- Jeshi la Simba SC limemaliza programu ya maandalizi ya kabla ya msimu ‘Pre season’.
- Kikosi cha Simba SC kurejea Tanzania leo Agosti 28, 2025 usiku.
- Hitimisho: kituo kinachofuata ni Simba Day na Ngao ya Jamii
Mara baada ya kumaliza salama kambi yao ya kujindaa na msimu mpya ‘pre eason’, hatimaye kikosi cha Simba SC kurejea Tanzania leo Agosti 28, 2025 usiku. Simba SC wanatarajia kutua nchini kutokea Misri, ambapo waliweka kambi ya takribani mwezi mmoja. Mara baada ya kutua kikosi cha timu hiyo kinatarajiwa kuendelea na programu, za kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu ya NBC 2025/26 na mashindano mengine.
SOMA HII PIA: Simba Day Septemba 10 2025 | Ali Kiba kutumbuiza | Ubaya Ubwela pasua kichwa
Cheza na shinda mamilioni sasa na ‘Kindege’ cha SportPesa kwa kubonyeza picha hii chini

Kuhusu safari ya kikosi cha Simba SC kurejea Tanzania leo Agosti 28, 2025 usiku

Msafara wa viongozi, makocha, wachezaji wa Simba SC unaarifiwa kuwa tayari umeanza safari ya kurejea Tanzania. Kuendana na taarifa za watu wa karibu ambao wamesafiri na kikosi hiko wameeleza kuwa, kikosi kinatarajiwa kutua Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere majira ya saa 10 Alfajiri. Hii ni baada ya kukamilisha kambi ya pre-season ambayo ilikuwa katika miji ya Ismailia na Cairo.
SOMA HII PIA: Selemani Mwalimu rasmi atua Simba SC: Aungana na Sowah, Mukwala kuelekea Ligi Kuu ya NBC 2025/26
Tujikumbushe kwa ufupi kuhusu kambi ya Simba SC Misri

Kambi ya Simba SC ilianza mwanzoni mwa mwezi Agosti, ambapo ilikuwa na vipindi vya wiki nne vya mazoezi ya kiwango cha juu. Hii ililenga kuwapa wachezaji nguvu, nidhamu na mipango ya kimbinu tayari kwa michuano ya ndani na ile ya Afrika. Mazoezi hayo yalihusisha ratiba za mazoezi ya utimamu wa mwili ambayo yalifanyika ‘Gym’ kabla ya mazoezi ya mbinu yaliyofanyika Uwanjani. Kambi hii kwa ukubwa pia ililenga kuboresha mahusiano ‘Chemistry’ kati ya wachezaji wapya na wa zamani.
SOMA HII ZAIDI: Simba SC inasukwa timu imara kuelekea 2025/26 | Wachezaji wapya wameanza kufunga magoli
Mechi za kiirafiki za kiushindani wa Kiufundi

Ingawa bado ripoti kamili juu ya mechi walizocheza Misri hazijatolewa. Imethibitishwa kuwa Simba SC imefanikiwa kucheza mechi takribani 5 za ushindani na timu mbalimbali za madaraja mbalimbali ya ligi za Misri. Mechi hizi zililenga kuangazia maendeleo ya namna gani wachezaji wanapokea mbinu za Mwalimu.
Huu hapa usajili mpya wa Simba SC

Simba SC imeongeza nguvu kwenye kikosi chao, hii ni baada ya kuleta wachezaji wenye thamani kubwa kwenye dirisha hili la usajili. Miongoni mwao ni: Rushine de Reuck raia wa Afrika Kusini, ambaye amewahi kukipiga na Mamelodi Sundowns kwenye nafasi ya ulinzi.
Alassane Kanté kiungo mchezeshaji aliyejiunga na Simba kutokea Athlétique Bizertin ya Tunisia. Staa huyu ana ubora mkubwa linapokuja suala la kuzipa uwiano safu ya ulinzi na ile ya ushambuliaji. Jonathan Sowah, huyu ni mshambuliaji rai awa Ghana ambaye amejiunga na Simba kutoka Singida Black Stars. Tayari jina la staa huyo limeimbwa sana huko Misri baada ya kuibuka shujaa, akifunga kwenye baadhi ya michezo ya kujipima nguvu.
Mohamed Bajaber, huyu ni kiungo mshambuliaji kutokea akisaini Simba baada yakumalizana na waajili wake wa zamani kikosi cha Kenya Police. Naye ni miongoni mwa wale walioanza kuonyesha cheche akiwa Misri, ambapo amefunga moja ya mabao makali. Aidha, Simba waliimarisha safu yao ya kiungo kwa kusajili wachezaji kama Neo Maema, Selemani Mwalimu,Morice Abraham, Hussein Semfuko, Anthony Mligo na wengineo.
Tathmini ya Kocha Fadlu Davids na Kikosi kipya
Taarifa kutoka kambi ya Simba zinasema kocha Mkuu wa Simba, Fadlu Davis amevutiwa sana na Chemistry ya haraka ambayo Sowah na Bajaber wameionyesha. Nyota hao wawili wameonekana kuzoeana kwa urahisi na nyota wengine. Walianza kung’ara tangu mechi yao ya kwanza ya kirafiki.
Uzoefu wa Rushine na Kanté umeelezwa pia kuchangia usawazo wa kutimiza maagizo ya kocha Fadlu, ambaye ameeleza wazi kwamba usajili huu unalenga kuleta ushindani katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika
Hitimisho: kituo kinachofuata ni Simba Day na Ngao ya Jamii

Baada ya kambi ya takribani wiki nne pale Misri na Kikosi cha Simba SC kurejea Tanzania leo Agosti 28, 2025 usiku, sasa Simba SC wanatazamia kuuanza rasmi msimu wa 2025/26 kwa matukio makubwa mawili. Tukio la kwanza ni kilele cha siku ya Simba maarufu ‘Simba Day’ ambayo inatarajiwa kuwa Septemba 10, mwaka huu. Baada ya tukio hilo litafuata tukio la mchezo wa Ngao ya Jamii ambao umepangwa kupigwa 16, Septemba mwaka huu.

