Simba Day ----Simba Day ----
  • Ni msimu wa 17 tangu kuanzishwa kwa tamasha kubwa la Simba Day.
  • Makala hii ya Simba Day inatarajiwa kufanyika Jumatano Septemba 10, 2025 likitarajiwa kufunika.
  • Simba SC vs Gor Mahia FC, moto utawaka kwa Mkapa, katika burudani hii ya soka.
  • Video ya Mbosso akianguka baharini yashtua, kufanya tamasha kesho?

Mambo yameiva ndani ya Simba SC, ambapo kesho Jumatano Septemba 10, 2025 wanatarajia kufanya tamasha kubwa la Simba Day. Pamoja na burudani nyingine mechi kali ya Simba SC vs Gor Mahia FC ndiyo inasubiriwa kwa hamu. Tamasha mwaka huu litafanyika Uwanja wa Mkapa, huku msanii Mbosso akipewa jukumu kubwa la kutumbuiza.

SOMA HII PIA: Jezi mpya Simba SC 2025/26 uzinduzi Agosti 31, 2025 wafana | Serikali yatoa maagizo mazito

Cheza na ushinde mamilioni leo kwa kupaisha Kindege cha SportPesa (bonyeza picha hii chini)

image

Alichosema semaji Ahmed Ally kuhusu Simba SC vs Gor Mahia FC tamasha la Simba Day 2025

Semaji
Semaji

Akizungumzia maandalizi ya tamasha hilo, Meneja Habari na mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amesema: “Septemba 10, 2025 ni Simba Day. Ni wazi mara nyingi Simba Day inafanyika wiki ya kwanza ya mwezi wa nane. Lakini kutokana na kubanana kwa ratiba na hasa mashindano ya CHAN imefanya imesogea hadi mwezi wa tisa.

Burudani ya kihistoria

Semaji alivyoingia
Semaji alivyoingia

“Ndugu zangu mwaka huu tumewaandalizia mambo makubwa yani unaingia unakuta burudani, na hadi unatoka unapata burudani. Natoa agizo kwa Matawi yote ya Simba ni marufuku Simba Day kuwasha TV ya tawini. Wanachama wote waje uwnajani. Shughuli pekee ya tawini ni kukutana asubuhi, ili kwenda uwanjani.

“Hata mwezi Septemba pia haikuwa rahisi kupata tarehe sababu ya ratiba. Tukiwa tunaingia msimu huu wa 17 tumeanzisha utamaduni wa kufanya uzinduzi wa Wiki ya Simba nje ya Dar es Salaam. Mwaka jana ilikuwa Morogoro na mwaka huu tumezindua mkoani Iringa,” amesema Ahmed.

Simba Day
Simba Day

SOMA HII ZAIDI: Ligi Kuu ya Tanzania 2024/25: Muhtasari wa Msimu

Usajili wa mastaa wapya Simba SC wampagawisha Semaji

Utatu wa ushambuliaji Simba SC
Utatu wa ushambuliaji Simba SC

Kuhusu mastaa wapya waliosajiliwa Simba, Ahmed amesema: “Heshima ya Simba Sports Club inakwenda kurudi msimu wa 2025/26, tumechoka kushikwa sharubu na watoto wadogo. Mnyama anarudi kwenye ufalme wake. kwa usajili tulioufanya niwahakikishe Wanasimba msimu huu ni Ubaya Ubwela Part Two.

“Hii Simba tunayozungumzia hapa imesajili mchezaji kutoka Mamelodi Sundown, tumesajili mchezaji kutoka Wydad, tumesajili mchezaji kutoka Tunisia. Wachezaji ambao tumesajili msimu huu kwanza wana uwezo mkubwa sana na wana uzoefu. Ni wachezaji ambao tunaamini kwa njaa yao ya mafanikio itakwenda kutuvusha msimu huu.

“Timu yetu imekamilika. Mkiangalia golini kuna Moussa Camara na tumemuongezea kijana mwingine bora bado hatujamtambulisha. Upande wa kulia upo sawasawa na upande wa kushoto tumeleta watu bora zaidi, hawezi kupita binadamu wa kawaida. Mabeki wa kati ya uwanja hapo kuna hatari kwanza Chamou amebaki, Hamza bado yupo kufanya kazi zake za kistaarabu lakini tumemsajili mtu anaitwa The Rock. Acha nisimalize utamu, tukutane Simba Day.

“Katikati yupo Kagoma lakini tumemuongezea mtu anaitwa Kunta Kinte. Ila eneo la mbele ndio kuna balaa zaidi. Kuanzia kwa Ahoua, Neo Maema, Mpanzu, sijamtaja Sowah, mfalme Gomez, itoshe kusema mwaka huu timu tunayo. Majonzi tuliyopitia kwa miaka minne huu ndio mwisho wake.”

Kocha Fadlu aukubali mziki wa kikosi chake kipya

Simba SC vs Gor Mahia FC
Fadlu Davids Head

Kocha Mkuu wa Simba, Fadlu Davids ameweka wazi kuwa ameridhika na kikosi chetu kuelekea kuanza kwa msimu mpya wa mashindano 2025/2026. Fadlu amesema msimu uliopita ulikuwa ni kwa ajili ya kujenga msingi wa kikosi. Kocha huyo amesema sasa wana  timu imara, ambayo inaweza kufanya vizuri kwenye mashindano ya ndani na nje.

“Tunategemea kuwa na msimu mzuri zaidi ya uliopita, tumefanya usajili mzuri kwenye kila eneo. Baada ya juzi dirisha la usajili kufunga nimeridhika na aina ya kikosi nilichonacho. Natarajia mambo makubwa msimu huu.”

Hitimisho: Video ya Mbosso kuanguka baharini yashtua

Mbosso
Mbosso

Kwenye burudani, Simba walimtangaza msanii mkubwa ambaye ataimba kwenye tamasha la Simba Day. Mwaka huu wamemeleta msanii ambaye hajawahi kuimba Simba Day. Msanii huyo ni Mwanasimba. Msanii wa Simba Day 2025 ni Mbosso.

Katika kile kilichoshtua wengi msanii huyo leo Jumanne ‘ameshare’ video ikimuonyesha akipata ajali ya kuanguka. Hii imefanya wanasimba wengi kushtuka na kuingia hofu ikiwa ataweza kupafomu kesho. Lakini hakuna taarifa yoyote rasmi kuelezea tukio hilo.

SOMA HII PIA: Simba SC imepishana na mataji mawili makubwa siku 14, Kariakoo Dabi yayeyuka mazima

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.