- Hii ni mara ya sita kwa timu hizi kukutana, licha ya historia ya kukutana kwao kuanzia 1933.
- Spain imeshinda mechi nne, imepoteza mara moja na mechi moja ilimalizika sare ya 1-1 ilikuwa kwenye Euro 96.
- Bulgaria vs Spain 4/9/2025, makala hii inakuchambulia takwimu za vikosi, h2h, habari za timu n.k
Bulgaria na Spain kesho Alhamisi, wanatarajia kufungua mechi zao za kufuzu kuelekea Kombe la Dunia la FIFA 2026. Hii ni kwa ukanda wa UEFA katika kundi gumu E, linalowajumuisha pia Timu za Uturuki na Georgia. Michezo hii inatarajiwa kupigwa katika kipindi cha mapumziko ya ligi kupisha mechi za kimataifa.
Bado haujashinda kindege? Cheza na ushinde mamilioni leo kwa kupaisha Kindege cha SportPesa (bonyeza picha hii chini)

Kuhusu mechi ya Bulgaria vs Spain 4/9/2025

Soka la Ulaya linaelekeza macho yake kwenye mchakato wa michezo ya kufuzu kwa Kombe la Dunia la FIFA 2026. Huku ushindani ukiwa mkali zaidi kwa mataifa mbalimbali, katika mchakato wa kusaka tiketi za mashindano hayo makubwa zaidi duniani. Ikumbukwe Kombe la Dunia 2026 linatarajiwa kuandaliwa na nchi za Marekani, Canada na Mexico.
Mchakato wa mechi hizi huathiriwa kwa kiasi kikubwa na mwenendo wa mechi za Nations League, za mwezi Machi na Juni. Tangu kuanzishwa mashindano ya Ulaya, timu zinazofika hatua za mwisho, hujiunga na mchakato wa kufuzu Kombe la Dunia baadaye. IkumbukweUreno walitwaa ubingwa baada ya kuishinda Spain kwa penalti 5-3, kwenye fainali ya 2025 mwezi Juni.
SOMA HII PIA: Spain vs Brazil: Preview, Team News & Prediction 23/24
Bulgaria vs Spain h2h
Hii ni mara ya sita kwa timu hizi kukutana, licha ya historia yao kuanzia 1933. Spain imeshinda mechi nne, imepoteza mara moja na mechi moja ilimalizika sare ya 1-1 kwenye Euro 96. Katika mchezo huo mshambuliaji nyota wa zamani wa Bulgaria, Hristo Stoichkov alifunga kwa penalti kabla ya Alfonso Perez kusawazisha kwa Spain. Mechi ya kwanza kabisa iliisha kwa Spain kushinda 13-0 mwaka 1933.
Mechi yam waka huu, ni mechi ya kwanza kati ya mataifa haya tangu 2002. Mara ya mwisho kukutana Spain ilishinda bao 1-0 kwenye mechi ya kirafiki. Mechi yao ya mwisho ya ushindani ilikuwa Kombe la Dunia la mwaka 1998 nchini Ufaransa, ambapo Uhispania ilishinda 6-1.
Taarifa za vikosi vya timu zote mbili
Kwa upande wa Bulgaria, mtihani mgumu ni kuchagua kipa wa kuanza. Kati ya Dimitar Mitov wa Aberdeen na Svetoslav Vutsov wa Levski Sofia wanawania nafasi hiyo wote wamekuwa kwenye fomu. Bulgaria wanatarajiwa kutumia mfumo wa mabeki watano, kujaribu kuzuia mashambulizi ya Spain.
Kwa upande wa Spain wachezaji Gavi (Barcelona), Fabian Ruiz (PSG), na Yeremy Pino (Crystal Palace) watakosa mechi kutokana na majeraha. Kiungo wa Bayer Leverkusen Aleix Garcia na mshambuliaji wa Rayo Vallecano, Jorge de Frutos wameitwa kuchukua nafasi zao.
Kikosi cha kwanza cha Bulgaria kinachotarajiwa

Mitov; Minkov, Dimitrov, Petkov, Nedyalkov, Nurnberger; Despodov, Shopov, Gruev, Milanov
SOMA HII ZAIDI: Madrid vs Barcelona moto utawaka leo weka mkeka wako SportPesa
Kikosi cha kwanza cha Spain kinachotarajiwa

Simon; Porro, Le Normand, Huijsen, Cucurella; Pedri, Zubimendi, Olmo; Yamal, Williams, Oyarzabal
Taswira ya Kundi E
Kundi E la kufuzu Kombe la Dunia ukanda wa UEFA lina timu nne ambazo ni Spain, Bulgaria, Uturuki na Georgia. Kuna makundi sita yenye timu nne, ambayo ndiyo yameanza kampeni zao sasa. Pia kuna makundi mengine sita yenye timu tano, ambayo tayari yamecheza mechi nne.
Mfumo wa kufuzu
Timu ya kwanza katika kila kundi itafuzu moja kwa moja Kombe la Dunia la msimu ujao. Timu ya pili itaingia mtoano, ili kutafuta nafasi. Katika makundi yenye timu nne, timu mbili zitafungashwa virago. Katika makundi yenye timu tano, timu tatu zitafutwa.
Washindi wa pili 12, kutoka kwenye makundi ya sasa wataungana na timu nne bora kutoka makundi ya Nations League. Timu hizi ni zile ambazo hazitafuzu moja kwa moja, kwenye hatua ya mtoano mwezi Machi. Hii inalenga kutoa nafasi ya pili, kwa timu ambazo huenda zikapata matatizo kwenye makundi yao ya sasa.
Mechi za mtoano wa Kombe la Dunia 2026 zitafanyika vipi?
Timu 16 za Ulaya zitagawanywa kwenye makundi manne ya mtoano yenye timu nne kila moja. Kila kundi litacheza nusu fainali na fainali ya mtoano kwa mchezo mmoja tu, tarehe 26 na 31 Machi. Timu nne zitafuzu kwa Kombe la Dunia.
Je, kundi la Spain ni gumu zaidi?

Baada ya Spain kuifunga Uholanzi kwenye robo fainali ya Nations League mwezi Machi, ikajikuta ikiingia moja kwa moja Kundi E. Georgia yenye winga wao hatari wa PSG, Khvicha Kvaratskhelia, ilikuwa timu hatari zaidi kati ya tatu kwenye droo. Georgia itaikaribisha Uturuki siku ya Alhamisi na kisha itacheza dhidi ya Uhispania Oktoba 11. Lakini hii haitoshi kulipa hadhi ya Kundi gumu.
Hitimisho: Kundi gumu zaidi ni lipi?
Wachambuzi wa soka la Ulaya wanasema kundi gumu zaidi kutabiri ni lile la timu nne za; Uswisi, Uswidi, Slovenia na Kosovo. Uswisi ilifika robo fainali ya Euro 2024 na inaundwa na washambuliaji ghali zaidi barani Ulaya, Benjamin Sesko (Man United), Alexander Isak (Liverpool), na Anthony Elanga wote wakigharimu zaidi ya $300 milioni msimu huu.
SOMA HII PIA: Athletic Club Bilbao – Muhtasari, Historia ya Klabu, Kikosi cha Wachezaji, Ratiba, Matokeo, Takwimu, Tuzo na Habari Mpya

