Davids Fadlu (-)Davids Fadlu (-)
  • Yanga SC imempasua uwanjani kwenye mechi za ushindani katika mechi walizokutana nje ndani 2024/25 Kariakoo Dabi
  • Fadlu Davids ameondoka Simba SC ikiwa kwenye maandalizi ya mechi ya kimataifa dhidi ya Gaborone United Uwanja wa Mkapa.
  • Mrithi wa mikoba yake anatajwa kutambulishwa hivi karibuni huku kocha msaidizi Seleman Matola akiwa kwenye majanga mazito CAF.

RASMI Fadlu Davids ameondoka Simba SC kwa kusitisha mkataba wake. Awali ilikuwa ni tetesi ambazo tuliziripoti mapema zimetimia Septemba 22 2025. Licha ya jitihada kubwa kufanyika kwa viongozi kubaki na kocha huyo msimu wa 2025/26 imeshindikana. Ni mchezo mmoja wa ushindani alikaa benchi kwenye ardhi ya Tanzania ilikuwa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga SC.

Paisha Kindege cha SportPesa uvune mamilioni

image

Kuna nafasi kubwa kuvuna mamilioni sasa hivi ambayo yanakusubiri. Rahisi sana unachotakiwa kufanya ni kupaisha Kindege cha SportPesa. Cheza Aviator sasa upate mgao wako.

Fadlu Davids ameondoka Simba SC taarifa kamili hii hapa

Fadlu Simba
Fadlu Davids aliyekuwa kocha wa Simba SC 2024/25. Source: Simba SC.

Viongozi wametoa taarifa kamili kwamba Fadlu Davids ameondoka Simba SC. Taarifa hiyo imetolewa Septemba 22 2025. Mchezo wa mwisho kwa kocha huyo kukaa benchi ilikuwa Septemba 20 2025 dhidi ya Gaborone United.

Katika mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa Afrika Simba SC ilipata ushindi wa goli 1-0. Mfungaji pekee alikuwa ni Ellie Mpanzu. Pasi ya upendo kutoka kwa Shomari Kapombe ilikuwa ni ya mwisho kushuhudiwa na Fadlu akiwa benchi.

Soma hii: Kocha Fadlu Davis kuondoka Simba SC? Utata waibuka! Simba watoa tamko hili

Taarifa ya Simba SC imeeleza namna hii: “ Uongozi wa Klabu ya Simba umefikia makubaliano ya kusitisha mkataba na Kocha Mkuu, Fadlu Davids baada ya kuhudumu na timu kwa kipindi cha mwaka mmoja.

“Makubaliano haya ni matakwa binafsi ya kocha Fadlu kwa uongozi wa klabu. Klabu ya Simba SC inamshukuru kocha Fadlu kwa kuiongoza Simba kufika fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu uliopita, (2024/25). Kumaliza ligi nafasi ya pili kwenye ligi kuu ya NBC.

“Uongozi wa klabu unamtakia kheri na baraka kocha Fadlu katika maisha ya soka nje ya Simba.”

Fadlu amevunja mkataba Simba SC

Fadlu Davids alitambulishwa Simba SC Julai 5 2024 akitokea Raja Casablanca ya Morocco ambapo huko alikuwa ni kocha msaidizi. Anaondoka Septemba 22 2025. Mkataba wake ulikuwa ni miaka miwili. Hivyo kocha huyo amevunja mkataba wa mwaka mmoja ambao ulikuwa umesalia.

Yanga SC mwiba mkali kwa Fadlu Davids

Profesa Pacome
Profesa Pacome kiungo mshambuliaji wa Yanga SC aliyefunga goli mbele ya Fadlu. Source: Yanga SC.

Kocha Fadlu anaondoka Simba SC akiwa hajaambulia ushindi mbele ya Yanga SC. Katika mechi za Kariakoo Dabi ilikuwa ni maumivu. Mechi mbili za ligi 2024/25 alifungwa nje ndani.

Mchezo wa mzunguko wa kwanza ilikuwa Simba SC 0-1 Yanga SC. Mzunguko wa pili ilikuwa Yanga SC 2-0 Simba SC. Ndani ya dakika 180 Fadlu alishuhudia akipoteza pointi sita uwanjani kwenye mechi za ligi.

Soma hii: Mo Dewji aibua jambo Simba SC

Katika Ngao ya Jamii 2024/25 alipoteza katika hatua ya nusu fainali. Ubao ulisoma Yanga SC 1-0 Simba SC. Fainali ya 2025/26 alipoteza Yanga SC 1-0 Simba SC.

Kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii goli la ushindi lilifungwa na Pacome Zouzoua. Nyota huyo alifunga goli pia kwenye mchezo wa ligi mzunguko wa pili 2024/25. Alichaguliwa kuwa mchezaji bora Juni 25 2025, Uwanja wa Mkapa.

Mrithi mikoba ya Fadlu Davids

Mgunda bosi
Juma Mgunda anatajwa kuwa mrithi mikoba ya Fadlu.

Taarifa zinaeleza kuwa kwa muda Juma Mgunda atainoa Simba SC. Hiyo ikiwa ni kuelekea kwenye mchezo wa kimataifa dhidi ya Gaborone United. Mgunda amekuwa akikabidhiwa mikoba mara kwa mara makocha wanapoondoka.

Seleman Matola ambaye ni kocha msaidizi huenda akakiongoza kikosi mchezo dhidi ya Fountain Gate. Katika Ligi ya Mabingwa Afrika ana adhabu ya kadi nyekundu. Jambo hilo litawafanya Simba SC kuwa na kocha kwenye benchi la ufundi ambaye hatakuwa Matola.

Mbali na Juma Mgunda inaelezwa kuwa Simba SC wapo kwenye mazungumzo na Julio ili awe kocha wa muda. Ikiwa watashindwa kumpata Julio Hemed Morocco naye jina lake linatajwa. Ni suala la kusubiri nanni atakuwa mrithi wa mikoba ya Fadlu.

Hitimisho

Fadlu Davids ameondoka Simba SC ikiwa ni mwanzo wa msimu wa 2025/26. Mchezo wa kwanza kwenye ligi Simba SC itakuwa nyumbani dhidi ya Fountain Gate. Kocha mpya anatarajiwa kutangazwa hivi karibuni.

image

Share this: