Fadlu -Fadlu -
  • Simba SC kwenye fainali ya CAF dhidi ya RS Berkane ilipishana na taji hilo kubwa Afrika kwa kufungwa jumla ya mabao 3-1.
  • Singida Black Stars wamewafungashia virago Simba SC kutinga hatua ya fainali kupambania taji la CRDB Federation Cup kwa kuwafunga jumla ya mabao 3-1.
  • Kariakoo Dabi iliyokuwa inasubiriwa kwenye CRDB Federation Cup imeyeyuka mazima kwa kuwa Simba SC kashindwa kupenya hatua inayofuata.

Simba SC imepishana na mataji mawili makubwa ndani ya siku 14 Mei 2025 kutokana na kushindwa kupata matokeo katika mechi muhimu walizoshuka uwanjani kusaka ushindi ndani ya dakika 90 kwa wapambanaji kupambania kombe.

Fadlu Davids
Fadlu Davids, Kocha Mkuu wa Simba SC. Source: Simba SC.

Taji kubwa la kwanza ambalo Simba SC ilipishana nalo ni lile la Kombe la Shirikisho Afrika ambapo kwenye mechi mbili ambazo ni dakika 180, Simba SC ilipoteza kwa jumla ya mabao 3-1. Ilianza kufungwa ugenini kisha ikatoshana nguvu na wapinzani wao wa CAF wakiwa nyumbani.

Kombe la kwanza kupishana na Simba SC

Mchezo wa kwanza ugenini ilikuwa ni Mei 17 2025 nchini Morocco ubao ulisoma RS Berkane 2-0 Simba SC na ule mchezo wa pili ambao uliamua mshindi wa jumla ulichezwa Tanzania, baada ya dakika 90 ubao ulisoma Simba SC 1-1 RS Berkane.

Wakati Simba SC ikipishana na taji la Kombe la Shirikisho Afrika ilikuwa na kete nyingine ya hatua ya CRDB Federation Cup ikiwa hatua ya nusu fainali. Simba SC walikuwa na dakika 90 kupata ushindi ili kucheza hatua ya fainali kuwania kombe jingine.

Mutale vs RS Berkane
Joshua Mutale kwenye mchezo wa fainali ya pili dhidi ya RS Berkane. Source: Simba SC.

Ngoma ilikuwa nzito kwenye mchezo huo ambao ulichezwa Mei 31 ikiwa ni funga mwezi walipopoteza kwa kufungwa jumla ya mabao 3-1 ikiwa ni kipigo kikubwa wanapokea Simba SC kwenye mashindano hayo hatua ya nusu fainali.

Kombe la pili Simba SC inapishana nalo

Katika mchezo huo Simba SC ilikuwa inaingia uwanjani ikiwa imetoka kupoteza taji la kwanza mbele ya RS Berkane. Hivyo kupoteza mchezo dhidi ya Singida Black Stars kwa kufungwa mabao 3-1 ndani ya Mei 2025 kunaifanya timu hiyo kupishana na mataji mawili makubwa.

Kupoteza kwa Simba SC mbele ya Singida Black Stars kunafanya Kariakoo Dabi iliyokuwa inasubiriwa kwenye hatua ya fainali kuyeyuka mazima kwa kuwa tayari Simba SC amefungashiwa virago na Singida Black Stars kwenye hatua ya nusu fainali.

Fainali ya CRDB Federation Cup inatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Amaan, Zanzibar ambapo ni watani wa jadi wa Simba SC, Yanga SC vs Singida Black Stars wanatarajiwa kushuka uwanjani kumsaka bingwa mpya na bingwa mtetezi ni Yanga SC.

Kete za Simba SC  zilivyopigwa

Simba SC 1-3 Singida Black Stars, Mei 31 2025

Simba SC 1-3 Singida Black Stars, Uwanja wa Tanzanite Kwaraa. Huu ulikuwa ni mchezo wa hatua ya nusu fainali CRDB Federation Cup ambao ulikuwa unatimiza siku ya 14 kwa Simba SC kupishana na taji kubwa la pili.

Mukwala Vs Singida BS
Mshambuliaji wa Simba SC Steven Mukwala kwenye mchezo dhidi ya Singida Black Stars. Source: Simba SC.

Katika mchezo huu Simba SC ilianza kufungwa kipindi cha kwanza kupitia kwa Jonathan Sowah ambaye ni mshambuliaji namba moja ndani ya Singida Black Stars. Huyu alimfunga kipa namba moja wa Simba SC, Moussa Camara.

Camara alikwama kukamilisha dakika 90 kwenye mchezo baada ya kupata maumivu na nafasi yake ilichukuliwa na Ally Salim ambaye ni kipa namba mbili yeye alifungwa mabao mawili na Emmanuel Kayeke ambaye alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo.

Inahusiana na hii: Simba SC 1-3 Singida Black Stars Mei 31: Magoli yote nusu fainali CRDB Cup, H2H, Fainali Yanga SC vs Singida Black Stars

Simba SC 1-0 Singida Black Stars, Mei 28 2025

Simba SC 1-0 Singida Black Stars, mchezo wa ligi Uwanja wa KMC Complex. Katika mchezo huu Simba SC ilivuna pointi tatu muhimu kwa bao lililofungwa na Steven Mukwala ambaye alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo. Mei 28 2025 ulichezwa.

Simba SC 1-1 RS Berkane, fainali CAF

Simba SC 1-1 RS Berkane, Uwanja wa New Amaan Complex. Huu ulikuwa ni mchezo wa hatua ya fainali ya pili iliyochezwa Tanzania. Katika mchezo huu Simba SC ilikuwa inapaswa kupata ushindi wa mabao 3-0 kwa kuwa mchezo wa ugenini ilipoteza.

Sare mbayo waliipata RS Berkane ilikuwa ni tiketi kwa RS Berkane kuwa mabingwa wa kombe la Afrika na Simba SC ikigotea kuwa washindi wa pili Afrika wakipoteza kwa jumla ya mabao 3-1. Mchezo huu ulichezwa Mei 25 2025.

RS Berkane 2-0 Simba SC, fainali CAF

Mei 17 2025, RS Berkane 2-0 Simba SC, hii ilikuwa fainali ya kwanza ambapo Simba SC ikiwa ugenini ilikubali kupoteza mchezo wa kwanza kwa kufungwa mabao 2-0. Kipa aliyeanza langoni alikuwa ni Moussa Camara alifunga mabao mawili ndani ya dakika 15.

Mechi zijazo kwa Simba SC

Yanga SC vs Simba SC

Bacca v Ateba
Bacca vs Ateba kwenye mchezo wa Kariakoo Dabi mzunguko wa kwanza. Source: Yanga SC.

Mchezo huu wa Kariakoo Dabi ni wa ligi unatarajiwa kuchezwa Juni 15 2025 ambapo awali ulitarajiwa kuchezwa Machi 8 2025 ukaahirishwa na Bodi ya Ligi Tanzania. Yanga SC ni wenyeji wa mchezo huu ambao wao wamekuwa wakieleza kuwa ni mechi mbili wanazitambua. Kwenye ratiba ya mechi ambazo Yanga SC imebakiwa nazo mchezo wa Kariakoo Dabi haupo kwenye orodha. Ni Tanzania Prisons na Dodoma Jiji hizi ndizo mechi ambazo Yanga SC inataja kuzitambua.

Soma hii: Yanga SC vs Simba SC inayodhamiriwa Juni 15 2025 Dabi ya Kariakoo mechi ipo, au haipo?

Ken Gold vs Simba SC

Juni 18 2025 ni Ken Gold vs Simba SC mchezo wa ligi ambao utakuwa ni mzunguko wa pili kwa wababe hawa kukutana uwanjani kwenye msako wa pointi tatu muhimu ndani ya uwanja katika mchezo wa ligi ambayo ni namba nne kwa ubora.

Simba SC vs Kagera Sugar

Funga msimu wa 2024/25 kwa wababe hawa wawili utakuwa ni mchezo wa Simba SC vs Kagera Sugar. Huu unatarajiwa kuchezwa Juni 22 2025. Ikumbukwe kwamba kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza Simba SC ilivuna pointi tatu mbele ya Kagera Sugar ambayo imeshuka daraja.

Msimu wa 2024/25 umekuwa na ushindani mkubwa kutokana na uwekezaji ambao umefanywa na timu nyingi. Timu mbili tayari zimeshuka daraja ikiwa ni Kagera Sugar na Ken Gold inayotumia Uwanja wa Sokoine kwa mechi za nyumbani.

Share this: