Simba SC vs Gor Mahia FCFadlu Davids Head
  • Simba SC inasukwa kuwa katika ubora kwa msimu mpya unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa 2025/26.
  • Jonathan Sowah amefungua akaunti ya magoli akiwa na uzi wa Simba SC, alifunga akitokea benchi.
  • Fadlu Davids kwenye mkakati mzito wa kazi, Jean Ahoua mkali wa kucheka na nyavu anatengenezwa upya.

Fadlu Davids, Kocha Mkuu wa Simba SC amesema inasukwa timu imara kuelekea msimu mpya wa 2025/26. Timu ya Simba SC ipo kambini nchini Misri ikiwa ni maandalizi ya msimu mpya. Kocha huyo amebainisha kila hatua wanayopitia ina umuhimu.

Paisha kindege ushinde mamilioni

Kuna mamilioni yanakusubiri sasa hivi. Unachotakiwa kufanya ni kupaisha kindege upate mgao wako. Cheza Aviator ushindi unakusubiri.

Aviator banner

Huyu hapa Fadlu Davids

Simba SC ilicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Kahraba Ismailia na kupata ushindi wa magoli 2-0. Kwenye mchezo huo kocha amebainisha kuwa wachezaji walishirikiana kutafuta matoke. Aliongeza kuna umuhimu kuongeza nguvu kubwa eneo la ulinzi.

Fadlu Davids
Fadlu Davids Kocha Mkuu wa Simba SC. Source: Simba SC.

Soma hii: Fadlu Davids Kocha Mkuu wa Simba SC anatajwa Raja Casablanca

“Kuna hatua ambazo tunazipiga kwa wakati huu. Ushindani upo mkubwa kwa sasa kwenye kila eneo wakati tunazidi kujenga timu imara. Mchezo wetu uliopita wa kirafiki tulikuwa na mpango tofauti.

“Ukiangalia kipindi cha kwanza kulikuwa na wachezaji wengi wageni. Tukakamilisha mchezo tukiwa tunaongoza kwa goli moja. Hata kipindi cha pili tulikuwa na hatua kutokana na mabadiliko ambayo tulifanya.

“Kuna aina ambayo tunaendelea nayo kwa sasa. Kila kipindi kulikuwa na aina yake ya uchezaji. Tunafanyia kazi kubwa eneo la ulinzi kuendelea kuwa bora. Ninawapongeza wachezaji kwa kazi kubwa.

Msikie Jonathan Sowah mshambuliaji mpya Simba SC

Sowah Goal
Sowah mshambuliaji wa Simba SC akifunga kwenye mchezo wa kirafiki.

Soma hii: Mechi ya kirafiki: Simba SC 2-0 Kahraba Ismailia

Kwenye mchezo huo magoli yalifungwa na wachezaji wapya. Mohamed alifungua ukurasa kwenye kufunga. Jonathan Sowah alifunga goli la pili.

Sowah amesema: “Nafikiria tulikuwa tayari kwa mchezo. Ukiangalia namna ilivyokuwa hakuna ambacho nilikuwa nafikiria ambacho kitatokea. Kutoka eneo ambalo nilikuwa na chaguo nililofanya. Ushirikiano mkubwa unafanyika kwa yule anayeanza ama kutoanza.

“Nilishangazwa na goli ambalo nilifunga kwa kuwa sikufikiria kwamba ningefunga. Kulikuwa na makosa kwenye mchezo wetu hilo niliona. Nilianzia benchi na kila wakati nasema kuwa ni Mungu ambaye anajua.

“Pengine kama ningeanza sina uhakika kama ningefunga. Ukiangalia namna nilivyofunga nilikuwa katika mazingira ambayo hayakuwa rahisi. Sikuwa nafikiria kufunga ila nilifikiria kutoa pasi kwa Leonel Ateba.

“Kutoka eneo ambalo nilikuwa nipo niliona wapinzani hawakuwa na kasi kubwa nikafanya maamuzi kupiga. Tumefanya kile ambacho mwalimu amekuwa akituambia. Bado tunazidi kupambana kwa ajili ya kuwa imara,”.

Bajaber nyota mpya Simba SC kaanza kucheka na nyavu

Mohamed Bajaber ambaye ni ingizo jipya amesema amefurahia kufunga goli. Aliongeza kuwa mchezo huo ni muhimu kwa ajili ya msimu mpya. Katika mchezo huo wa kirafiki nyota huyo alifunga goli akiwa ndani ya 18.

“Nimefurahi kupata dakika kwenye mchezo wetu wa kirafiki. Dakika ambazo nimepata ni muhimu kwangu. Hata kufunga ni jambo ambalo limenifurahisha.

“Kwenye mechi za maandalizi ya msimu mpya haya magoli hayatazamwi sana. Kikubwa ni kuona kwamba tunakuwa tayari kwa msimu ujao. Kwani hilo ni kubwa zaidi kwetu.

“Nilipata nafasi kufunga kwenye mchezo na hilo lilitokana na kuwa kwenye mazingira mazuri. Unaona chaguo la haraka kwenye kufanya maamuzi. Hivyo ilikuwa na siwezi kuahidi kuhusu wakati ujao.”

Kambi nchini Misri kazi inaendelea

Mpanzu Misri (-)
Mpanzu nyota wa Simba SC akiwa kambini Misri.

Soma hii: Elie Mpanzu Kibisawala ni Simba SC 2025/26

Kikosi cha Simba SC bado kinaendelea na kambi nchini Misri. Ikumbukwe kwamba ni Julai 8 2025 kundi la kwanza lilikwea pipa. Agosti 12 wachezaji wa Simba SC walifanya mazoezi mepesi kurejesha miili sawa baada ya mchezo wa Agosti 11 2025.

Simba SC inashiriki Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo ni namba nne kwa ubora Afrika. Ipo kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika. Msimu huu ni tofauti na msimu uliopita wa 2024/25.

Ikumbukwe kwamba msimu wa 2024/25 ilishiriki Kombe la Shirikisho Afrika. Katika kombe hili ilifika mpaka fainali. Kwenye mchezo wa fainali ilipoteza kwa kufungwa jumla ya mabao 3-1 dhidi ya RS Berkane ambao ni mabingwa.

Hivyo kwa sasa inafanya maandalizi kuwa imara zaidi. Katika ligi ya NBC ilishuhudia ubingwa ukienda Yanga SC. Na mashindano mengini ni CRDB Cup ambapo ilishia hatua ya nusu fainali.

Kinara wa magoli Jean Ahoua yupo Misri

Jean Misri
Jean Ahoua kiungo mshambuliaji wa Simba SC akiwa Misri. Source: Simba SC.

Soma hii: Jean Ahoua anaondoka Simba SC Feisal kurithi mikoba

Kinara wa magoli ndani ya ligi msimu wa 2024/25 Jean Ahoua yupo kambini. Kiungo huyo mshambuliaji alifunga jumla ya magoli 16 kwenye ligi. Katika mabao hayo alifunga magoli 15 kwa mguu wa kulia na moja kwa pigo la kichwa.

Ni miongoni mwa wachezaji ambao wanapewa nafasi kufanya vizuri msimu ujao.Utakuwa ni msimu wake wa pili akiwa na uzi wa Simba SC. Awali tetesi zilikuwa zinaeleza kuwa huenda akaondoka ndani ya kikosi hicho.

Hitimisho

Simba SC msimu wa 2024/25 ilikuwa inajenga timu kwa kuwa na wachezaji wapya wengi. Wakongwe waliobaki katika kikosi hicho wanaongozwa na Mzamiru Yassin ambaye yupo kambini. Shomari Kapombe yupo katika kambi ya timu ya taifa ya Tanzania.

image
Share this: