikuwa ni sehemu ya makubaliano ya kufanikisha uhamisho huo. Chanzo hiko kimeeleza kuwa kocha, Pantev anatarajiwa kuwasili Dar es Salaam mara moja ili kuanza kazi rasmi.

Kocha Pantev anatarajiwa kutumia sehemu kubwa ya benchi la ufundi la sasa. Licha ya msimamo huo, lakini kocha huyo pia anatarajiwa kupewa nafasi ya kuongeza nguvu. Hii itatokana na mapungufu na ubora wa benchi la ufundi la sasa kuendana na tathimini ya kocha huyo mpya.

Mfahamu zaidi kocha, Dimitar Pantev

Pantev mwenye umri wa miaka 49, ni mzaliwa wa Varna, Bulgaria. Mkufunzi huyo ana urefu wa mita 1.79 ambaye aikuwa akihudumu kama kiungo wa ulinzi, na ulinzi wa kati wakati akiwa mchezaji. Amecheza soka kwenye klabu mbalimbali za kwao Bulgaria ikiwemo Spartak Varna.

Mafanikio yake kama kocha

Ubingwa wa Gaborone United
Ubingwa wa Gaborone United

Kocha huyo mpya wa Simba SC ana rekodi nzuri ya mafanikio katika klabu tofauti barani Afrika. Akiwa kocha wa Gaborone United, aliongoza timu hiyo kushinda Ubingwa wa Ligi nchini Botswana msimu uliopita 2024/25. Pia amefanya vyema akiwa kocha wa Victoria United nchini Cameroon.

SOMA HII PIA: Simba SC inasukwa timu imara kuelekea 2025/26 | Wachezaji wapya wameanza kufunga magoli

SEO Banner LV

Mfumo na Falsafa za Dimitar Pantev

Pantev anasifika zaidi kwa falsafa ya soka la kushambulia na umiliki wa mchezo. Falsafa hii ilishuhudiwa katika michezo yao ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Simba SC. Katika michezo hiyo miwili licha ya Simba kupata ushindi wa jumla wa mabao 2-1 na kufuzu, lakini walikumbana na ushindani mkubwa.

Malengo ya Simba SC na mtihani kwa kocha Pantev

Meneja wa boli- #NguvuMoja
Pantev

Simba SC inatarajia Pantev atarejeshe utawala wao ndani ya ligi ya Tanzania. Hii ni baada ya utawala huo kuchukuliwa na watani zao Yanga SC kwa misimu 4 mfululizo.  Mtihani mwingine mkubwa wa kocha huyo mpya ni kuhakikisha Simba SC, inaleta ushindani mkubwa kwenye mashindano ya kimataifa, hasa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kocha huyo atakabiliwa na changamoto ya kuunganisha kikosi kipya. Kuweka mfumo wa ufundishaji unaolingana na matarajio ya mashabiki. Mwisho atapaswa pia kushindana na timu kadhaa zilizo na nguvu ndani na nje ya Tanzania.

Mastaa wapya Simba SC kurudi kambini fasta

Kufuatia uteuzi huo, mastaa wa Simba SC ambao walikuwa kwenye mapumziko, wanatarajiwa kurejea kambini haraka. Mara baada ya kurejea kambini taratibu za kuanza mazoezi ya pamoja zitafanyika mara moja. Hii ni pamoja na kocha huyo mpya kutambulishwa kambini.

Mabosi Simba SC watoa tamko zito

Kwa upande wa uongozi wa klabu, Mwenyekiti wa Bodi ya Simba SC, Crescentius Magori, amesema kwamba: “Tumechagua kocha ambaye tunaamini anaweza kuendana na mipango ya Simba, hasa katika kuhakikisha tunarejea katika nafasi ya juu ndani na nje ya nchi.

“Kocha mwenyewe amethibitisha na kusisitiza kuwa ana shauku ya kuanza kazi rasmi na Simba SC. Lakini pia kukutana na wachezaji wake wapya. Hii yote ni katika kuhakikisha tunafikia malengo yetu msimu huu.

Hitimisho

Licha ya changamoto za hapa na pale mwanzoni mwa msimu huu. Simba SC imeanza mzunguko mpya kwa kishindo baada ya kufanikiwa kushinda mechi zao 2 za kwanza. Uteuzi wa Dimitar Pantev unaleta matumaini kwa mashabiki kwamba timu itarejea kuwa tishio, katika michuano ya ndani na ile ya kimataifa.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.