- Mchezo wa kwanza kwa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara ya NBC Yanga SC kuchezwa Uwanja wa Mkapa.
- Rekodi zinaibeba Yanga SC mbele ya Pamba Jiji FC kutokana na ushindi mkubwa waliopata katika mechi zilizopita.
- Francis Baraza Kocha Mkuu wa Pamba Jiji amebainisha kuwa hakuna presha watawakabili kwa umakini wapizani wao.
Rekodi zinaibeba Yanga SC mbele ya Pamba Jiji FC kuelekea kwenye mchezo wa leo Septemba 24 2025 Uwanja wa Mkapa. Katika mechi mbili 2024/25 Pamba Jiji FC ilipoteza zote kwa kufungwa. Ndani ya dakika 180 Wanajangwani walishinda nje ndani katika mechi za ushindani
Paisha Kindege cha SportPesa uvune mamilioni
Muda ni sasa kuvuna mamilioni ukipaisha Kindege cha SportPesa. Ushindi unakusubiri rubani usisite kupaisha kindege. Cheza sasa Aviator upate mgao wako.

Rekodi zinaibeba Yanga SC mbele ya Pamba Jiji

Wakiwa wanatarajiwa kukutana Septemba 24 2025, rekodi zinaibeba Yanga SC mbele ya Pamba Jiji. Wababe hawa kwenye mechi mbili zilizopita Yanga SC ilishinda nje ndani. Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza ilikuwa Yanga SC 4-0 Pamba Jiji FC na mchezo wa mzunguko wa pili, Pamba Jiji FC 0-3 Yanga SC.
Soma hii: Yanga SC vs Pamba Jiji FC Septemba 24 2025 Uwanja wa Mkapa
Rekodi za Yanga SC VS Pamba Jiji FC 2024/25 NBC
| Yanga SC | Pamba Jiji FC |
| Ushindi mechi mbili | Hakuna ushindi |
| Mabao yakufunga 7 | Imefungwa mabao 7 |
| Oktoba 3 2024/ Yanga SC 4 | 0 Pamba Jiji, (Uwanja wa Azam Complex) |
| Februari 28 2025/ Pamba Jiji FC 0 | 3 Yanga SC, (Uwanja wa CCM Kirumba) |
| Pointi 6 | Pointi 0 |
Kocha Mkuu wa Yanga SC Romain Folz kuhusu Pamba Jiji FC

Soma hii: Yanga SC vs Pamba Jiji FC Septemba 24 2025 Uwanja wa Mkapa
“Tunatarajia kukutana na upinzani mkubwa kutoka kwa wapinzani wetu. Kimsingi tunakwenda kucheza kwa bidii na kwa tahadhari kubwa. Nahitaji wachezaji wangu kuwa kuongeza umakini kila dakika wawapo uwanjani.
“Tunakwenda kucheza mchezo wetu wa tatu wa ushindani, kwetu ni mchezo muhimu sana na tumejiandaa kufanya vizuri. Tupo tayari kwenye kila idara. Tumepata Pre-Season bora ambayo itatusaidia kwenye mechi zetu,” amesema Folz.
Frank Assinki wa mchezaji wa Yanga SC kuhusu Pamba Jiji FC

“Sisi Wachezaji wapya tuna morali ya kufanya vizuri na kuisaidia timu yetu, kwa ujumla tumekaribishwa vizuri na tumeshafahamu Yanga SC inataka nini, kwa pamoja na wenzetu tupo tayari. Tunawaalika Wananchi kutuunga mkono.
“Sisi kama wachezaji tumejiandaa vizuri tangu tukiwa Pre Season hivyo tuko tayari kufanya tulichokifanyia mazoezi. Niwaomba mashabiki wa Yanga SC waje kwa wingi ili tuanze ligi na ushindi,” .
Francis Baraza Kocha Mkuu wa Pamba Jiji FC
Kocha Mkuu wa Pamba Jiji FC, Francis Baraza ameweka wazi kuwa hakuna presha. Kuelekea katika mchezo huo anaamini watacheza kwa utulivu. Aliongeza kwamba mbinu zitabadilika kulingana na wapinzani wao.
“Kila mchezo una mbinu zake hivyo hilo sitaliweka wazi kwa sasa. Kwa upande wa maandalizi kila kitu kipo sawa. Wachezaji wanatambua huu ni mchezo wa aina gani ambao tunakwenda kukutana nao.
“Tumetoka kupata pointi moja ugenini ulikuwa ni mchezo wa tofauti. Namna ambavyo tulikabiliana na wapinzani wetu Namungo FC itakuwa tofauti na mchezo wetu dhidi ya Yanga SC. Hawa ni mabingwa mara nne mfululizo nao kuna mbinu zao za kuwakabili hilo linafahamika,” amesema Baraza.
Kelvin Nashon mchezaji wa Pamba Jiji FC kuhusu Yanga SC

Kiungo mkabaji wa Pamba Jiji, Kelvin Nashon amebainisha kuwa hawana hofu. Nashon aliongeza kuwa wanahitaji matokeo mazuri. Matokeo ya mchezo uliopita dhidi ya Namungo FC wameyasahau.
“Tumetoka kupata pointi moja ugenini, yale matokeo tumesahau. Ambacho tunaangalia kwa sasa ni mchezo wetu wa mbele. Tunawaheshimu wapinzani wetu kikubwa ni kuona kwamba tunapata matokeo mazuri.
“Wao ni mabingwa hilo tunalifahamu lakini halitupi mashaka. Hatuna presha kwa kuwa tumeambiana kwamba kinachohitajika ni ushindi. Mashabiki wajitokeze kwa wingi kutushangilia.”
Hitimisho
Rekodi zinaibeba Yanga SC mbele ya Pamba Jiji kutokana na matokeo waliyopata msimu uliopita. Licha ya kupata ushindi haitoi matokeo ya jumla kwa Yanga SC kwenye mchezo wa leo. Pamba Jiji FC wamebainisha kwamba wapo tayari kwa ushindani.


