- Meneja wa Habari na Mawasiliano Simba SC Ahmed Ally amewaambia mashabiki wasivae jezi za zamani siku ya Simba Day, Septemba 10 2025
- Hii ni kufuatia uzinduzi wa jezi mpya Simba SC 2025/26 ambao hapo awali ulitarajiwa kufanyika Agosti 27 2025 lakini uliahirishwa na terehe ilipelekwa mbele mpaka Agosti 31 2025.
- Simba SC rasmi imezindua jezi mpya ikiwa ni maandaalizi kuelekea msimu mpya wa 2025/26.
Jezi mpya Simba SC 2025/26 zimezinduliwa kwa kishindo na mwitikio mkubwa wa mashabiki. Uzinduzi huo umeacha historia ukiwa ni tofauti na msimu wa 2024/25 walipozindulia Mikumi. Agosti 31 2025 uzinduzi ulifanyika katika ukumbi wa Super Dome, Masaki na mgeni rasmi alikuwa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Gerson Msigwa.
Paisha Kindege cha SportPesa ushinde mamilioni
Muda wako sasa kupaishia Kindege cha SportPesa na ushinde mamilioni. Rahisi sana cheza Aviator ushinde.Mgao upo kila siku unakungoja.

Ahmed Ally kuhusu uzinduzi jezi mpya Simba SC 2025/26

Soma hii:Mfungaji bora wa muda wote John Bocco na Jonas Mkude kupewa tuzo Simba Day
Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC, Ahmed Ally amesema kuwa uzinduzi wa jezi mpya umefanywa kimataifa. Aliongeza kuwa kila Mwanasimba na asiye Mwanasimba ni muda wa kufurahia jezi mpya. Amesisitiza wahakikishe wananunua jezi Original.
“Ubora wa tukio umefanywa katika hadhi yake. Tumefanikiwa kwa asilimia kubwa na watu wametoa viingilio vikubwa. Bila shaka watu wamejionea jezi zao za Simba SC ambazo bila shaka hii ni jezi bora kuwahi kutokea katika maisha yetu ya Simba SC.
“Wazabuni wote wa Simba SC wamefanya kazi kubwa. Ukitazama jezi ambayo alituvalisha Vunjabei ilikuwa ni jezi bora. Hivyo kila mzabuni anakuja na ubora wake. Ubora haupaswi kufanana ila unapaswa kuzidi kutofautiana na kupanda juu.
“Ni jezi ambayo huwezi kuiona popote na kitambaa chake ni cha hali ya juu. Simba SC ni ya kimataifa. Tunaingia kwenye timu ambazo zinavaa jezi bora.
“Kuhusu jezi ambazo zilivuja mimi sijui kuhusu zile jezi. Macho yangu yamejikita kwenye hizi jezi mpya. Nilisema wakati ule kama jezi ile iliyovuja licha ya kupigwa picha kwenye kamera ambayo ni mbovu, watu wanaweza kutofautisha ubora.
“Simba Day tunavaa jezi ya mnyama mpya. Na ninapenda kuona kwamba Simba Day hakuna mtu anayekuja na jezi ya zamani. Kuna raha kubwa kuwa na jezi hii mpya ambayo ipo kwa sasa. Hata wale ambao hawana timu ninawakaribisha wanunue jezi za Simba SC,” amesema Ahmed Ally.
Mgeni rasmi Gerson Msigwa atoa maagizo mazito

Katika tukio la uzinduzi wa jezi za msimu wa 2025/26 Agosti 31 2025, ukumbi wa Super Dome, Masaki mgeni rasmi alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Gerson Msigwa. Msigwa amesema ni muhimu mashabiki wa Simba SC kuhakikisha kuwa wanapata bidhaa original na sio feki .
Amebainisha kuwa anatambua gharama zilivyo kweye kuendesha timu. Katika kuhakikisha mipango inakwenda sawa lazima mashabiki wanunue vifaa. Miongoni mwa vifaa hivyo ni jezi ambazo ni mpya.
“Kwa niaba ya Serikali ninapenda kuwapongeza wawekezaji wote waliofanikisha jambo hili. Michezo inahitaji pes ana michezo haihitaji manenomaneno. Nimefurahi kuona namna ambavyo uwekezaji unafanyika.
“Hakuna ubishi ni lazima kuwaheshimu wadhamini. Niliwahi kuwa kiongozi wa Majimaji, chamoto nilikiona. Tulikuwa tunapeleka sembe kwa ajili ya kula wachezaji kwa sababu hatukuwa na pesa.
“Mnaposoma habari mchezaji amenunuliwa kwa bei fulani ni pesa. Hizo pesa zinatoka kwa wawekezaji. Jambo lingine nit imu inapozindua jezi ni muhimu kununua vifaa vya timu. Kuendesha timu sio kitu kidogo.
“Sibahatisha na ninaelewa. Mimi ninalea timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars. Kulea timu sio kitu kidogo. Hapo ujue kwamba ninakaa na timu kwa muda mfupi.
“Tuache kuhujumu timu zetu. Moja ya hujuma kubwa ni kununua vifaa ambavyo ni feki. Tukatae kununua vifaa feki. Kwa hiyo ninawaomba sana tuacha kununua vitu feki.
“Mwanasimba sema mwenyewe moyoni mwako kwamba sitanunia jezi feki. Uzuri safari hii kuna QR Code. Kwa kununua vitu halisi itaongeza thamani kwa timu na kujenga viwanja bora,”.
Agosti 27 mpango kazi ulikwama awali
Awali mpango kazi wa uzindi wa jezi mpya za Simba SC ulitarajiwa kufanyika Agosti 27 2025. Kutokana na sababu za kitaalamu tukio hilo lilisogezwa mbele. Tarehe mpya iliyopangwa ilikuwa ni Agosti 31 2025 ambayo hiyo haikusogezwa mbele.
Burudani yatolewa na King Kiba

Soma hii: Simba Day 2025 msimu wa 17 viwango vingine
Katika uzinduzi wa jezi mpya za Simba SC kulikuwa na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali. Miongoni mwa waliotumbuiza ni mfalme, Ali Kiba. Mbali na Kiba pia Yammi mwanadada mrembo mwenye sauti laini alitumbuiza.
King Kiba baada ya kutoa burudani akikonga nyoyo za Wanasimba alizungumza kidogo kuhusu jezi mpya. Msanii huyo mkubwa Tanzania na Afrika alisema jambo lililofanyika ni kubwa. Aliongeza kuwa ni mud awa furaha ya Wanasimba kuendelea.
“Nimeona namna ambavyo jezi mpya za Simba SC zimezinduliwa. Ni jezi nzuri ambazo zinampendeza kila mtu. Hakika hili ni kubwa na kila mmoja anapaswa kujivunia.
“Wanasimba furaha kubwa ni kwenye kupata jezi mpya. Hakika kila mmoja atakuwa na furaha na huu ni mwanzo. Hatukuwa na matokeo mazuri wakati uliopita lakini huu ni msimu mwingine,” alisema Kiba.
Hitimisho
Uzinduzi wa jezi mpya Simba SC 2025/26 umekuwa gumzo kila kona kutokana na ubora wake. Katika jezi tatu rangi ya bluu inatajwa kupendwa zaidi. Tayari kwa sasa jezi zinapatikana Tanzania nzima.

