Yanga SC yashusha mashine hii nyingine usikuDoumbia Yanga
  • Zinahesabika siku kwa ajili ya tamasha kubwa linalotarajiwa kufanyika Uwanja wa Mkapa
  • Yanga Day kuna orodha ndefu ya wachezaji wapya kuelekea msimu wa 2026/27 wanaosubiriwa kwa shauku kubwa.
  • Zimbwe Jr wa Yanga SC anaingia kwenye orodha ya wachezaji wakubwa wazawa waliokuwa gumzo katika usajili.

Yanga Day ni Septemba 12 ikiwa ni Wiki ya Mwananchi. Zimebaki siku 2 tukio hilo kubwa likamilike. Hili ni tamasha maalumu kwa ajili ya utambulisho wa wachezaji wapya na wale waliokuwa katika kikosi msimu wa 2024/25.

Paisha Kindege cha SportPesa uvune mamilioni sasa

Ni rahisi sana kuvuna mamilioni ukipaisha Kindege cha SportPesa. Rahisi sana kupata mkwanja. Cheza sasa Aviator upate mgao wako.

image

Yanga Day wanasubiriwa kutambulishwa wapya  

Yanga Day kuna wachezaji ambao wanasubiriwa kwa shauku kutambulishwa. Hii inatokana na kuwa ni wapya ndani ya kikosi hicho. Pia ni siku maalumu ambayo watakuwa uwanjani na uzi mpya wa Yanga SC kuashiria kuanza kwa pazia jipya la ligi ya NBC 2025/26.

Ecua Elastin

Ecua Celestin
Ecua Celestin nyota mpya wa Yanga SC 2025/26.

Soma hii: Yanga SC imetambulisha wapya 10 dirisha la usajili

Huyu Agosti Mosi 2025 alitambulishwa Yanga SC kwa dili la miaka miwili. Msimu wa 2024/25 alikuwa anacheza Zoman FC alifunga magoli 15 na pasi 12 za magoli. Rekodi hizo ni kwenye mashindano yote. Yeye ni raia wa Ivory Coast.

Doumbia

Agosti 3 2025 Yanga SC ilimtambulisha kiungo, Mohamed Doumbia. Nyota huyu ana umri wa miaka 26 amejiunga na Yanga SC kutokea FC Slovan Liberec ya Jamuhuri ya Czech. Anatajwa kuwa na uwezo kwenye majaribio ya mashuti ya mbali na kutengeneza nafasi za mabao kwa wengine.

Anatajwa kurithi mikoba ya Aziz Ki. Ikumbukwe kwamba Aziz Ki msimu wa 2024/25 alikuwa ndani ya Yanga SC yupo kwenye changamoto mpya. Ni Wydad Casablanca ya Morocco nyota huyo yupo.

Sifa kubwa ya Aziz Ki ni mashuti ya mbali na mapigo huru. Msimu wa 2023/24 alichaguliwa kuwa MVP wa ligi ya NBC, kiungo bora. Mbali na tuzo hizo alitwaa tuzo ya ufungaji bora baada ya kufunga mabao 21.

Boyeli

 Yanga SC walifunga ukurasa wa Julai 31 2025 kwa kumtambulisha Andy Bobwa Boyeli. Nyota huyo mwenye miaka 24 alikuwa anacheza Sekhukhune United ya Afrika Kusini kwa mkopo kwa msimu mmoja. Julai 31 alifunga ukurasa kwa wachezaji waliotambulishwa Julai.

Lassine Kouma

Utambulisho wake ni Lassine Kouma mchezaji mpya ndani ya kikosi cha Yanga SC. Huyu ni mrithi wa mikoba mikoba ya Khalid Aucho. Kasajiliwa Yanga SC akitokea Stade Malien.

Ni jezi namba 8 amekabidhiwa kuwa utambulisho wake akiwa Jangwani. Msimu wa 2025/26 uzi namba 8 ulikuwa ni utambulisho wa Khalid Aucho. Kiungo huyo mkabaji hatakuwa ndani ya kikosi cha Yanga SC baada ya mkataba wake kuisha.

Balla Conte

Balla Conte
Balla Conte nyota mpya wa Yanga SC.

Soma hii: Balla Conte amesaini rasmi Yanga SC na kutambulishwa kuelekea Ligi Kuu NBC 2025/26

Huyu usajili wake ulikuwa na mvutano mkubwa kwa kuwa alikuwa anatajwa kuwa kwenye rada za Simba SC. Julai 18 2025 Yanga SC ilimtambulusha Moussa Balla Conte. Ingizo hili jipya ni kutoka CS Sfaxien ya Tunisia yeye ni raia wa Guinea.

Offen Chikola

 Mkali wa kutumia mguu wa kushoto akiwa uwanjani kwenye majukumu yake ni njano na kijani. Anaitwa Offen Chikola alitambulishwa Yanga SC Julai 22 2025. Ni kandarasi ya miaka miwili. 2024/25 akiwa na Tabora United alifunga mabao 8 kati ya 28 yaliyofungwa na timu hiyo. Yanga SC inaingia kwenye orodha ya timu ambazo Chikola alizifunga msimu wa 2024/25.

Casemiro

 Jina lake ni Abdulnassir Mohamed maarufu kwa jina la Casemiro alitambulishwa rasmi Jangwani, Julai 23 2025. Ni mzawa ambaye atakuwa kwenye changamoto mpya. Anaingia kwenye orodha ya wachezaji wapya ndani ya kikosi cha Yanga SC chenye maskani yake Jangwani, Dar.

Ninju

Jina lake ni Abubakar Nizar Othuman, maarufu kwa jina la Ninju kutoka Azam FC alitambulishwa rasmi Julai 27 2025.

Romain

Ilikuwa ni Julai 23 2025 Kocha Mkuu wa Yanga SC Romain Folz alitambulishwa. Kocha huyo anabeba mikoba ya Miloud Hamdi aliyekuwa akikinoa kikosi hicho. Msimu wa 2025/26 atakuwa kwenye benchi la ufundi.

Zimbwe Jr

Zimbwe Kapten
Zimbwe Jr ingizo jipya Yanga SC.

Soma hii: Baada ya ‘Tshabalala’ na Conte Yanga SC yashusha straika Boyeli: Tetesi usajili Ligi Kuu ya NBC 2025/26

Mohamed Hussen beki wa kushoto alitambulishwa Yanga SC akitokea Simba SC. Huyu anasubiriwa na mashabiki kutokana na uwezo wake. Kuondoka kwake Simba SC kulikuwa na mvutano mkubwa kwani alikuwa nahodha hapo.

Mashabiki wanamsubiri kwa shauku utambulisho wake. Ikumbukwe kwamba alitambulisha akiwa katika majukumu ya timu ya taifa. Aliripoti kambini baada ya mashindano ya CHAN kwa mara ya kwanza.

Hitimisho

Yanga Day ni tukio kubwa ambalo linaambatana na burudani mbalimbali.Mbali na utambulisho wa wachezaji kuna mchezo wa kirafiki Yanga SC vs Bandari. Hii yote ni kufungua pazia la 2025/26.  

image
Share this: